IMANI NA KUOMBA NI VITAMINI YA ROHO


392680-Bruce-Lee-Quote-The-possession-of-anything-begins-in-the-mind-1024x576 IMANI NA KUOMBA NI VITAMINI YA ROHO

Mwanadamu hawezi kuishi bila ya hivyo.

Naamini kama ukiwa na Imani utaweza kutunza Uaminifu, Utakuwa na tabia nzuri,kama ni mtu wa shukrani, Utaona Mungu akifungua milango kwa ajili yako

Amini ndani yako mwenyewe, kuwa na Imani kwa uwezo wako! bila ya kuwa mnyonge lakini ni kwa sababu ya ujasiri na nguvu iliopo ndani yako unaweza kufanikiwa na kuwa mwenye furaha.

Kila mara kuwa wewe, Express yourself, kuwa na imani ndani yako, angalia mafanikio na kopi yako.

Tunza ndoto yako iwe hai, Tambua kuwa mafanikio huja kwa imani iliopo ndani yako, maono, uchapa kazi, uamuzi na kujitolea. kumbuka kila kitu kinawezekana kwa wale wanaoamini.

Maisha yamejaa furaha na machozi; uwe na ujasiri na kuwa mwenye imani.

Unapokuwa unalenga baraka, Mungu anakuhakikishia hizo baraka na Utele.

Kuwa na imani na vitu vidogo, kwa sababu  vitakupa nguvu ya kutambua uongo ulipo .

prayer-1024x691 IMANI NA KUOMBA NI VITAMINI YA ROHO
shukrani inapokuwa ndani yako

Moyo wenye Shukrani ni mwanzo wa vitu vikubwa.Ni msingi wa maendeleo kwenye ukweli wa kuomba, Imani, Ujasiri, Furaha, Kuridhika na Ustawi.

Kupenda Ina maana kupenda kitu ambacho hakiwezi kupendeka.Kusamehe ina maana kusamehe kitu kisichosameheka. Imani maana yake ni Kuamini kisichoaminika.Tumaini maana yake ni kutumaini  wakati ambapo hakuna tumaini.

Mungu hawezi kukupatia kitu ambacho hukiwezi kwa hio ondoa stress zako. Imani ni kuchukua hatua  wakati ambao  hujui  na huoni mbele yako hatua zilizo kamili.

Kwenye kina cha moyo wangu ,nyakati za giza, Kitu kilichonitoa huko ni maombi. wakati mwingine maombi yalinisaidia, wakati mwingine  maombi yalinishukuru,  nilichokigundua ni kwamba  Urafiki wa karibu na mawasiliano  na ushirika na Muumba mara zote hunisaidia. najua msaada wangu, ni maombi.

1956934866-faith_trust_pixie_dust_plain-1-1024x546 IMANI NA KUOMBA NI VITAMINI YA ROHO

Ni kukosekana kwa Imani  kitu ambacho hutufanya tushindwe kukabiliana na changamoto, Lakini jiamini tu. Imani ni kuamini kile usichokiona.

Naandika kuhusu nguvu ya kujaribu, kwa sababu nataka niwe sawa ninaposhindwa.Naandika kuhusu Ukarimu kwa sababu napigana na uchoyo.Naandika kuhusu Furaha kwa sababu nafahamu huzuni..Naandika kuhusu Imani kwa sababu  karibu ningepoteza imani yangu, na najua jinsi ilivyo unapovunjika moyo na kuhitaji  kuokolewa.Naandika kuhusu shukrani kwa sababu nashukuru kwa kila kitu.

Kwa kadri unavyotunza akili yako na moyo wako kwenye mwelekeo sahihi, Kila siku karibia Imani na shukrani, Naamini utapata nguvu ya kuishi  maisha ya ukamilifu na yenye kujaa furaha, maisha ya utele uliyoahidiwa.

Haijalishi kilichotokea wakati uliopita  au kitu chochote kinachoendelea sasa hivi, Hakina nguvu ya kukushikilia  wewe ushindwe kuwa na  maisha mazuri ya sasa na baadae kama utatembea na Imani katika Mungu. Mungu Anakupenda! Anataka uishi maisha ya ushindi ili uweze kumiliki ahadi zake  kwenye maisha yako ya leo.

Mungu anatafuta mtu wa kumtumia, na kama unataka kutumiwa na Mungu, Atakuja kwako. Ombi la hatari ambalo unatakiwa kuomba ni  hili; Nitumie mimi.

Nakutakia baraka na uwe na imani ya baraka hio katika maisha yako.

Tafadhali toa maoni yako , swali lako. na shirikisha wengi facebook

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Previous MOYO ULIO NA FURAHA UNATOKANA NA KUJIJALI
Next AMANI INAKUFIKISHA KWENYE MAFANIKIO YA MALENGO YAKO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.