1-AZRQPlQh6-8p8k38ahDrAQ-1-1024x683 Advanced Mindset (Akili iliyopevuka)

Tuanze siku yetu, wiki yetu kwa kufahamu  akili iliyopevuka ni akili ipi.

Akili iliyopevuka inaona  fursa  katika kila hali, iwe kuna tatizi au hakuna tatizo. iwe kuna furaha au huzuni. Lakini akili iliyolala, inaona matatizo katika kila hali.

Ukitaka akili yako ipevuke , mwakilishe Mungu. Ongea maneno ambayo Mungu anapenda kuyasikia kutoka kwako, kwa sababu yeye amesema kuwa anaomba ufanikiwe kama roho yako ifanikiwavyo. Ufanikiwe kiakili, kimwili, kiuchumi, na kiroho.Hapo utapata usalama .

Aina Za watu.

1.Viongozi

2.Watumishi wa Mungu

3.Wafanya biashara

4.Super star

5.Watu wanaofikiri

6. Wajinga

7.Watu waoga.

Zipo sehemu 4 ambazo zinaweza kuwatengeneza watu hawa.

1.Nyumbani

2.Kanisani au msikitini

3.Shuleni

4.Barabarani.

Jiulize wewe umetengenezewa wapi?  Ukianzia nyumbani kwa wazazi wako au nyumbani kwako unawajengaje watoto wako. Unawajenga katika ujasiri au katika woga? unawajenga kuwa watu wema na wenye upendo?   unawafundisha kuwa na mahusiano mazuri? . Mnaenda kutafuta maarifa kanisani au msikitini?  mafunzo wanayopata shuleni yanakithi hali halisi ya mtoto wako? anajengwa katika kipaji alichonacho?  Akiwa huko barabarani anajifunza nini? Je anaenda  au wewe mwenyewe unaenda kwenye semina mbalimbali kupata maarifa? unajitahidi kutafuta  kinachokujenga au uko kwenye makundi ambayo yanakubomoa?

images-3 Advanced Mindset (Akili iliyopevuka)

Akili iliopevuka inaitwa fursa.Andaa akili yako ipate kuona fursa. kwenye fursa kuna Imani. hatuendi kwa woga tunaenda kwa imani. tafuta network ya watu wenye akili , wenye kufikiri  tembea nao, au jifunze kwao. jifanye mjinga ili kupata kitu unachokitaka. watu wenye akili ya kupevuka wanajifunza kila mara, hushuka, hujishusha ili kufahamu jambo. wanatumia muda wao vizuri.

Jaribu kukaa chini angalia ni sehemu gani umeingiziwa  hofu.woga, wasiwasi na ukashindwa kujitambua , umeshindwa kuona fursa. Ni wapi ulikoingiziwa hizo shida. Je ni nyumbani, kanisani, msikitini, shuleni au barabarani?  Ukijua, Anza sasa hivi kuondoa hofu, wasiwasi,  mashaka kwa kutafuta maarifa. Tafuta semina mbalimbali nenda kajifunze uondoe ujinga.

Uwe mtu wa Imani , Imani ni jicho la Mungu. Bila Imani huwezi kumpendeza Mungu. Hatuendi kwa woga bali kwa imani. Ukitaka kuwa na akili iliopevuka , jitahidi kutunza akili yako, nguvu zako, hisia zako, na fikra  au mawazo yako.

badilisha mitazamo yako, kuwa mtu wa mitazamo mizuri, kinywa cha ukaidi ukitenge mbali na wewe na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe. Kuwa mlinzi wa mawazo yako ili mtu asije akakuingizia mambo mabaya yakakubomoa. Kuwa makini na yale unayoyasikia, unayoyaona na kuyahisi, kuwa makini na matendo yako.

Mtazamo wako unachukua asilimia mia moja ya maisha yako. chunguza akili yako iko kwenye nini. Kila mwanadamu amejifungia roho ya aina yake.

Roho ya Pesa

Roho ya chuki

Roho ya Upendo

Roho ya ugonjwa

Roho ya mapepo

Mtazamo wako ndio unakuonyesha akili yako kama imekomaa au haijakomaa. Unaona nini, nini, Fursa au unaona matatizo? Jipime sasa.

Nakutakiwa mwanzo mzuri wa wiki yako iwe ya kujitofautisha.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here