Fahamu Kuishi Kwa Amani Wakati Wengine Hawawezi


can__t_we_live_in_peace____by_ra3iiskyline-d3ab4db-1024x576 Fahamu Kuishi Kwa Amani Wakati Wengine Hawawezi

Tunaishi katika Ulimwengu mgumu  na tunashambuliwa kila wakati.Miaka ya leo ina mabo mengi ambayo yanaeleweka na yasioeleweka. Lakini bado unaweza kuishi kwa amani.

Tumeona tukikwama katika mambo mengi,  na majaribu , changamoto nyingi bado zinakuja. Matukio mengi yakutisha yasioelezeka akilini mwa watu. Tv zinatuongezea mawazo mabaya. mitandao mbalimbali inajaribu kutuweka katika kupata taarifa mpya kila leo. Na ukifikiria sana kila taarifa inaweza kuwa na ukweli ndani yake au isiwe na ukweli.  Ni ngumu kuamini na kutunza.

Kitu kizuri ambacho nataka ujue ni kwamba, pamoja na matukio yote, changamoto zote zinazotokea , taarifa zote ambazo unasikia, ziwe kweli au sio kweli.  Ni muhimu kutunza ufahamu wako, uwe na uwezo wa kuchuja , na uwe makini katika kuongea,  na kuchukua hatua popote pale inapohusika. Tunaweza kushikilia mabadiliko yaliopo , nasi tuwe tayari kubadilika. Bila shaka, Ni muhimu kuwa watu wa kukumbuka kuwa na kiasi  kwa kila kitu. Nafahamu kuwa unao uwezo wa kutambua kitu ambacho ni negative na ambacho ni postive katika Ulimwengu huu.

Hatuhitaji kutumia nguvu nyingi kutafuta sababu ambazo hatuhitaji kuwa nazo. Kuwa watu wa kukata tamaa na kukatishwa tamaa na matukio ambayo wakati mwingine hayatuhusu. Hatuhitaji kuwa na wasiwasi , tuwe watu wa kuogopa . Lakini kama tukiruhusu hisia hizi  ni kwa sababu hatujachuja taarifa ambazo zimetufikia. Tumewaza vibaya. tumeacha njia nzuri ya kuwaza kwetu ndio maana tunakutana na wasiwasi, woga, huzuni, upweke na mambo mengine kama kukosa amani na furaha.Tujaribu kuwa watu wa mitazamo mizuri. Tusishikwe sana na mitazamo ya Ulimwengu na mambo ya baadae.

why-should-we-only-rest-in-peace-why-can-t-we-live-in-peace-too Fahamu Kuishi Kwa Amani Wakati Wengine Hawawezi

Watu wengi wanasema kuwa ni vizuri mtu kuwa na taarifa zote ili kujua kitu gani kinaendelea hapa Ulimwenguni ili uwe Raia mwema. Lakini mimi sipingani na mtazamo huo, lakini ni sawa na kuwa na umuhimu wa kuwa na ufahamu. Lakini kama unapata wasiwasi, woga, kuchanganyikiwa au kukata tamaa ya maisha , kukosa tumaini, kuzidiwa na mawazo, Nafikiri hio haitakuwa nzuri kwako. Kwa hio tunawezaje kuwa na amani  na matumaini kama kila mtu anashauri kuwa ni lazima kuwa na taarifa zote ? Hapa kuna baadhi ya maoni ya kufanya iwepo uwezekano.

Tembea njia ya Katikati.

Kama katika kila kitu maishani lazima kuwa na ufunguo wa kuthibiti upataji wa taarifa  kwa kila tukio, hasa yanayohusiana na yajayo. Fungua ufunguo wako kwenye taarifa ambazo ni positive kwako, ambazo huko ndiko nguvu yako inakoelekea.  Zaidi ya hapo utataka matatizo yawepo mkononi mwako.

Uwe Na Amani.

Hata kama kuna kitu chochote  kimekaa vibaya katika mazingira yako ya aina yoyote, Amani yako iwepo.Na uwe na nguvu ya kuitengeneza hio. Kuwa makini katika kuboresha amani . Na ufahamu kuwa wewe ndio unaewashauri wengine kurahisisha mambo ili wawe na amani.

Uwe mtu wa kujaribu kuwa na tumaini.

Ni ngumu kuwa na amani wakati unapoona baadhi ya matukio yanazidi. Lakini kama ukitaka kubaki na amani yako  na kuwa chanzo cha badiliko la baadae, utashikilia tumaini kwa gharama yoyote. na utakapothibitisha , anza kushirikisha hilo tumaini kwa wengine ili nao wafahamu kuwa kuna tumaini .

Amini kwamba kila mtu analo kusudi.

Ni ngumu kuamini kuwa kila mtu anaona hivyo, hasa mambo yanapokuwa magumu. Hasa wakati huu ambao akili za watu zimefungwa na taarifa mbaya. watu wamekuwa na woga, wasiwasi, wamekosa matumaini. Ni ngumu hata kuaminika. lakini unaweza kupata imani katika kila unachokiona kwa jicho la Mungu. positive eye. Ukaamua kusaidia kuondoa maumivu yao na wewe ukazidi kuiona amani .

Sasa basi , zaidi ya yote, Ulimwengu unatutaka tuwe imara,  Mioyo yetu iwe wazi, tuwe vyombo vya amani. Ni uamuzi wetu kutengeneza Ulimwengu tunaotaka ili tuishi humo na kuacha mengine nyuma. Kwa hio mimi kama mwalimu wako leo,mwalimu wa roho yako. Nakushauri hivi. Usiukumbushe Ulimwengu kwamba kuna matatizo na magonjwa, Bali ukumbushe kuwa kuna amani, uzuri na uhuru wa kuishi.

Tafadhali kama umepata kitu ndani ya makala hii , washirikishe wengi , kutoa ni moyo. Ukipata toa. usisahau kulike page yangu.

Kisha Subscribe.

 

Previous Tabia Zinazobadilisha Maisha Kwa Urahisi
Next Msingi Wa Siri Uliojificha Ndani Yako

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.