Imani Katika Maisha Yako,Kazi Na Biashara


28242-faith-makes-miracles.1200w.tn_-1024x596 Imani Katika Maisha Yako,Kazi Na Biashara

Maisha ya mwanadamu yana fomula. Yana kanuni , Yana vielelezo,  Yana sheria na masharti mbalimbali. Kuna kanuni za kivutio, kanuni za kupanda na kuvuna.Na nyingine nyingi .

Lakini leo napenda nikuletee Aina moja tu  ,  fomula ya maisha.

Biblia inasema kwamba Mungu ni Alpha na Omega, Ni kweli kabisa. Lakini nikiangalia hapa naona kuna mgawanyo. Mungu amegawanyika. Yeye ni Mwanzo, Na pia ni Mwisho.

Ina maana kwamba , kama yeye ni mwanzo, Hapo katikati kuna nafasi mpaka kufikia mwisho.

Hapo katikati  ni mimi na wewe. Hapo katikati kuna Muda wako na muda wangu. Hapo katikati ndio maisha yangu, ndio maisha yako. Hapo katikati kuna milima, kuna mabonde, kuna kukata tamaa, kuna kuinuliwa, kuna mafanikio, kuna biashara, kuna kazi, kuna kuoa na kuolewa, kuna mapito mbalimbali. Hapo kati kuna  masaa 24. Hapo katikati kuna siku zako 120

Alpha ndio Mungu ambaye kila mtu anaishi naye kila siku. Mungu tunayemuomba kila siku. Ni mungu wa maombi. Lakini Mungu wa Omega ni Mungu wa Vitendo.

Mungu wa Omega sio kila mtu anamfikia, ni wachache sana , tena ni wale wanaofikiri sana na kuweka  vitu vyao katika matendo.

Mungu wa Alpha ni Mungu wa kila mtu.Kila mtu anaweza kumfikia kwa urahisi mkubwa. kwa sababu ya kutokufikiri kwa kina na kutenda. utakuta mtu kila siku anaomba lakini hachukui hatua yeyote.

Twende tuangalie baadhi ya mifano.

Walokole wengi, na huenda wakristo wengi , Mungu wao ni Alpha. kwa nini nasema hivyo? ni kwa sababu maombi yao ni mengi sana chumbani lakini hawachukui hatua.

1.Ukiomba kupata ujasiri wa kuongea barabarani ili kuvuna nafsi na kumletea Yesu watu wake. Ujasiri utatangulia barabarani.  Unatakiwa uende sio kuanza kujivuta mara kesho, siku ijayo, wiki ijayo ,mwezi ujao na hata mwaka ujao. Nenda utakutane na ujasiri huko barabarani unapomwambia mtu habari njema ya uponyaji, kumpenda Mungu, Kuwapenda wengine. Kuipenda nfasi yake, kuwapenda majirani.

2.Ukiomba kazi . Roho ya kazi huwa inatangulia huko kazini.  itakubidi uende kwenye makampuni mbalimbali ili kuomba kazi na kupeleka  barua zako za kazi kwa imani.

Baada ya kufanya hivyo rudi nyumbani anza kumshukuru Mungu kwa kukupatia kazi. Halafu kuanzia hapo anza kufanya kazi ya kujitolea. Unaweza kufanya kazi ya Mungu, kufua au kusafisha kwa Yatima. Kusafisha mazingira, kuzibua mitaro. Yaani hapo unakuwa unafungua milango ili Mungu Afahamu kuwa unahitaji kazi. Mtaani kwako kuna wajane, wasaidie, kuna wazee , wasaidie, kuna uchafu, safisha mpaka watu waanze kukushangaa. ukiona watu wanakushangaa na kukuzarau, tambua kuwa karibu unainuliwa. karibu unapatiwa kazi  unayoitaka.

Ukimaliza kazi rudi nyumbani mshukuru Mungu wako. Haitachukua muda mrefu utaitwa kazini. Lakini uvumilivu unahitajika. Huo ndio ukweli.

Watu wengi wanamtumia Mungu wa Alpha tu , Hawamtafuti Mungu wa Omega. Wanataka wakitoka tu wapate wanachokitaka. imani haiwezi kukuokoa bila ya matendo. Onyesha imani yako kwa matendo.

Kama ukiwaza kitu, kufanya kitu fulani, halafu ukaamua kwenda huko, tayari utamuunganisha Mungu wa Alpha na Omega.

Chukua hatua kwa yale yote ambayo unawaza kuyafanya . Fanya maamuzi ili ukutane na Mungu wa Omega.

Natumaini kuna kitu umepata japo kidogo kikusaidie .

Mungu Akubariki unapofanya maamuzi ya kujitolea kabla hujaona kazi halisi unayotaka.

Tumia kilichopo mkononi  mwako , acha kutafuta kitu ambacho hakipo kwenye mikono yako.

Unao muda tumia muda wako vizuri. Kuwa makini na unachokisema, kukiwaza, kuona, unachokisikia, unachokihisi, na hata unachokifanya.

Share ili kuwasaidia wengine.

Subscribe kupata makala mpya .

Previous Mambo 10 Yanayoboresha Mahusiano Yako
Next Inapokuwa Ngumu Kupenda Tena

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.