Imani Inayovutika ( The elastic Faith)


B027-B-信神就當順服神-Katika-Imani-Yako-kwa-Mungu-Unapaswa-Kumtii-Mungu-SW Imani Inayovutika ( The elastic Faith)

Kama Imani yako sio ya plastic, haiwezi kukua. haiwezi kuvutika. Kuna imani za chuma, mbao, kamba, ambayo kila mara inaona hofu, mashaka  unapoingia katika magumu. lakini Mungu alimpa mwanadamu Imani ya Plastic. 

Mitume walimwambia , Bwana tuongezee Imani. Bwana akasema, Kama mngekuwa na Imani kiasi cha chembe ya Haradali, mngeuambia Mkuyu huu Ng’oka ukapandwe baharini, nao ungewatii.

Mnyama anaishi kwa matumaini, kwa upendo. Lakini mwanadamu anaishi  kwa vitu vitatu,  Imani , matumaini na Upendo. Na mwanadamu amewekewa moyo wa kuthubutu. Ongeza imani inayotanuka.

Yesu ni Imani

Mungu Ni Pendo

Roho mtakatifu ni Muda

Imani huja kwa kusikia, kitu unachokisikia kinakuletea imani.  Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo.

Huwezi kumpenda Mungu pasipo Imani. Imani pasipo matendo , imani yako imekufa. Imani inayofanya kazi na Hekima, hufanikiwa.  mwanzilishi wa imani ni YESU.ukiwa na imani ya pesa, tambua tu kuwa imani yako ni ya kamba. inaweza kukatika muda wowote.

Mungu anambariki mtu ambaye ana hekima, maarifa na ufahamu. Kwa sababu Mungu aliumba Ulimwengu kwa Hekima maarifa na Ufahamu mkubwa.

Kila mtu hufanikiwa kutokana na imani yake. Lakini ni muhimu kama imani hio ni ya Plastic. imani inayokua, imani ya kudumu. imani yenye akili. Maana ni nani ambaye anafahamu nia ya Bwana ili Amwelimishe?

Kiwango chako cha Imani Kikikua na Upendo wa Mungu Unakua Ndani Yako. Roho ya Bwana itakaa ndani yako, roho ya Hekima na ufahamu, Roho ya Ushauri na Uweza, roho ya maarifa na kumcha Bwana. na furaha yako ni katika kumcha Bwana.

Kiwango chako cha Imani kikikua , Tunda la roho litajaa ndani yako.  Upendo, furaha amani,uvumilivu , utu wema, fadhili, uaminifu, upole  na kiasi.  Utaishi katika kweli ya Mungu, Uhalisia wako utajulikana.

Mungu anapenda kusoma vitu kwenye soft copy sio hard copy. Akili ya mwanadamu na moyo wa mwanadamu ndio Kioo cha Mungu.

Pigana vita vizuri vya Imani. shika uzima ule wa milele ulioitiwa.

Vitu vilivyoshikilia maisha yako, vinasababisha uwe mtu wa hofu, wasiwasi, huzuni. lakini ukiwa na imani ya kukua, imani ya plastic utavishinda  na utaishi maisha ya kweli.

Penda nafsi yako Mpende jirani yako , Mpende Mungu. Wapende na kuwafanyia watu vizuri. Jitambue, jithamini, Jikubali,  Fahamu Ulimwengu.

Kumbuka ukimpenda jirani yako hutaweza kumwibia, hutaweza kumsema vibaya, hutaweza kuzini naye, hutamtamani.  Ukimpenda jirani yako kwa jinsi hio utapata wema na utajengwa  katika nguvu ya Mungu.

Usitembee kwa kuona, tembea kwa Imani kama Mungu anayvotumia imani  .jiwekee msingi ulio bora kwa kufikiri, kutoa mawazo, kutafuta taarifa na kuziweka kwenye karatasi.

Imani ni sasa. Sasa hivi. Usiseme utaanza kuamini kesho, mwezi ujao hapana. Imani ni sasa hivi.

Mungu Akuongeze Imani.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

 

Previous Tatizo Sio La Wanawake.
Next Acha Kujilinganisha Na Wengine

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.