Jifunze Kumpenda Mtu Unayemuona Kwenye Kioo


1-4-1 Jifunze Kumpenda Mtu Unayemuona Kwenye Kioo

Kwa miaka mingi nimekuwa kwenye Sayari hii, Ni mekuwa nikihangaika kwa ajili ya kujikubali jinsi nilivyo kama mtu. Kujifunza kupenda kila kitu nilichonacho kama ni kibaya au kizuri.

Sikufahamu nitaanzia wapi  inapokuja kujifunza  ni kwa jinsi gani nitajipenda.

Kwa muda mrefu nilifikiria kuwa niko vizuri jinsi nilivyokuwa. Ukweli sikuweza kutoka ndani ya nyumba bila ya kupaka kitu usoni mwangu ili kujihakikishia kuwa naonekana vizuri. Lakini nilijiona niko vizuri kwa hilo.Wewe je?

Nilipojua kuwa kujipenda ni undani zaidi ya kutazama nje , au jinsi watu wanavyokuona. Ni zaidi ya nilivyofikiria . ni zaidi hata wewe unavyofikiria sasa.Lakini kama  unaelewa nakupongeza kwa hilo.

man-in-the-mirror-1024x980 Jifunze Kumpenda Mtu Unayemuona Kwenye Kioo

Nilianza kuongea na rafiki yangu kuhusu somo hili—-Ufahamu wa kipekee, Kujikubali, kujipenda n.k. Tulivyokuwa tunaongea alisema. kwa nini  hujithamini.?

Nilimtazama usoni mwake jinsi alivyokuwa na ujasiri wa kuongea. Akasema  .Hapana, kwa kweli ni sababu huna pesa ya kutosha kwa ajili yako mwenyewe.

Nilienda kulala lakini akili yangu ilijawa na maswali mengi . kwa nini siwezi kujipenda, kwa nini najiumiza , kwa nini nafikiri kuwa sijakamilika? list iliendelea…

Baada ya hapo nilianza kufanya kazi zangu kwa utofauti kwa kujali muda, nilianza kujifunza mambo mengi mbalimbali kila ninapokuwa sina kazi zingine. nilisoma vitabu, nilisikiliza video  kuhusu namna gani naweza kujipenda. niliacha makeup,  nilianza kushukuru kwa nilichonacho.

Kusema kweli nilienda zaidi ya kuandika vitu nivipendavyo.  nilianza kujipenda. nilifanya hivyo kabisa. sio kwa kujaribu.. nilianza meditation, mazoezi, kula vizuri.

Kwa kweli vitu hivi vilianza kuniletea mabadiliko kidogo kidogo. nilianza kubadilika jinsi ninavyowaza, nilianza kuona picha ya tofauti maishani mwangu. niliona thamani.

Sasa  huu muda mdogo, bila shaka , sio kwamba utaweza kubadilika kwa siku moja,  lakini ni kila siku  naendelea kukua katika hilo. kila siku najifunza zaidi kuhusu mimi kama mimi. nimeona upendo  ndani yangu.

Ninapopaka makeup sasa, ni wakati tu nahitaji, sio lazima. napaka ili kufurahia kufanya hivyo.

Ninapofanya mazoezi, sio kwa sababu nataka kuwa kama mtu fulani , au kutaka kuonekana tofauti. Lakini ni kwa sababu nataka niwe na afya nzuri, nataka niwe mwenye nguvu, niwe imara, nafanya kwa ajili yangu.

black-woman-looking-in-mirror-1 Jifunze Kumpenda Mtu Unayemuona Kwenye Kioo

Sehemu nyingine muhimu , naikubali ngozi yangu,  namkubali huyu mtu, mimi nilivyo, kwa vyovyote.  kwangu mimi hio ndio hongera yangu bora. kuwa na ujasiri  wangu mwenyewe imenifanya kuwa mwenye furaha

Watu wanaona vigumu kujisikia vizuri wao wenyewe  kwa sababu jamii  inatazama ”viwango ” hivyo ndivyo vinaharibu watu.

Kwangu mimi hili neno viwango naona ni ujinga fulani hivi.  nahitaji kusahau kabisa neno hili.

Kitu kikubwa unachotakiwa kufanya ni kujipenda mwenyewe. Fahamu kuwa una thamani. kwa sababu kila mtu ana kitu cha muhimu . iwe ni kipaji, hamu ya kitu kingine, au ni mtu wa kujali watu kwa ujumla.

Kilichopo ndani yako ndicho kinachohesabiwa.

Unahitaji kujipenda  kwanza kabisa  kabla hujampenda mtu mwingine kiukweli. Kwangu mimi hio ndio kweli, kwa sababu wewe ni mtu pekee unayeweza kufanya mambo makubwa.

 

Previous Msichana Mwenye Ujasiri Anafahamu Kwamba Maisha Yanasonga
Next Ushauri Kwa Wasichana Ambao Bado Hawajaolewa

2 Comments

 1. skudhany
  August 15, 2017
  Reply

  Ni kwel kabisa tulioweng hua hatujui thaman zet ndio mana tunakua hatujipend coz hatujal ila kw somo hili dada. Umetufumbua macho tulio wengi. You’re creative every

  • August 16, 2017
   Reply

   Asante Sikudhany. Subscribe ili uweze kupata kitu bora kila siku.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.