amor-a-primera-vista Jaribu La Muda Kwa Mwanadamu

Kwa nini watu wengi hawafanyi vizuri; Unaweza kuwa hufanyi vizuri kumbe kuna mtu mwingine amebeba  jibu la maisha yako.

Fahamu kitu ambacho unataka kukifanya. kitu kinachoingia kwenye  kazi yako ni MUDA.  Unakubali kupita kwenye magumu kuanzia sasa? Miaka 5 kuanzia sasa? Miaka 10 kuanzia sasa? Utaendelea kuwa mwenye Imani?

Haijalishi unapita mapito gani, Wewe songa mbele uwe na mtazamo mzuri  na matendo yako yawe mazuri. Tunza wajibu wako endelea kutimiza malengo yako.

Anza kazi ya kuipenda nafsi yako, kumpenda jirani yako, haijalishi ni wa dini gani, haijalishi ni wa  aina gani mpende , Penda watu wote ambao unaona wanateseka kama wewe.Katika shule hii hakuna kushindwa. Zaidi sana utakomboa wakati, wala hutapoteza muda wako.

Njia za Mungu ni za juu sana kuliko njia ya mwanadamu,  Mawazo ya Mungu si mawazo ya Mwanadamu.Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake Mungu ni za juu na mawazo yake Mungu ni ya juu kuliko ya mwanadamu. Kama vile mvua ishukavyo, na theluji kutoka mbinguni wala hairudi huko, bali huinywesha ardhi na kuichipuza. Ikampa mtu apandaye mbegu na mtu alaye chakula.Ndivyo litakavyokuwa neno la Bwana litokalo katika kinywa chake, halitamrudia bure bali litatimiza mapenzi yake na kufanikiwa katika yale aliyoyatuma.

Mawazo ya wenye bidii huelekea utajiri. lakini mawazo ya wenye  pupa  huelekea uhitaji. Ukienda njia ya Mungu, utafanikiwa, njia ya Mungu ni ya utaratibu, haina haraka. Ukitaka kufanya mambo makubwa unahitaji uwe na tabia ya tofauti.

Tabia ni maendeleo ya kupita katika majaribu mengi maishani mwako na kubaki na imani  unapopitia hayo majaribu. Kamwe usiogope ukweli, kwa sababu ukweli utakuweka huru. Itakusaidia kujitambua. Amini kila kitu kitaenda vizuri kwa ajili yako. Inaweza isionekane kama kizuri , unaweza usipende, unaweza usielewe,  unaweza kuona kama hutendewi ipasavyo, Lakini Amini tu . rejea hapo juu. njia za Mungu sio njia zako…

Kataa uchungu, kataa hasira,  Amini kuwa  utapona, utafanikiwa, usijihukumu, usijilaumu.

Kwa kadri unavyokuwa na Hekima , ndivyo  unavyoweza kutawala mazingira yako, watu wanaokuzunguka, mambo ambayo hayajakamilika, na tabia ambazo hazielezeki. Fungua jicho la tatu, jicho la Hekima. tambua kuwa imani ni jicho la Mungu. Imani ni sasa hivi. Ni sasa.

8118633087_dd7f104893_o Jaribu La Muda Kwa Mwanadamu

Muda ukiingia Pesa inaingia. Lakini mazoezi ni muhimu. Kinachotofautisha watu kwenye mahusiano, biashara, familia, kazi ni Upendo .

Subscribe kupata mafunzo mapya kila mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here