JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:


 

chiting-1024x682 JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:

Uaminifu ni jambo la msingi na ni chombo  pekee kinachofaa ndani ya mahusiano mbalimbali, kama  ya biashara, mke na mume, mtu na mchumba,  marafiki na familia.uaminifu ni uwezo unaoleta imani kwa mtu, na ni njia  ya kukupeleka katika  ubora wako.

Si kila mtu anaweza kuaminika, tunatakiwa kuwa makini katika hilo, kwa sababu madhara yake ni makubwa sana. Imani inajengwa na historia ya mtu mmoja ambaye anaweza kuaminika na ni katika sehemu ambazo ameonekana kuwa ni mkweli na mwaminifu.

kitu kimoja cha ajabu sana kuhusiana na imani ni kwamba , inachukua miaka  kuijenga, lakini ni dakika kuibomoa.kuna namna nyingi ungeweza kumwamini mtu au la.  fuatana nami  katika maneno haya yanayoweza kuvutia, na kuamini neno moja inahitaji uvumilivu  mkubwa.

IMANI..INACHUKUA MIAKA KUIJENGA, SEKUNDE KUIBOMOA, NA HUTAWEZA KUITENGENEZA TENA.

ix2pc4dl059jmih6ky6c JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:

1.Mahusiano bila uaminifu ni sawa na simu bila network, utacheza game tu.

2.Nakuamini. ni sifa nzuri kuliko nakupenda.kwa sababu huwezi kumwamini mtu usiempenda,lakini utampenda mtu unayemwamini.

3.Mahusiano mazuri hayahitaji ahadi,hali ya kifedha, yanahitaji tu mwanamke mwaminifu na mwanaume ambaye ni mwaminifu.

4.moja lazima liwe  linategemea imani ya watu, na imani yao kama mmoja ataweza haribu maisha yao.

5.Nafikiri tunaweza kuwa salama zaidi tunapoaamini mipango tulioiweka  kuliko tufanyavyo.

6.Ni gharama kubwa tusipoaminiana.

7.Huwezi kupona kabisa bila ya kuwa na imani japo kidogo tu katika maisha.

8.Amini  insticnt yako mwenyewe,makosa yako ni yako , badala ya kumsingizia mwingine.

9.Imani inaweza kukusaidia kufahamu vitu unavyovihitaji kabla   ya kufungua moyo.

10.Jibu linakuja pale unapomwamini mtu halafu ukagundua kuna siri imefichika.

11.Amini tu harakati,maisha hutokea katika hizo harakati,matukio mbalimbali sio ya maneno.amini  harakati.

12.Mkosoaji ni mtu ambae angeweza kumuuliza Mungu kitambulisho chake.

13.Watu wengi husema kuwa serikali ni ya muhimu,kwa sababu wanaume hawawezi kulinda wenyewe. lakini kuna mtu anasema serikali ni mbaya kwa sababu hakuna mwanaume anayeweza kuamini kumlinda mtu.

14.Harusi ni sherehe tu ya mapenzi, Uaminifu , wenza,kuvumiliana,taabu ni muda wowote uliopo ndani ya ndoa.

15.Katika Mungu tunaamini, wadudu wengine wote mpaka kuwapima.

16.Usimwamini mwanaume kupitiliza,wala bachela kuwa nae kwa karibu sana.

17. Ukifanikiwa kumsaliti mtu, usifikiri huyo mtu ni mjinga.

18.Ukiwa na moyo mzuri, unasaidia sana, unapenda sana, na mara zote utaonekana unaumia sana.

19.Msichana anapokuelezea matatizo yake, haina maana kuwa analalamika, ina maana anakuamini.

20.Tafuta mwenza anayekutia moyo katika maendeleo, ambaye hatakuangusha , atakayekufanya utikise dunia. na uamini kurudi kwako.

21.Ukiamini sana unaweza kudanganywa, na utaishi kwa taabu, labda uwe umeamini kitu sahihi.

