aid1225971-v4-728px-Find-Healing-in-Forgiveness-Step-4 Anza Kusafisha Moyo Wako  Kupokea Yalio Mapya

Msamaha ni zawadi  tunayotoa kwa ajili yetu wenyewe.

Msamaha hauhusiani na jinai au uhalifu wa  makosa ya mtu. Ni kuhusu kuondoa mizigo ilopo ndani yako mwenyewe ili usiwe muathirika.

Niliwahi kusikia watu wakisema kuwa , Kukataa kusamehe ni sawa na kunywa sumu halafu utegemee mtu mwingine  augue . inaweza kuwa kweli, Tazama kwenye maisha yako mwenyewe jinsi ilivyo .

Mara nyingi tumetegwa katika Ulimwengu huu  kwa kujilaumu na Kujihukumu, Msamaha unaweza kuonekana kama ni kidonge  kichungu  kukimeza. Hasa kwa wale ambao wametendewa mambo mabaya  kama kubakwa, kupoteza, na kupata maumivu kwa ajili ya fulani. Kwa nini tuwasamehe wale waliotukosea? Kwa nini tusiwaache waondoke na walichokifanya?

forgiveness-quotes-in-english Anza Kusafisha Moyo Wako  Kupokea Yalio Mapya

 

Jibu ni : Ili kwamba tuweza kuwa na nguvu zetu wenyewe.

Kwa kufanya hivyo,Kwa pamoja tunahitaji kuwa na mitazamo tofauti  katika kusamehe kuliko kufuata mila na tamaduni  ambazo sio sahihi. Kwamba  kama una nguvu  ni kwa sababu unasamehe, lakini asiye na nguvu ni mtu asieweza kusamehe.

Ni kweli , Ukisamehe utaweza kuachilia mizigo na mambo yote yaliopita na kuendelea na yaliopo wakati huo. Ugumu upo pale kama hutaweza kujaribu kusamehe, hutaweza kupata urahisi  wa kutoka ulipo. Jaribu kwa bidii, sio tu kutumia muda  wa kutaka kuelewa hasara itakayotokea kwao, lakini ni kwa ajili yako ili uishi kwa furaha.

Unapokuwa na uelewa kama huu , itakuwa rahisi kwako kusamehe, mara nyingi utapata faida kubwa kuliko kama usingesamehe. utajikubali mwenyewe na utakuwa mtu mwenye amani nyingi kila wakati.  Uchaguzi ni lazima . Tazama kama unataka kubaki mtu wa lawama na kuhukumu  na kuwa muathirika katika  mazingira hayo , au  utajitia nguvu mwenyewe kwa kukubali kusamehe kwa kila kinachotokea usichokipenda mbele yako, au kufanyiwa vibaya na mtu , ili uwe huru katika maisha yako.

110 Anza Kusafisha Moyo Wako  Kupokea Yalio Mapya

Ukiona nyumbani , kazini kwako ,shuleni kwako , au katika mazingira yeyote uliyopo, kuna watu ambao wanakufanya usiwe na amani , kila wakati wanakukwaza. Anza sasa hivi kumwomba Mungu Kila baada ya dakika 60. Inapofika saa kamili mwombe Mungu, Omba toba fupi , sema nisamehe maovu yangu yote na uniponye na magonjwa yangu yote. Omba  Hekima, ufahamu, Uweza, Roho ya ushauri. Halafu omba Uwe na Upendo, Utu wema, Fadhili, Uvumilivu, Nidhamu, Uaminifu na Kiasi. mshukuru Mungu na Msifu Mungu. Atafanya wepesi katika mapito yako.

Ukiwa na hivyo vitu ndani yako , utakuwa na nguvu ya kushinda , nguvu ya kusamehe, nguvu ya kuvumilia, nguvu ya kutawala, na nguvu ya Kibali.

Toa maoni yako kusaidia wengine.

Subscribe ili kupata makala mpya mara kwa mara.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here