light-in-dark-1024x624 IMANI NA MASHAKA

Imani ni Uhakika wa mambo yatarajiwayo, Ni bayana ya mambo yasionekana .

Maisha yanahitaji Imani, Inahitaji imani kusafisha meno yako, kuvua nguo zako, kuweka alarm, na kwenda kulala kila siku inapofika usiku

Kitu cha kukumbuka ni kwamba maisha sio ya kudumu. kwa hio tunapoweka alarm, tunapojiandaa kwenda kulala tunaamini kitu , tunaamini kufika kesho , siku ambayo hatujawahi kuiona. Hii ni Imani.

Kila dini ina imani yake. Kuna wanaoamini Jumapili ndio siku ya ibada, Kuna wanaoamini IJumaa ndio siku ya ibada, wapo wanaamini Jumamosi ndio siku ya ibada. Na  hii yote ni kwa sababu ya mazoea, sio kwa sababu ya imani. Unaweza kuanza imani yoyote na ukaifanya kuwa ndio imani yako na ukafanikiwa.

Ufahamu na utulivu ni moyo, imani na ibada ni kichwa, imani na ibada viko kichwani  kwa sababu  kichwa kina macho , ambayo yana maono  ya kutazama kwa ndani zaidi.

Kuna imani nyingi duniani, hakuna hata moja ya kumzidi mwingine, tena hakuna inayokuja kirahisi. Imani inatakiwa kufanyiwa kazi. Ndio  wapo wanaoweza kuamini kirahisi. Lakini wapo ambao hawawezi kuamini mpaka waifanyie kazi  na kuizoea wao kama wao.

Ukweli ni kwamba wapo wanaofanya imani kama uchawi. Lakini ukweli ni kwamba , imani ni nzuri kwetu. Wachunguzi waligundua kuwa , watu wenye imani ya kutosha wanaishi kwa muda mrefu, wanapona haraka zaidi,  na hii imehakikishwa kwa kuwa wengine wanaona kama uchawi, wengine wanaona ni sayansi, lakini ni imani ya mtu.Imani mara zote ipo hapo.

Hii inatokana na mafundisho ya kiroho na ukweli halisi uliopo. ina maana kwamba tuna imani ndani ya tunachokiamini, uwezekano wa  kuponya na kuwaponya wengine kwa Upendo na hudumu ya kiroho iliopo kwenye jamii. Ingawa tunatafuta kwa njia tofauti lakini wote tunalengo moja na tunarudi kwa Mungu mmoja.

Ndani yako uwe na utakatifu , na uwe mtu wa kutenda mema yale ambayo Mungu ameagiza .

Tunapokuwa na imani mashaka hujitokeza.

2bc74614d4756de9bfa5909823e6c021-1024x683 IMANI NA MASHAKA

Wanaokuwa na mashaka huingiza matatizo makubwa, kimvuli hukaa badala ya mashaka. Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba hatuwezi kuzuia , hata mtu anapojaribu kukaa kimya na kutafakari bado huwa na mashaka…akili haitulii…sidhani kama nafanya sahihi. Inawapata hata watakatifu. Lakini kumbuka imani  ndio inakusaidia kuondoa mashaka.

Imani ni kila kitu.uwe na imani na watu wanaokuzunguka, uwe na imani na uwezo wako.Amini kwamba kila kitu kinapita, haijalishi kina ugumu gani, ubaya gani, . uhakika wa maisha ni kwamba kila hali hubadilika. Kwa hio wanawake na wanaume tufuate imani, achilia mambo yasiowezekana.

Unapoona kitu kimekushinda , unaweza kutulia kwa muda na baadae kuanza tena, kila kitu kipo kwenye mpangilio, hata kama hatuoni  jinsi ya kubadilisha hali ngumu.tunaweza kuwa wapya, kupata nguvu mpya na kujiongeza . Acha, vuta hewa safi, tulia, refresh yourself,na anza tena. Yale yale ni ya kweli katika maisha . kama mambo hayaendi vizuri, au huwezi kukabiliana  na maumivu yaliopo,  tulia kwanza na utaanza tena upya.

when-waves-of-doubt-rock-your-faith-dont-panic-1040x326-1024x321 IMANI NA MASHAKA

This is timeless wisdom and timeless advice. Jaribu katika imani ulionayo.

Imani ya kujaribu kucontrol maisha yetu au maisha ya wengine wanaotuzunguka, sio nzuri.

Imani ni kusamehe , kuachilia, na kuwa hivyo, tunapoamini tunakuwa wakweli na kuwa wazi. Tunaishi wakati uliopo. Tunakuwa na furaha, hatuna woga , wasiwasi, wa kufikiria kesho itakuaje, inabaki kuwa ni siri ya maisha yetu na tunapata tumaini.

Barikiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here