22.Unaweza kupenda kirahisi bila ya kuamini na kukumbatia bila ya kukumbatiwa.

23.Tumezaliwa na ufahamu wa kuamini na kukubali, wengi wetu hubakia na kukubali.

24.Nikikupa moyo wangu , sitakupa mamlaka ya kunitawala, kunitukana, nakupa kwa sababu nimekuamini utalinda zaidi.

25.Namwamini kila mtu lakini siamini ushetani uliopo ndani yao.

26.Unaweza kuwa na imani yako na nguvu zako mwenyewe.

27. Uamuzi wa kuamini au wa kutomwamini mtu, ni sawa tu na uamuzi wa kupanda mti au kutokupanda  juu ya mti kuona uzuri wa tawi.na kwa sababu hio watu huamua kubaki wenyewe ndani ya nyumba, ambako ni vigumu kupata sprinter.

28 Wa kumwamini ni Mungu tu.

29.Iwe urafiki wa mahusiano , vitu vyote vinajengwa na imani.bila hivyo hakuna kitu.

30.Bila mawasiliano hakuna mahusiano,bila heshima hakuna mapenzi,bila kuaminiana hakuna sababu yakuendelea….

31.Mahusiano ni kuaminiana , na kama utacheza kiaskari ndani yake , ni wakati wa kuacha hayo mahusiano.

32.Mmoja awe ni mfano kwa watu , na  kuwafanya watu waamini, wasije kuharibu.

33.Nahofia kukosa thamani na tabia nzuri kwa ajili ya kukaripia watoto, kulaumu , kuwapa adhabu watoto, lakini naamini katika mahusiano mazuri ya wazazi na watoto wanaokua pamoja, kunakuwa na mahusiano mazuri ya kujenga imani, kuongea vizuri na kusaidiana kwa pamoja.

34.Tumepewa maisha ili yawe mazuri , maisha ya ushindi. yafanye yawe hivyo.

35.huwezi kushikana mikono kwa kutumia ngumi ngumi.

36.Jiamini usisubiri kuaminiwa na mtu.

37.Nafasi huwa na nguvu mara zote. tupia nyavu kwenye bahari ni utapata samaki.

38.Rafiki wa kweli nitampenda, yule ambaye tutakuwa nae kwa hali na mali, kwenye shida na raha.lakini wale ambao hufurahi nami wakati wa raha sio rafiki wa kweli.

39.Kuna nguvu katika imani, wewe weka nyavu zako ndani ya maji utapata samaki.

40.Ukigundua nguvu ilioko ndani ya mawazo yako, hutawaza ubaya tena.

41.njia moja tu ya kumfanya mwanaume awe mkweli  ni kumwamini.

42.Bora kutomwamini mmoja wa marafiki, kuliko kudanganywa na wao.

43.Penda wote lakini usimwamini hata mmoja.

44.Nwatamania wale waaminifu na wakweli.

45.Uaminifu wa kweli ni akiba unayojiwekea.

46. Kukaa kimya na kusubiri ukamilike na kuwa mwaminifu kwamba utakuwa mkamilifu,kunamiujiza ya akili walionayo wanadamu, imefahamika na wenye hekima.

47. uwezo wa kufungua tumaini lililofungwa,uaminifu, na sababu ya kufunga uaminifu wa ndoto njema ni wa Mungu pekee.

48.Uaminifu una nafasi kubwa kuliko  kupendwa.

49.Ubunifu unatokana na  uaminifu, amini uwezo wako usitegemee kitu tofauti na kazi tofauti.

50.uaminifu wetu katika mahusiano, unategemea makubaliano yetu, yanayoonyesha maslahi yetu, lakini pia maslahi ya watu..

51. Ukimwamini mwanaume, atakuwa mkweli kwako, waheshimu  wataonyesha heshima kwako.

52.Weka matarajio ya juu kupata mwanaume au mwanamke mwenye heshima, mwaminifu na mwenye kukuthamini kama unavyotegemea.chukua majaribio na mafunzo kwa vitendo na wape uaminifu wako.

