FUNGUA MOYO KWA AJILI YA KUPENDA


holding_hands_church-1 FUNGUA MOYO KWA AJILI YA KUPENDA

Hii Ni Amri Nimewapa Mpendane

Kujifunza kupenda.

Inawezekana kuna swali moja tu ambalo watafutaji wanahitaji kujiuliza wenyewe kuhusu  hali zao za kiroho ya kwamba, Napenda kwa kiasi gani?

Nilisikia hadithi  kuhusu watu wawili mwanamke na mwanaume walikuwa wakienda  nyumba ya ibada, kabla hawajafika kwenye gate walianza kujilaumu kuhusu maisha yao wenyewe. tabia zao, Kwamba wamekuwa wazazi bora? Amefanya kitu gani cha kukamilisha kusudi lake?, Anahudhuria ibada ipasavyo?  Natoa kwa ajili ya kuwapa wenye mahitaji? Na walipokaribia kuingia  walijiuliza swali moja tu, Najipenda na kuwapenda wengine kwa kiasi gani?

Kama unataka wengine wawe na furaha waonee huruma. Mama Tereza alisema , haijalishi ni kiasi gani tunafanya,lakini ni kiasi gani tunapenda kuweka nguvu katika kufanya hivyo?. Haijalishi ni kiasi gani tunatoa, lakini ni kiasi gani tunatoa kwa upendo?

Kujifunza jinsi gani utampenda mtu, watu, ni lengo na ni kusudi la maisha ya kiroho.

Sio kujifunza jinsi ya kuinama kuabudu, jinsi ya kuomba, jinsi ya kumeditate, au mazoezi tu. Lakini ni kujifunza kupenda. Upendo ndio Ukweli.Upendo ndio mwanga.

Kwa upande wako huwa unafikiria nini kuhusu Upendo?.Unafikiria watu unaowapenda, watoto wako, mwenza wako mpenzi, wazazi wako, rafiki yako? Au kitu kingine kama mbwa, ng’ombe, mbuzi, gari, nyumba. Unafikiria vitu unavyovipenda?  Unafikiria kuhusu kumpenda Mungu?, kupenda jamii, kupenda nyimbo, michezo au kusoma? Vipi kuhusu upendo kwa walio huru na wafungwa?

Je unafikiria kweli kuhusu mwenyewe, kujipenda, kujiheshimu, kujithamini, na kujikubali?

faithgodreachingjpg-1 FUNGUA MOYO KWA AJILI YA KUPENDA

Tunapoongelea kuhusu upendo katika maisha yetu, tunaongelea  kukubaliana na kitu kizuri, kwa maana kwamba tunapenda kwa sababu kitu au mtu kafanya kitu ambacho tunajisikia vizuri. Tunaposema tunampenda mtu, lakini tukitazama ndani ,kitu gani hasa tunachokipenda? Mara nyingi mawazo yetu huiga tabia iliopo, kama napenda ninavyojisikia wakati niko na wewe–mara nyingi. au napenda kazi yangu, huku unatamani siku ya ijumaa ifike haraka. Sasa kuna maana gani hapa. Ni kwa sababu huyu mtu tunampenda kwa sababu ya kitu tunachopata, vivyo hivyo na kazi, kwa sababu inatupatia  malipo?

Tunapotembea katika njia ya kiroho, tunapata kuelewa nini maana ya upendo.. Tunajifunza kufungua moyo na kutafuta kwa ndani zaidi thamani ya upendo.

1.Upendo unaoonekana

Upendo huu unaitwa upendo wa kikemia.unatokea unapovutiwa na mtu mwingine wa jinsia tofauti kwa muunganiko wa matendo, ni upendo wa kimapenzi, matamanio au shauku. Upendo wa hisia  na wakati mwingine hakuna hisia.

2.Upendo wa Hisia

Upendo huu hutuonyesha ushirika, tunapata upendo huu kutoka kwa wazazi, watoto , marafiki na mates.upendo huu ni wa ndani na hutufanya tuweze kufungua mioyo yetu.

3.Upendo Wa Ufahamu

Huu ni unconditional love , ni upendo wa Mungu, ni upendo wa aina zote. Ni upendo mgumu kuutunza. Upendo huu huelezea uwezo wa mtu bila ya kuhesabu kitu.nimesema upendo wa ufahamu kwa vile ni  upendo wa  wenye nia ya kujenga . hauna bahati mbaya; hauhusiani na matamanio,  uhitaji, ndoto; hutegemei kitu ni kupenda bila sababu.

Kwa hio unapotembea katika njia ya kiroho unatakiwa uwe na upendo huu wa ufahamu. Tuwe na upendo ambao hauna sababu.

Watu wanasema kuwa  sisi sio wakamilifu. hatuwezi kuwa na upendo kama wa Mungu, lakini ni nani anaweza kupenda kama Mungu? Sisi ni wanadamu tunajaribu kuelewa na kutunza maana ya upendo wa Mungu. Tunaweza kuanza kidogo kuonyesha upendo kwa watu, tukiwa tunafanya hivyo kila siku tutaweza kuwa na upendo wa kweli Ni kama kujenga misuli ya mwili unapokuwa unahudhuria gym.

Upendo ndio iwe lengo letu, tujitahidi kujifunza kupenda, tufungue mioyo kwa ajili kupenda.

Previous DALILI ZA HATARI 8 NA MBAYA SIKU YA KWANZA  UNAPODATE NA MTU
Next WAKATI MTU UNAEMPENDA HAKUPENDI UTAFANYAJE?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.