DALILI 7 ZA KUJUA KAMA UKO NA MWENZI SAHIHI:


 

 

DALILI-7-ZA-KUJUA-KAMA-UKO-NA-MWENZI-SAHIHI DALILI 7 ZA KUJUA KAMA UKO NA MWENZI SAHIHI:

Kila siku ni valentine, huo ndio mwendelezo wa kukua vizuri kwa mahusiano yalio imara bila ya kujali vyeo .kutafuta hekima na maarifa katika safari hii ya  ya kujifunza  jinsi ya kujipenda na kupenda wengine .

kuna watu wengi wanauliza kuwa nitajuaje kama nipo na  mke sahihi?

kwanza inabidi  kufahamu kwanza, na kujiuliza kwa nini  nahitaji mahusiano. na je yatafika wapi!,

watu wengi hufanya  kupata wenza kwa sababu

1.kupata mapenzi , ulinzi,uthibitisho , usalama na kupata mtoto , au mtu wa kukamilisha na kujaza upweke alionao ili  ajisikie mkamilifu na  kuwa mwenye kustahili  kwa sifa.

2.hutaka kuwa na mapenzi na mtu, au kupata kampani  ili azidi kukuza hisia zake za kimwili.

Inabidi kwanza wewe uwe ni mtu ulie sahihi  ndio utakapopata mtu sahihi , huwezi kupata mtu sahihi ikiwa wewe sio sahihi, au unaweza kupata mtu sahihi lakini wewe ukawa sio sahihi. ina maana kwamba lazima kwanza wewe uwe ni mwenye kujipenda ndipo utapenda na wengine

Pia ujifunze  kuwa mtu mkamilifu ili uje kupata mtu alie mkamilifu. kwa hio inabidi uwe na maswali mengi kabla hujaanza kuchukua maamuzi ya kutafuta mtu sahihi.Jiulize  , umekamilika au ni tamaa tu inakupeleka kutafuta mtu wa kukukampani.?

kama nia yako ni kupata mapenzi  tu , basi hapo bado  hujakamilika, lazima uwe na kazi kubwa ya kufanya ndani ya moyo wako kabla .unahitaji kupata kazi ya kujifunza  kujipenda , na kujifunza majukumu ya kupenda wengine, uwe na hisia za kujisikia mkamilifu na usalama  za namba moja, yaani kupata na kutoa.

jiulize maswali yafuatayo.

1.je mtu ulie nae ni muwazi kiasi cha wewe kujifunza kitu kwake?

mtu muwazi ni rahisi kjifunza  kujua kama anajipenda na kuwapenda wengine, lakini mtu wa kificho ni vigumu kujua , na hutaweza kujifunza kitu kwake. uwazi ni chombo  cha msingi sana katika mahusiano yeyote. hata kama kuna migogoro ni rahisi kurekebisha baina yenu . lakini watu wenye kificho ni ngumu hata kama kuna migogoro wanakuwa na hasira , hufoka , huhamaki, wanakuwa na hisia kali za kimwili zaidi. kwa hio sio sahihi.

2.ni mtu anyethubutu kujali na ni mwenye huruma na uelewa na mtu wa kukubalika na anakubali jinsi ulivyo. kukosekana kwa  uelewa  ni dalili ya moja kwa moja kuwa   sio sahihi

3.unapata zile hisia  za msingi , zile cheche  zinazokuvuta  kwake? unapenda kuwa karibu nae? unapenda jinsi alivyo?

Inawezekana ana harufu fulani hupendi,  kama huna hizi hisia ndani ya miezi 6 ya kuwa na huyo mtu basi hakufai, uelewe huyo ni rafiki tu wa kupita hawezi kuwa mwenza wa maisha .

4. je anajitahidi kulazimisha ili awe sahihi?

 

unaweza kuwa ,mnafanya vitu kwa pamoja , lakini bado unaona kama kuna upungufu fulani kwako huyomsio mtu sahihi kwako, hata ukijitahidi vipi huwezi kufika mbali nae.

5.mnashirikiana katika kipato chenu?

mnakubaliana katika matumizi?, uzazi, kula  manunuzi ya vitu, mazoezi,usafi na kuwajibika kwa pamoja  na mnaelewana?.

6.Mna imani moja ? na labda wote mnapenda siasa?

hiki ni kinyume cha kujifunza kuwa sahihi na kuwa wazi  , hapo unatakiwa umakini sana, kuna watu huwa wanaficha tabia zao  kwa kuwa wanataka kuolewa au kuoa.

7.je huyu mtu ameathirika na kitu chochote?katika maisha yake ambacho ametumia labda kimemharibu. kama vile madawa ya kulevya , labda aliwahi kubakwa , kunyanyaswa, ,labda mlevi wa pombe,  au anapenda tv,  au instagram, internet n.k

ukimpenda mtu  lazima upende na kila kitu alichonacho, jinsi alivyo, lakini ujue kuwa wote tumeumizwa na kitu fulani katika maisha na kila mmoja anhita kupata nafuu kwa mwenzake usitegemee mabadiliko ya mtu , umepata ulichoona. lakini ukiwa na subira  unaweza kuwa na matumaini ya kubadilika. lakini pia kumbuka sio sahihi.

Inabidi ukubaliane na hilo au uamue kuondoka, kwanini? kwa sababu kutegemea kubadilika  unweza kupata magonjwa ya moyo.

kumbuka: unatakiwa kwanza wewe  uwe mwenza sahihi ndipo utakapopata mwenza sahihi. tunavutwa na hisia  za kawaida  za mahitaji ya muda   na kujipenda mwenyewe, ni bora  ujipende kwanza .

bora ubadilike na kujua zaidi upendo wa kweli katika mahusiano ili  uwe kamili katika maisha yako yote.

toa mawazo yako katika hili hili kusaidia wengine

 

 

 

Previous UNATAFUTA NINI KWENYE NDOA?
Next UNAOGOPA SARATANI YA MATITI? NJIA 8 ZA KUTUNZA AFYA YA MATITI:

2 Comments

  1. […] dalili 7 za kujua kama uko na mwenzi sahihi. […]

  2. […] -dalili saba za kujua kama uko na mwenza sahihi. […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.