muda-660x400 Hii Ni Nzuri Wakati Unapochagua Kujisamehe

Siwezi kukiri kwamba nimekuwepo kwenye mahusiano mazuri. Nimepita kwenye mambo mengi hasa linapokuja swala la upendo na nina uhakika wa kujaribu tena. 

Lakini naamini kabisa kuwa tunajifunza uzoefu. Kitu ambacho nimejifunza na kukikumbuka ni  kwamba , mwache mtu ambaye anakufanya ukose amani , uwe na maumivu na usirudi tena kwake. Ingawa kuna vitu ambavyo vinatufanya kubaki lakini je unao uwezo wa kuvulia magonjwa yanayotokana na maumivu?

Leo kidogo nimekuja kitofauti kabla mwaka huu haujaisha kabisa , tuambiane ukweli. Kila mtu utakayekutana naye atakuambia kuhusu kuweka msingi mzuri wa mahusiano.  Msingi unaotoka kwa kila mtu.

Wengi wanasema  msingi wa afya wa mahusiano ya kudumu ni Uaminifu. Wengine watakuambia msingi mzuri wa kudumisha mahusiano ni  mawasiliano. Utakapojenga msingi huo yataibuka mengine ambayo hukuwahi kusikia wala kuona.” perfect” romance. Hii inakusanya , uaminifu, mvuto,  ukweli,  uwazi, nguvu,  na kuendelea zaidi.  Katika kucheza na vyote hivi,  utashangaa mjuzi wa upendo wa dunia hii hawezi kutulia bila ya kuwa na swali. Ningependa kushauri kuwa hakuna hata mojawapo litakalofit.

Inatokea katika mazingira tofauti . katika misingi ya mahusiano ya kawaida, huenda katika kufanyia mazoezi hutaweza kuwa tofauti.  Kila mtu analeta upekee wa kwake  uzoefu wa kwake. Kila mtu ana maoni yake, mtazamo wake, uelewa wake. Ni ujinga kufikiria kuwa Upendo unatengenezwa kama formula ya kutafuta jibu la hesabu. haiwi kwa urahisi hivyo. Nafikiri kuna kitu kimoja tumekimisi kila mmoja wetu inapokuja katika kufanikiwa katika mahusiano. Kitu hicho ni Msamaha

Katika umri wangu nimefanya makosa kwa kufikiri kuwa msamaha ni kwa ajili ya mtu ambaye amenikosea. Kwamba atasema nisamehe na kumsamehe ili aweze kuendelea na maisha yake.

Nimekuja kugundua kwamba msamaha sio kwa ajili ya mtu mwingine ni kwa ajili yangu.

Msamaha ni kuwa huru. Kupitia kitendo cha kumsamehe mtu ni kama kujiambia kuwa  ni wakati wa kuachana na Machungu na Hasira, Unaweza kusafisha akili yako ndani ya mawazo yako yale yanayojirudia kichwani. Unaweza kuondoka kwa busara na mwenye nguvu kuliko ilivyokuwa mwanzo. Msamaha unakufanya uishi maisha yenye furaha.

Hii imenileta kwenye point nyingine.

Wakati napata uzoefu katika kujua kuwa msamaha ni wa kipekee, hapakuwa na shaka nilipowasamehe wengine. Kuna uzuri. Uzuri wa kusamehewa na mtu .Kwenye kosa la kibinadamu. Ulimwengu unapoonyesha sura ya makosa kama hayo katika mahusiano, na yakawa ni ya kurudia rudia, ni hatari.  mahusiano hayo  huwa yanakosa nafasi, ndio maana unakuta mtu hawezi kumsamehe mwenzake.

Kwa upande wangu  nilifanya kinyume kabisa, Sikujali hisia za mtu, nimeumiza mtu, nimeumizwa mara nyingi,  Lakini niliporudi kwenye akili zangu, sikutaka kitu chochote zaidi ya kuhitaji kujisamehe na kuondokana na maumivu yote.  Ingawa nilifikiri nitajilaumu, au nilifikiri sikuwa sahihi. lakini nilijua kuwa niko sahihi. nilianza kujitoa mwenyewe kwenye sumu kali. niliamua kuwa bora kila siku na kwa watu niwapendao.  Nilianza kujisamehe kidogo kidogo  kutokana na makosa niliyoyafanya. Lakini nimekaa hapa leo nikuambie kuwa haikuwa rahisi kujisameje  au kumsamehe mtu ambaye aliniumiza.  Lakini kwa pumzi hiyo hiyo naweza kukuambia kuwa  inawezekana.

Ipo hali ambayo mtu anajaribu kuwa na nguvu, hasa pale anapokuwa na huzuni, kuona huruma, kujaribu kuelewa na kuanza kufikiri kuwa haiwezekani. hio yote ni udhaifu  na utakusababisha ukutane na mauti.  Kusamehe inahitaji nguvu.  Kuelewa inahitaji  nguvu zaidi kuliko kutii na kuliko kutembea peke yako Hapa Ulimwenguni.

Usinielewe Vibaya. Kuna mambo ambayo ni magumu kusameheka. Nimekuwa nikiwatia  nguvu na kuwashauri wanawake na wanaume ambao wamekuwa wakifanyiwa vibaya ndani  ya mahusiano yao kusamehe na kubaki. Ingawa katika kizazi cha sasa hakina uvumilivu,  Hatutaki kuvumilia na kupewa majina mazuri ya kuwa mvumilivu na kumpa mwenzako nafasi ya tatu. Lakini kumbuka msamaha ni kwa ajili yako. Sio kwa ajili ya wazazi au marafiki au wengine.  Unajifahamu vizuri kuliko  mtu mwingine anavyokujua, unaweza kufanya maamuzi unapoona Yatosha  Kuwa ni Yatosha maumivu, Ni Yatosha kweli.

Kwa hio huenda ni wakati  ambao unajiuliza maswali. Huenda hupati mapenzi unayostahili kupata. Au huna amani . Ondoa kwa Neema. Watakie mema. Na usirudi nyuma. Lakini kabla ya kufanya hivyo ni vizuri kuangalia hisia ulizonazo. hakikisha uko vizuri.  Hakuna mpangilio ulio kamili, unajaribu kufuata maisha yote mawili.  Sote tunakosea. Wote tuna nyakati  tabia zetu zinabadilika. Kama mtu huyo aliwahi kukusamehe kwa kitu fulani, huenda na yeye anatakiwa kusamehewa.

Wakati mwingine mtu aliyekuumiza wewe, ni huyo aliyekuponya 

Amekusaidia wakati uliokuwa mbaya, akakufanya ukae vizuri. Jaribu kumpa nafasi pia.

Usijidharau, Usijikatae mwenyewe. Lakini kumbuka , Upo uzuri unapojisamehe wewe mwenyewe

Take care of yourselves.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here