53. uaminifu wa kila mtu ni tofauti , haulingani. usimwamini mtu.

54.Kuondoa uaminifu utafanya maisha kuwa magumu, kuamini nako kunaleta hatari.

55.Familia inayoongea manone machafu, matusi matusi ,ni sehemu ambayo wanashiriki siri zao kwa wazi wazi na wanajisikia vizuri na tofauti na wengine.hawawi bora na hujitoa kwa wengine bila ya kujali.

56.Ukiamini kupita kiasi unaweza ukadanganywa, lakini pia utaishi na maumivu kama hutaamini.

57.Ni ngumu na haiwezekani kuendelea na maisha bila kuaminiana. utakuwa kama mfungwa ndani ya jela mbayan kuliko zote. nin ya kipekee.

58. Bila ya uaminifu, maneno huwa kama sauti mbaya inayotoka kwenye kitu kibovu . uaminifu ni maneno ya maisha yenyewe.

USIMWAMINI MTU:

5 JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:

59. Mwanadamu atakuangusha kimaisha, ahadi zitavunjika,usitegemee kitu kwa mtu, jiamini tu wewe.

60.Watu watakuangusha kimaisha, usitegemee kitu kwa mtu jiamini mwenyewe.

61.Siku ya wajinga duniani mwezi wa 4 usiamini chochote,na usimwamini mtu ni kama siku zingine.

62.Usimwamini mtu , jisemee mwenyewe siri zako, usimwambie mtu na hakuna wakukudanganya.

63.Mara nyingi vitisho sio vinavyokupinga, ni wale ambao wanahitaji kuwa upande wako, na ukweli ni kidogo.

64.Usimwamini mtu huwezi kujua ni lini marafiki wa kweli wataonekana.

65.Kama mtu atakuumiza, atakugeuka na kukuvunja moyo, wasamehe maana wamekusaidia  kujifunza kuhusu uaminifu na umuhimu wa kuwa makini unapofungua moyo.

66.Simwamini mtu,nimechoka kusaidia, na nimepata watu wote na ninafanya mwenyewe.

67.Usimwamini mtu, rafiki huyo huyo,familia, utakufa kwa ajili yao watakuua.

68.Hata siku usimwamini mtu,jifunze kuhusu wao, ukiwa pamoja nao.halafu jifunze  kuamini, usipofanya hivyo utajilaumu .

69.Watu huuliza kwa nini ni vigumu kumwamini mtu,na wengine huuliza kwa nini ni vigumu kutunza ahadi.

70.Usimwamini mtu ambae anakueleza mambo ya siri za wengine,kwa sababu na zako atawaambia wengine.

71.Unapotegemea kitu cha mwisho mtu akifanye, ndicho hicho cha mwishi  hufanya kabla hujajifunza kwao.

72.Uwe makini na huyo unaemwamini, kwa sababu hata meno yako hung’ata ulimi wako.

73.Usimpe mtu siri yako,kwa kuwa usipotunza, siri yako usitegemee wengine watunze.

74.Huwezi kupata mwaminifu siku hizi , kwa kuwa  unapoanza kuwaamini unaonyeshwa kwa nini  uwaamini.

75.Uwe makini na mtu unaeshiriki nae matatizo pamoja,kumbuka si kila rafiki anaetabasamu ni mwema kwako.

76.Uwe makini na wale unaowaamini kwa sababu, mara husema rafiki zako kumbe wanakung’ong’a nyuma.

77.Niliwahi kuwakuta rafiki zangu wakinisema , pindi tu niliporudi bila wao kutarajia .usimwamini mtu.

78.Uwe makini yule unayemwamini asije akageuka , maana hata huyo ni mwongo.

