AKILI YAKO ITAJUAJE KAMA KILA KITU KIPO KWA AJILI YAKO.


Inawezekana hujawahi kutambua kabisa kuwa kila kitu kipo kwa ajili yako.Yaani Afya, furaha, amani, upendo, pesa, heshima ,hekima na mengine katika maisha .
Mungu anasema kila kitu unachotaka,unachohitaji tayari unacho hata kabla hujaomba nimekupa vyote, lakini hujaelewa jinsi system inavyofanya kazi na huna uzoefu na hilo.
Hapa hata mimi palikuwa pananichanganya sana, hongera wewe ambaye ulikuwa tayari umegundua hili. Kwa sababu anasema kila kitu kinachotokea sasa kilikuwepo tayari ila ni wewe tu hujui na hukuona kuwa vipo.

Jukumu kubwa hapa ni kutambua aina tatu za vifaa ambavyo vinafanya kazi hio navyo ni ,

  • Mawazo au fikra.
  • Maneno.
  • Matendo.

Tumefungwa kwenye vitu hivyo, kitu tunachokifikiria, maneno tunayoongea, na kitu unachokifanya. Kwa mfano,
Mtu anasema kuwa Mungu nipe chakula cha leo, si ndio kitu unachowaza na kukitaka? Mungu jibu lake ni ndio umepata, Nahitaji pesa nyingi, ukweli hata mimi nahitaji pesa nyingi, lakini jibu lake ni hilo hilo ni kweli unahitaji pesa na umekuwa ukisema mara nyingi, Ugonjwa huu utaniua, ni kweli kabisa huo utakuua, Ndoa yangu mbaya, ni kweli ni mbaya, ndio ni mbaya, kazi hii siipendi,nimechoka na maisha haya, ndio umechoka na maisha hayo, ni kweli kabisa.

Majibu ya Mungu siku zote ni Ndio, hata kama ni kitu kizuri au kitu kibaya, Positive au Negative yeye ni ndio. Maana yeye ni wa kila kitu , wa kila mtu.
Kitu cha muhimu cha kuzingatia hapa ni katika Msingi wako wa mawazo.Najua si kitu rahisi kwa mtu ambae hana msingi mzuri wa mawazo yake, lakini nguvu huvuta kila kitu, ukiwa na nia ya kubadilika utaanza pale ulipo kuweka msingi ulio imara kwa sababu ni msingi wa kila kitu hapo.
Usihukumu kwa mwonekano.
Fuatilia kila siku makala zangu ujifunze namna ya kupata ufahamu utakaokusaidia katika kila sekta ya maisha yako.
Mimi tayari nimeanza ,Je wewe utaanza lini?”

Previous Mambo 10 Mazuri Ambayo Yatatokea Mara Tu Utakapoacha Kuwaza Kuhusu Watu Watanionaje
Next Uko Tayari Kujaribu Kitu Kipya?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.