BlogQuote06-1024x576 Hatutaki Kisasi , Tunafikiria Tu Tunachokitaka

Inatokea kwa kila mtu;Tunakuwa na uzoefu wa maumivu tunayopata kutoka kwa mwingine , Na hutuacha na hasira ya kisasi  na huzuni ambayo tayari inakuwepo ndani yetu

Au kwa maana nyingine ,  tunahisi tunaweka  katika muda fulani na huo muda  bado hauna kitu chenye faida kwetu.

Kisasi sio kitu tunachokihitaji, ni kitu tunachokifikiria tu kuwa tunakitaka. Tunachokitaka ni amani na kuelewana. Tunataka kukubalika katika mazingira  na  kuwa na uwezo wa kuachilia maumivu yaliotokana na hayo. Hatutaki kuteseka, Tunahitaji watu hawa waelewe kwamba kwa nia moja au bila nia yoyote tumepitia hili. Tunataka tuelewe kuwa kipo kitu kizuri Ulimwenguni kinachotuweka sawa. Na kama sisi ni watu wazuri, mazuri yatakuja kwetu.

Hivi vitu vinatupoteza.Kuwa watu wazuri hatuwezi kuwa na uhakika wa uzuri,  hii ndio maana kujikubali na kuelewa ni muhimu sana  katika maisha yetu yote. Tunahitaji kujifunza  kukubali vitu vibaya vinapotokea,  sio kwa sababu  sisi ni wabaya lakini ni kwa sababu  ndivyo ilivyo. tunahitaji kuelewa.

Tunahitaji kuelewa kuwa watu mara zote sio wazuri tu na sio wabaya tu pia. Wakati mwingine ni wazuri na wakati mwingine ni wabaya. Kisasi ni kupoteza nguvu na muda, kwa sababu mabaya unayojisikia kuhusu mtu huyo , Yatakurudia tena wewe.

it-is-your-karma-6-2 Hatutaki Kisasi , Tunafikiria Tu Tunachokitaka

Kuna wakati ambao nilipata  maumivu  ambayo niliona kuwa sikustahili kabisa kuyapata, nilijisikia kama kudharauliwa. Kufukuzwa katika hali ambayo  hujui kitu chochote mbele yako. Nilifikiria kwa nini wasingeniwezesha kubadilika , nilifikiri kwa nini  vitendo hivyo vitokee bila ya kuelewa hali halisi iliopo. kitu cha muhimu nilichokichukua muda huo kupitia matendo yangu hayana sababu kwa yale ambayo yalifanyika . Mara nilipokubaliana na hili, niliweza kuona  hali halisi na maumivu yalianza kutoweka.

Tatizo hili lilitokea mahali ambapo niliweza kuona maneno na maumivu.Kuanza kuelewa na kutambua  moja baada ya lingine. ilisaidia,lakini utoshelezi wa kweli unatokana na kufahamu na kuelewa kwa hatua moja au nyingine. hii haikuja katika uhakikisho au  kunielezea nilivyo, ilikuja kutokana na amani  na uelewa wa hali halisi pamoja na nia  ya wale wahusika. hii ni hatua ya ndani ya kuelewa  kwa mwanadamu  kuliko kuwa na haraka ya kufanya kisasi.

Hii sio kusema kwamba kama una nia nzuri  ulimwengu  utakuwa wako. Ingawa  kila wazo zuri huvuta wazo zuri, nguvu nzuri huvuta nguvu nzuri. Na hii huanzia  katika kukubali jinsi mambo yalivyo. Tunapokubali mabaya, tunaweza kuyafurahia mazuri. Kwa hio , Tunapofurahia mabaya , tunaruhusu kukubali kikamilifu yalio mazuri

Fanya mambo mazuri na mambo mazuri yatakuja kwako. kwa sababu tunahitaji tunahitaji kuelewa, sio kwenye matatizo yetu tu bali na ya wengine. tunahitaji kutoka katika giza na tunataka kuona mwanga. kufahamu kweli, uwazi  wa kila mtu.

Ukiwaza mabaya utazalisha mabaya, lakini ukiwaza mazuri utazalisha mazuri. Uko kwenye Friquence ipi?

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here