couple-254683_960_720 Hivi Unajua Nguvu Ya Mahusiano Huja Baada Ya Kujaribu Upendo Huu

Upendo mara nyingi  hauji kwa urahisi,  hata kama umekutana na mtu sahihi, kunatokea  upinzani na mawasiliano mabaya  kwenye  changamoto  ya kuonyesha upendo  uliopo kati ya watu wawili.

Hujawahi kujiuliza kama kweli huyo mtu unayempenda kama na yeye anakupenda? huenda hajawahi kukuambia kwa maneno kuwa anakupenda lakini kuna dalili ya vitendo mbalimbali anaonyesha kwako. hata  hivyo unajaribu kila njia ili uweze kujua kama kweli anakupenda  kwa kumpelekea zaidi na kumpatia muda wako  lakini haonyeshi kuvutiwa . Unaweza ukamwelezea kama mtu asiye na shukurani  lakini huenda hathamini  aina ya upendo unaoonyesha.

Unapohisi kuwa uko sahihi katika upendo unaoonyesha , lakini kutoa kwako na kupokea huo upendo  inaonekana ni mgumu  kwa kuwa  lugha unayotumia sio  anayoijua huyo mtu.

Kuna wakati nilimpenda mtu kupita kiasi cha kupenda. Kila nikiangalia upande wake nauona upendo wa kweli  , lakini  hathubutu kuniambia kuwa ananipenda. Basi nikaamua kuwa naye karibu ili angalau asome mazingira niliyo nayo wakati huo, lakini hakufanya hivyo.  Nilikasirika  nikamua kumtoa akilini mwangu  haikuwezekana. Nikafunga na kuomba lakini wapi. ilinisumbua muda mrefu . Nilipogundua kuwa lugha niliyotumia sio ambayo yeye anatumia nilipona.

Ni Nini Lugha Ya Mapenzi?

Lugha ya mapenzi inajielezea kwa njia nyingi tofauti. Hapa nakuletea njia 5 tofauti ili ujipime uko katika njia gani . Na pia huenda hapa isiwepo hata moja kwa ajili yako.

1.Maneno ya Uthibitisho.

Hii ni njia ambayo mtu anaitumia zaidi kuliko vitendo. Anaongea meneno  mengi kwa ajili ya kujielezea upendo alionao kwa mtu, hisia alizonazo kwa huyo mtu kuliko matendo ya mwili kama kutumia muda  na kutoa zawadi mbalimbali.

2.Vitendo vya Huduma.

Nigerian-Traditional-Wedding-Bunmi-and-Mayowa-couple-cutting-the-cake-LoveweddingsNG Hivi Unajua Nguvu Ya Mahusiano Huja Baada Ya Kujaribu Upendo Huu

Hawa ni watu wanaoamini kwamba vitendo vinaongea kuliko maneno. Huonyesha upendo kwa kupitia vitendo zaidi  kuliko kumwambia mtu maneno.Hii inaonekana pale anapotumia muda kwa ajili ya mtu , kufanya kitu ambacho hawezi kukifanya kwa mtu yeyote , kumpa zawadi, kumpikia chakula au kumtoa  kwa ajili ya dinner.

3.Kupokea Zawadi.

Wengi hufikiri kutoa au kupokea zawadi ni dalili ya  upendo. Hufikiri kuwa huyo mtu amekuwa akimfikiria kila wakati. hio inaonyesha kuwa upendo wao umekubalika  na kufanya siku yao kuwa nzuri.

4.Ubora Wa Muda

Screen-Shot-2017-02-13-at-9.56.32-PM-e1487044660193-1024x666 Hivi Unajua Nguvu Ya Mahusiano Huja Baada Ya Kujaribu Upendo Huu

Muda ni kitu ambacho cha muhimu kwa kila mtu , kwa hio kutoa muda kwa ajili ya mtu  ni kuonyesha jinsi gani unampenda huyo mtu . Watu wengi huona njia hii kuwa ni ya nguvu kuliko njia yeyote, Hasa wale wanaojua matumizi ya muda. Hii ni njia ya muhimu kuliko kusema maneno  au kufanya kwa vitendo.

5.Mguso Wa kimwili.

Thee-Urban-Sophisticate-discusses-the-difference-between-complimenting-someone-and-flattering-them.-www.iDateDaily.com_ Hivi Unajua Nguvu Ya Mahusiano Huja Baada Ya Kujaribu Upendo Huu

Mguso wa kimwili ni muhimu katika mahusiano, iwe ni kwa sex au kushikana mikono, kukumbatiana. Watu wengi hufahamu hili kuwa ni njia yenye nguvu kuliko zingine . Njia hii inaelezea upendo kuliko maneno au vitendo vingine vyote.

Unaweza kukubaliana na baadhi ya mawazo haya ya kuonyesha upendo kwa mtu au usikubaliane nayo, na huku ndiko kunakotokea matatizo. Hakuna hata njia moja isikuwa sahihi au ambayo ni sahihi ya kumwambia mtu kuwa tumia hii. Lakini kama mwenza wako anaonyesga upendo wake kwa mguso wa mwili  chukulia njia hii kwa lugha ya tofauti sana.

Chukua hio lugha yake na ijaribu jinsi gani utawasiliana naye ili kuujua upendo alionao.

Kila mtu anaweza kuonyesha upendo kwa njia ya tofauti kwa mtu anayempenda.  Tumekuwa tukionyesha  upendo wetu kwa wengine  kwa kutarajia nao wataonyesha upendo kwetu. Lakini kama tutapokea tofauti tunaelewa kuwa hawana upendo kwetu kama tunavyoonyesha upendo wetu kwao. Na hii ndio inayofanya kiwango cha mahusiano kushuka. Lakini inatakiwa kuchukua muda ili kuelewa aina gani ya upendo  anaotumia au ni aina gani ya upendo anahitaji. Hii ni kwa sababu kila mtu ana lugha tofauti ya kujielezea upendo wake.

Chukua muda wa kumsoma mwenza wako, mtu unayempenda , Ili ufahamu ni aina gani ya upendo anaonyesha kwako. Kila mtu akijua hili , Mahusiano yatajengwa kwenye msingi imara.

Lakini hii isichukuliwe na Upendo wa mapenzi. Tazama jinsi gani anakutreat wewe na kuwafanyia watu wengine. Familia na marafiki .

Kwa hio hakikisha unafanyia kazi hili la kufahamu thamani ya lugha ya mapenzi alionayo. Kwa mwanamke na mwanaume. Ukipata matokeo tumia njia hio  na uelewe jinsi gani mtaonyeshana upendo kila mmoja.

Toa maoni yako kusaidia wengine.

Umependa makala hii? share kwa wingi kisha  Subscribe kupata makala nyingine mpya.

Usisahau Subscribe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here