DALILI ZINAONYESHA KWAMBA UNA WASIWASI WA KUZIDI. JINSI YA KUONDOA WASIWASI HUO.


how-to-stop-worrying-so-much-1024x576-1024x576 DALILI  ZINAONYESHA  KWAMBA UNA  WASIWASI WA KUZIDI. JINSI YA KUONDOA  WASIWASI HUO.

Nina ufahamu wa ukweli kwamba   mimi ni mtu wa wasiwasi sana ,  nimekuwa nikijipelekesha mwenyewe kama kichaa  wakati mwingine   kufikiria na wasiwasi,

na katika mambo ya kawaida madogo madogo sana  ukweli  ni fikra mbaya,  sio afya  , kuwa na ufahamu wa  kutofikiria sana  ni ufunguo wa kutunza akili.  

1.Una tatizo la kupata usingizi.

Mwili umechoka,  lakini unajikuta  hujielewi na huna usingizi, wote huwa tunafikiria mambo yaliotokea siku nzima,  au kuwa na wasiwasi wa kesho,  na kutopata usingizi ndio hasa huongeza  matatizo.

Tafakari,  hata kama ni kufanya kwa muda kidogo, itakusaidia  kutuliza akili. Chukua muda mfupi  ukiwa kitandani, anza kukumbuka vitu vizuri vilivyotokea  siku hio,  shukuru kwa ajili ya hivyo vitu vizuri. Fikiria  vichekesho vya kazini,   mkumbuke mtu wako wa karibu kwa kitu chochote kizuri alichofanya,  jiambie kuwa unaondoa wasiwasi kabisa,  jiambie kuwa kesho ni siku mpya na utaenda kufanya vitu bora  zaidi ya jana, nguvu ya kutulia na  na ilio na fikra nzuri  zitakusaidia  kurahisisha akili yako  na kupata usingizi mzuri.

2.Unaamka na wasiwasi.

Unapanga  kulala na kutengeneza usiku, lakini  ni asubuhi ,  tayari umeamka na umejaza wasiwasi ndani ya kichwa chako.  Unatembea ukiwa mzito, fikira zinakusumbua  hujui utaanzaje siku,  watu wengi hutambua kuwa  nyota njema huonekana asubuhi , na asubuhi mbaya huharibu siku nzima.

Usiondoke kitandani mpaka umejisemesha maneno mazuri, sema unaenda kufanya siku yako iwe nzuri,  jiambie kuwa utakabiliana na changamoto zote zitakazotokea,  jiambie hutabeba wasiwasi hata kidogo ndani yako , hakuna fikra mbaya ndani yako.

3.Mara nyingi una mihemuko na hasira.

Unakuwa na wakati mgumu siku nzima bila ya kudondosha chozi,  unajikuta umekwazwa na vitu vidogo vidogo  tu  kama vile  kuhisi treni kuanguka. Inaonekana kam unahitaji  muda kidogo  wa kujirekebisha.

Pata muda wa kujijali mwenyewe,  ambao utakufanya kutulia na kufurahi. Kama  unafurahia uoto wa majani miti toka katembee,  nunua kitu kizuri unachohitaji muda ule,  unaweza kununua hata ice cream cone ,  tembelea marafiki wa kweli wanaoweza kukufanya ucheke., jaribu kulia   kama unaweza, unaweza kumtembelea mshauri yeyote alie karibu yako ili akupe ushauri.

4.Unajilaumu.

Binti yako amefeli mtihani wake  kwa sababu  ulisahau kumsaidia   kujifunza usiku kabla ya mtihani, mumewe hakupata chai asubuhi hio kwa sababu ulipitiliza kulala. Hakuna sabuni ya kuogea kwa  taulo la kujifutia kwa sababu ulichelewa kufua, hakuna maziwa kwa kuwa hukununua ulisikia uvivu wa kwenda dukani.

Huwezi kubeba uzito wote huo wa maneno begani mwako,  sisi ni wanadamu. Tunafanya makosa . tunaweza kufanya mambo kiasi kwa muda .  huenda familia ikusaidie kufanya kazi zingine za nyumbani ,  umefanya sana , lakini huwezi kufanya zote,  hata hivyo kujilaumu  kwa ajili ya vitu kutokwenda vizuri. Angalia tu vile vilivyokwenda vizuri, ushukuru.

5.Una hofu na watu , unaangalia usoni na kusikiliza  wanasema nini.

Unatembea huku una wasiwasi, eti watu wanakusema, wanakuangalia nywele mbaya,  wanakucheka,  hata viatu ulivyovaa  unaona havifai , unahisi watu wana kucheka.

Mara  nane zaidi ya kumi, vitu hivi viko vichwani mwetu. Usiachie hivi vitu vidogo vidogo vikutawale kichwani mwako. Hatutakiwi kuwa na wasiwasi ,  wala tusifikirie  mambo yalijificha , kwa chochote hata kama mtu atakuwa hamanishi kukusifia sema asante. Pita zako tabasamu kila wakati. Usiachie hata kidogo fikra mbaya zikutawale.

6.Fikra zako  zinawaza bili.

Wengi wetu huwa tunafikiria  na kuwa na wasiwasi na bill. Tukabiliane nazotu. bili zinauzi sana,  lakini tukumbuke ni sehemu ya maisha , zinakuja kila mwezi,  kubaki kuwa na wasiwasi nazo hazitaondoka, zipo tu.

Labda uchukue muda sasa kuandika  bajeti  plani. Pengine ni wakati sasa wa kuangalia kuongeza kipato cha familia. Kwa kufanya kazi kwa bidii au kufungua biashara ya pili kama una biashara moja. Itasaidia kupunguza wasiwasi.

Kuwaza sana  na kuwa na wasiwasi ni kibinadamu kabisa , maisha sio rahisi ,  na wote tunahitaji kupata kitu kizuri kwenye sahani. Inabidi kutambua wasiwasi unatoka wapi ili  tupate njia rahisi ya kukabiliana navyo. Tafuta njia  ya kuacha au kupunguza kuwaza sana na kutokuwa na wasiwasi sana,   itakusaidia kuwa na afya njema  na kuwa na akili ya utulivu  na kupata usingizi  mzuri usiku na moyo wa upendo.

 

Previous SIRI 10 ZA KUTENGENEZA URAFIKI WA KIMAPENZI KATIKA MAHUSIANO MAPYA.
Next Best Messaging Apps in 2016 for your smartphone

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.