Jeraha La Aibu Linaweza Kuwa Ndani Zaidi Na La Kudumu


20664159_1574326332631355_7667322420229679677_n Jeraha La Aibu Linaweza Kuwa Ndani Zaidi Na La Kudumu

Nafikiri hakuna mtu ambaye anapenda kuambiwa kuwa hana akili. Mara nyingi watu wanawaambie wengine kuwa hawana akili. Hakuna mtu asiye kuwa na akili . kila mtu ana akili.

Wengi hufikiri kuwa kusema hivyo itarekebisha tabia  kuliko  kuwaadhibu kwa njia nyingine,  wazazi wengi huwaita watoto wao mbwa, paka, mbuzi.

Wengine hutumia neno la huna akili kwa kuelezea kuwa hawakubaliani ni kitendo kilichofanyika

Aibu inatokana na wewe mwenyewe, kutokuwa na uhakika  na tabia yako. Ni tofauti na Hatia,  Kitu kinachokutesa wewe mwenyewe , kwa mtazamo wako mwenyewe na unawadhuru wengine.

Aibu inabadilisha au kufuta Tabia?  Jibu linategemea na lengo . Kwa watu wanaojali  kuhusu  mitazamo ya wengine juu yao, Aibu inaweza kufuta  tabia mbaya. Ni aina ya Adhabu, Aibu ni kitu ambacho watu wengi hukiepuka. Ingawa kuna faida ndani yake.

Woga wa  kukataliwa  unaleta mtu kujiona kutengwa  na kukosa nguvu ya kujitawala  katika kisaikolojia, kimwili na katika ustawi.

Ukiwa unamwambia mtoto kila siku hana akili na kumuita majina ya ajabu, hio sio aibu ya mtoto peke yake. ni Aibu yako. Kwa sababu ataweza akawa na tabia isiokubalika katika jamii.

Aibu inaweza kukuonyesha jinsi ulivyo kuliko jinsi unavyotenda  mambo.  Hakuna lengo lolote  lililopo hapo. Kama hisia zingine zilivyo, Aibu inaweza  kuishi muda mrefu ndani  ya mtu.

Aibu ni kitu kibaya, sio kitu cha kukubalika.  Kwa ufahamu wa wazi  tabia hio haikubaliki  kwa sababu mara nyingi  inakufanya ujisikie kuwa mwenye Hatia. Kitu ambacho kinaweza kusababisha Huzuni au stress mbaya.

Ni vizuri kama utaanza kumtia mtu moyo kwa kujitamkia maneno mazuri na kujipongeza wenyewe wanapokuwa wamefanya kitu fulani kizuri.  Aibu inaondoa heshima ya mtu. Inashusha hadhi ya mtu. Kwa hio jitahidi kuangalia ni aina gani ya aibu iliopo ndani yako . shughulikia mapema. inawezekana kuondoa. Habari njema ni kwamba kinyume cha aibu ni ujasiri.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Tiba Ya Ndoa Ni Muhimu Kwa Ustawi Mpya?
Next Najifunza Taratibu Jinsi Ya Kutojisikitikia Hata Wakati Maisha Yanapokuwa Magumu.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.