Acha Kujilinganisha Na Wengine


BlackBusiness-630x334 Acha Kujilinganisha Na Wengine

Ingawa tunaishi katika  hali ya kujilinganisha au kujifananisha , Hii hali itahitaji mafunzo makini ya ubongo, lakini kusema kweli unahitaji kuacha tabia hii mbaya ya kujifananisha na mwingine

Acha kuingiza sumu hii mbaya kwenye ubongo wako na kwenye roho yako unapojilinganisha  na wengine. Hiki kitu kinatokea wakati tunapohitaji mafanikio katika  umri wetu, katika ndoa zetu,  kumiliki mali na  kuwa na watoto kwa kutamani na kutaka kuwa kama wengine

Kusema kweli ni kwamba kujilinganisha unapoteza uwezo wako  mwenyewe, unaweka uwezo wako katika mikono ya mwingine. kutaka kitu kama walichonacho watu wengine.  Kusikiliza kuhusu watu wanasema nini juu ya maisha yako. kutoridhika na ulicho nacho.

Tambua kuwa kila mtu ana safari yake tofauti. hatulingani. Kuna mtu anaweza kufanikiwa akiwa na miaka 21.  Wengi wanaweza kufanikiwa wakiwa na miaka 41. Kila mtu hupata mwenza amtakaye kwa wakati tofauti. na kupata watoto kwa wakati tofauti.  Kujilazimisha kuamini kuwa ni lazima kuolewa chini ya miaka 30, ni kitu cha kijinga na kitakupa mawazo na hata kuchanganyikiwa. kama mtu amefanikiwa katika umri huo ni yeye sio wewe.  Au kutaka kuoa mapema hata bila ya kupata kazi , nyumba, hio sio akili hata kidogo.  Fuata moyo wako. kama ukiwa tayari  fanya . kama bado usiige mtu. subiri wakati wako utafika.

Maisha ni zaidi ya kuoa au kuolewa. na ni zaidi ya mafanikio unayojilinganisha nayo. Maisha ni kuhusu kuwa mtu bora.. Ni kumkubali kila mtu ambaye anakuja na kuondoka katika maisha yako. Ni kuishi maisha ya ukamilifu.  Ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo. Ni kuhusu kumpenda mtu ambaye sio sahihi, wakati mtu ambaye ni sahihi  atakuja wakati ambapo umejifunza kuwakubali watu. Ni kuhusu kujiweka tayari katika changamoto utakazokabiliana nazo.

Na hutaweza kufanikisha haya kama utakuwa mtu wa kuogopa kwamba hujafanya kitu  ambacho rafiki zako wamefanya tayari, au wazazi kukulazimisha kufanya kitu ambacho moyo wako hautaki kufanya.

Kwa hio Acha kabisa kusikiliza kila kitu, acha kujilinganisha na mtu mwingine yeyote. Tambua kuwa wewe ni wa tofauti, kila mtu ana wakati tofauti. Safari yako ni tofauti.

Maisha hayajaisha mpaka yatakapoisha, Maana yake kila mtu anaweza kurejesha  uwezo wake uliopo ndani yake. Hakuna mwisho, kama utaona mwisho tambua kuwa kuna kona, songa mbele usirudi nyuma, Hio ni kona tu, Utapita na utaona njia sahihi uliotarajia kwa kiasi.

Kama wewe umekuwa mtu wa kujilinganisha kwa kila kitu, na kila mtu. unajaribu hili unashindwa , unajilinganisha na mwingine pia. Unasikiliza watu wanasema nini , wanawaza nini juu yako.Huridhiki na ulichonacho, Tambua kuwa upo kwenye hivyo vizuizi.

Anza kurudi katika ufahamu wako. Kumbatia uhalisia wa msamaha wa Mungu, Usijihukumu, Jifunze kutokana na makosa yako, Rejesha muda uliopoteza kwa kujilinganisha. Anza Kujisamehe mwenyewe, komboa wakati, Badilisha mtazamo wako, kuwaza kwako, kutenda kwako. Weka akili yako vizuri. Tumia muda wako vizuri.

Fanya kitu unachokipenda, shauku ya moyo wako. Kitu ambacho utafanya bila ya kutumia jasho. Jitambue. Muhusishe Mungu, Pata  mtu ambaye utajifunza kwake. Hata kama ni ndoa, tafuta ni ndoa ipi ya kujifunza, Tafuta taarifa. Gundua vitu vipya.

Acha kuingiza sumu mbaya ya kujilinganisha na mtu, huyo sio wewe. Kumbuka kuwa wewe ni wa tofauti.

Mungu Akubariki.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

 

Previous Imani Inayovutika ( The elastic Faith)
Next Mambo 10 Ambayo Nimejifunza Kuhusu Upendo

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.