519e18ae3282538ba7da7c7346589fbb FAHAMU SIRI YA KUMPENDA MUNGU KWA MOYO, AKILI NA NGUVU ZAKO ZOTE.

Ni miaka mingi nimekuwa nikijiuliza swali hili, nitawezaje kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote na kwa nguvu zangu zote? Kila nikisoma maneno haya  moyo wangu unaugua, nashindwa kuelewa kwa sababu ya kutofahamu siri ya kumpenda Mungu kwa namna hio ni ipi.

Katika kutafuta huku na huku ndio nikakutana na majibu ya maswali yangu. Jinsi ilivyo muhimu  kuweka misingi mizuri  katika maisha ya Kikristo.Kitu ambacho Mungu  ametuambia  kumpenda yeye kwa moyo, akili, roho na nguvu zetu zote.

Unapotumia nguvu lazima akili itumike na roho yako na moyo wako vyote vikishirikiana pamoja ndio hapo utagundua kuwa unampenda Mungu.

1.Kujipenda  na kujikubali, kujiheshimu, na Kujijali .

Unaweza kuona kama ni kitu kidogo lakini  unahitaji kutumia nguvu  kwa ajili  ya kujipenda, kujijali ,kujiheshimu na kujikubali. Mungu amesema kuwa Huwezi kumpenda yeye kama humpendi ndugu yako unayemuona.

Na kumpenda jirani yako kama nafsi yako.

903236 FAHAMU SIRI YA KUMPENDA MUNGU KWA MOYO, AKILI NA NGUVU ZAKO ZOTE.

Na hapa ndipo palipo na kila kitu , Ukitaka  heshima  lazima ujue siri ya kujipenda wewe, na kujijali, na kujikubali wewe kwanza.

Katika pitapita yangu nimegundua kuwa hata katika mahusiano yeyote hutaweza kukaa salama kama hujaanza kujipenda  na kujijali wewe mwenyewe.  Huwezi kuupenda mwili wa mwenza wako kama huupendi mwili wako. Ndio maana Mungu alisema kuwa Mpende Mke wako kama unavyojipenda wewe. Hapa ina maana kuwa ukijipenda utampenda na mwingine . Na  hio ndio kumpenda Mungu kwa moyo , roho , akili na nguvu.

2.Fahamu nia yako, na ifanye iwe ya juu,

  Jione kuwa uko ndani ya mwanga,Imarisha nia yako,  jifunze kusamehe, kujisamehe na kusamehe wengine, jifunze kuachilia,  tambua utakatifu ni upi,  kumbatia usichokijua,  halafu mruhusu Mungu afanye kazi yake. Somo makala hii  -KANUNI AMBAYO ITAKUWEKA KARINU NA MUNGU  ikusaidie kufafanua haya niliyoyataja.

3.Chagua njia moja tu usiwe vuguvugu.

Mungu anawapenda watu wote , na kila anayemuomba anasikiliza na kumpa kwa kadri ya hitaji lake. Vinginevyo kusingekuwepo watu duniani. Zipo njia mbili tu  .

-Njia ya Uzima

-Njia ya uovu, ambayo ni wengi wanaitumia.

Anza leo kutumia moja ya njia hizo na utaona matokeo yake. Ukimpenda Mungu  kwa moyo wako wote utachagua kwa hekima njia ya kuifuata.

Mtumikie kwa matendo yako mema,  Uwe mwaminifu,  uwe mkweli, Wapende watu, wahurumie wenye shida,

21NovP325BA800x600 FAHAMU SIRI YA KUMPENDA MUNGU KWA MOYO, AKILI NA NGUVU ZAKO ZOTE.

Kumpenda kwa roho ina maana ya kutumia utu wako wa ndani unapokuwa unafanya maamuzi na uchaguzi wa kutengeneza mtindo wa maisha yako, tabia yako. Fikiria  iwe ndio msingi wako.

4.Uwe na hekima katika kujua kuwa unatakiwa kutumiaje pesa, muda wako, Unaangalia nini, kitu gani kinakupa faraja, unasoma nini, aina gani ya marafiki ulionao?

Yatii maneno yake. Utii uwe ndio jambo la kwanza na hisia zitafuata. Hapo akili yako itafanya kazi kawaida kwa sababu akili hushika kile ambacho moyo  umekipokea, mfano ufahamu, kumbukumbu, kufikiria jinsi kazi ya mikono yake ilivyofanya Mbingu, nyota na mwezi na jua.

5.Mpende Mungu kwa macho yako na unachokiona, mpende kwa masikio yako kwa kusikia maneno yake,Sikiliza katika kubadilika, sikiliza zaidi kuliko taarifa, sikiliza mawazo ya watu, maumivu yao, epukana na umbea, kuteta, na mawazo mabaya, mpende kwa miguu yako kwa kuwatembelea wagonjwa, wafungwa na yatima na wajane. Mpende kwa midomo yako kwa kuwaambia watu maneno mazuri ya uzima.

Chagua kutenda mema leo ili kesho yako ikushukuru.

Kama umependa washirikishe wengi wajifunze.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here