Anza Wiki Kwa Kuboresha Kazi Zako Na Hali Ya Akili Yako


kazini Anza Wiki Kwa Kuboresha Kazi Zako Na Hali Ya Akili Yako

Wakati ambapo bosi wako ni changamoto.

Utawezaje kuboresha kazi zako na  hali yako ya akili.

Mabosi wenye changamoto hufanya siku kuwa na matatizo mengi. Tayari inakuwa ni mbaya., mabosi hawa wanakuwa ndio gumzo  la watu wote  baada ya kazi , na wakati mwingine ndio sababu watu hawawezi kupata usingizi mzuri wakati wa usiku. Baadhi ya mabosi ni wagumu sana kudeal nao  au kufanya nao kazi. Lakini  katika kesi nyingi, kuna matumaini ya kweli  na rahisi  na mazuri  wakati wa kazi.

Lengo la makala hii ni kukushirikisha  mbinu  na vidokezo  vya kuendeleza  mahusiano ukiwa na bosi mwenye changamoto.  tafadhali jaribu mbinu hizi na vidokezo hivi na naomba unijulishe  zimefanyaje kukusaidia wewe.

Mwambie bosi wako kwa uwazi kabisa  Kitu unachohitaji  ili uweze kufanikiwa.

bosimkorofi_1 Anza Wiki Kwa Kuboresha Kazi Zako Na Hali Ya Akili Yako

Bosi wako sio mtu ambaye anaweza kusoma akili yako. Unapokuwa na matumaini hayo kuwa bosi wako automatically anafahamu kitu unachohitaji ili kufanikisha kazi, Hii sio kesi ya kila mara.

Unapohitaji nafasi , Sema hivi. Bosi mimi naweza kuzalisha zaidi  bila ya kuingiliwa  na mtu ,Je  Naweza kushirikiana na wewe hio kazi kesho mchana badala ya kila baada ya masaa machache? Kwa kumwambia hivyo, ataelewa kuwa unahitaji kufanya kazi bila kusumbuliwa au kuingiliwa kila mara na jambo lingine. Utashirikiana nae hatua ambazo  anataka kuchukua kwa ajili ya  kufikia malengo.

Kumsimamia Meneja Wako Kwa Ufanisi.

Wakati mwingine , mabosi huwa hawaelewi.  hawajui kukupatia mapendekezo  na maoni unayohitaji. Kama hio ndio kesi, Usikwamishwe mezani pako kwa kutegemea  usimamizi wake. Badala yake,  mfundishe bosi wako  jinsi ya kukupatia uongozi unaotaka. Mwendee ofisini kwake  na umwombe akusaidie . au Kwenye kikao kijacho sema, ” Bosi tunaweza kupanga muda wa kwenda kwa ajili ya  wazo hili. Nahitaji kujifunza kutokana na ubora wake.”

Ongea maneno mazuri

Unapokuwa humpendi mtu fulani,Ni kama vile huyo mtu anajua kwamba humpendi.  kama utatabasamu ofisini, utakuwa, mara nyingi,  utapata tabasamu kutoka kwao. Lakini kama utakuwa mtu wa kiburi  na kujiona wa thamani kuliko wengine, Basi hatutakasirika kama bosi wako atakuondoa kwenye kibali alichokupa na kumpa mwingine. kumbuka upandacho ndicho unachovuna. ukipanda upendo utavuna Upendo. Ukipanda chuki utavuna chuki. Kuwa makini ni kitu gani unachokipanda ndani yako na kwa wengine.

Tabasamu na uwaambie watu Habari za asubuhi, au ongea kitu kidogo cha kuchekesha hata wakati mkiwa kwenye lift. Bosi wako anapokuwa anaona ubinadamu  wako,  Atakufanyia  kitu kizuri, utapandishwa cheo kwa uaminifu wako na kwa kuwa wewe ni mtu unayependa watu, unayefanya kazi  vizuri.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Fundisha Akili Yako Maarifa Na Ukue Kwa Furaha
Next Kwa Nini Ukiwa Kwenye Mahusiano Huna Uhakika Wa Kuwa Na Furaha

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.