optimistic-build-self-confidence DONDOO ZA KUKUONGEZEA  UWEZO WA KUJIAMINI.

Uko sahihi tayari… kama ulivyo tu.

Ni lini ulijitazama mwenyewe kwenye kioo na kujipenda kama ulivyojiona?

Kila siku tunashambuliwa  na  image za warembo  wanaokuwa nusu uchi na kuonyeshwa kwenye magazeti  juu, tayari  wana sura nzuri na miili midogo  isio na manyama nyama  yaliokusanyika  mahali. Viuno vidogo na mambo mengine mengi yanayomfanya akamilike kama mrembo

Haishangazi  wanaume wa kawaida na wanawake wa kawaida, kama wewe na mimi , ni wa muhimu sana  kwa ajili yetu.

Tunajitazama kwenye kioo, tunajilinganisha, na kujipenda kunapotea, tutaishije  kwenye hizo starndards zisizowezekana?

Lakini tunajaribu, kwa sababu ni nani asietaka kuonekana mzuri, ?

Mwanzo tulibadilisha vitu vidogo- vitu kama mitindo ya nywele zetu, wengine hata kubadilisha body zao kwa kuongezea  vitu vidogo, kwa ajili ya kupendeza, wanasema ukitaka kupendeza sharti udhulike. Hahahaa;, lakini  sikio la kusikia  lisikie , lisiwe sikio lisilosikia., na macho ya kuona yaone  kabisa, isiwe ni macho yanayoona lakini hayaoni..

Unaweza kuwa mrembo  kwa jinsi unavyojisikia  kuwa mrembo, hata kwa kupaka matango na nyanya   kwa ajili ya sebule yako kuwa safi, kwa namna yoyote ulivyo , kwa umbo lolote ulilonalo , unapendeza hivyo ulivyo.

lakini baadae, lakini hivyo vilikuja kubadilisha kitu  kikubwa, na hata huwezi kumfahamu mtu  kwa haraka. Mtu kujipenda kwa namna yake. kubadilika rangi na kubadilika umbo.

Wanasema kujiamini’’ ni kitu kizuri kwa mwanamke kwa kila anachokivaa, nami kidogo naamini, upande mwingine nasita. vaa kitu ambacho unajisikia amani  moyoni mwako, hata ukitoka  unajisikia vizuri kupita mbele za watu 

Kwa hio usiogope jinsi ulivyo unapojitazama kwenye kioo, Ni wewe tu, jiamini hakuna wa kulingana na wewe , ni wa kipekee, umeamka hivyo jimiliki .

Sema , ‘’Najisikia vizuri,  na niko sahihi,  najipenda mwenyewe, naonekana mzuri. ni mimi tu.

self-confidence DONDOO ZA KUKUONGEZEA  UWEZO WA KUJIAMINI.

Umeipenda hii makala ? mshirikishe na mwingine ajifunze. kisha toa maoni yako

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here