79.Watu huamini kuwa ni ngumu kusamehe,mimi nasema kusamehe ni rahisi  kuliko kujifunza kumwamini mtu kwa mara nyingine.

80.Damu ni nzito kuliko maji, lakini vyote huvuja. Usimwamini mtu.

81.Usimpe mtu moyo wako,kama hutaweza kumwamini.

82. Ni ngumu kuwaamini watu ambao tayari wameoonyesha kuwa hawakuamini.

83. Mimi naweza kukusamehe, lakini sio mjinga  wa kukuamini tena.

84.Kuna sababu mbili tu kwa nini watu hatuaminiani,1.hatufahamiani, 2.kwa sababu tunawafahamu.

UAMINIFU ULIOVUNJIKA.

break-up-sofa JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:

85.Hisia mbaya duniani  ni kufahamu kkwamba ulitumika na kudanganywa na mtu uliekuwa unamwamini.

86.Ni ngumu kumwamini mtu ambae ulijiachia kabisa kwake , halafu akakugeuka.

87.Kitu cha kuhuzunisha ni pale unapovunjika moyo na kuogopa kumpoteza mtu ambae unamwamini na kumpenda, halafu akakuvunja moyo,ni ngumu kupona.

88.Kitu kibaya zaidi duniani ni pale unapomwamini mtu na kila alichokuambia ni kweli, kwamba nakupenda, nakuhitaji, nakujali, unanifanya niwe na furaha, halafu mwisho unagundua kuwa sio peke yako uliyeambiwa hivyo.

89.Umbali hauharibu mahusiano, hofu , wasiwasi ndio uharibu.

90.ukiumizwa ni ngumu sana kukubali kuwa na mtu mwingine , utaogopa.

91.Uaminifu ni nguzo ya mahusiano, kosa dogo huharibu vitu vyote.

92.Ukisema utafanya kitu na hukifanyi unajidanganya, ndio maana huaminiki.

93.Mmoja anaposaliti kwenye mahusiano, hakuna sababu ya kubaki, kama anakupenda asingekusaliti.

94.Uaminifu unapioondoka kwenye mahusiano hakuna tena furaha.

95.Pale ulipogeukwa usingepata imani kwanza.

96.Siangalii kwamba umenidanganya, naangalia kuanzia sasa na kuendelea siwezi kukuamini.

97.Umbali unaweza kuwa ni changamoto ngumu katika mahusiano, uaminifu unapokosekana, wasiwasi huzaliwa.

98.Mahusiano bila uaminifu ni kama gari bila mafuta, unaweza kukaa humo unavyohitaji, lakini haliendi popote.

99.Wasichana wamejifunza, itachukua miaka kujenga  uaminifu, lakini  ukiwa na dukuduku utaharibu imani.

100.hakuna kinachoshindikana duniani, lakini uaminifu wa mara ya pili, ule uliovunjika umeshindikana.

101. mara nyingi uaminifu ni ule uliovunjwa na kuamini ni pale wewe unapoharibu.

102.Watu ambao hawakuamini kabla ya maelezo, hawatakuamini hata baada ya maelezo. uaminifu sio kitu cha kuomba upewe muda uonyeshe.

103.Ukiongea uongo mwanzo tu , na ukweli wako utakuwa wa kujiuliza.

104.Kitu cha kwanza ambacho tunataka watu wakifanye, ndio hicho ambacho wamefanya  hata kabla ya kujifunza kutoka kwao.

105.Kama utaanza mahusiano kwa uongo , utapoteza uaminifu wako , matarajio yao ndani yao pale ukweli unapoonekana.

106. Usivunje vitu 4 maishani mwako , ahadi,uaminifu, mahusiano,moyo wako wa upendo, kwa sababu unapovunja havipigi kelele lakini inaumiza sana.

107.Pole hufanya kazi pale kosa linapotokea., lakini samahani  haifanyi kazi pale uaminifu unapovunjika, kwa hio, kwenye maisha fanya makosa lakini usivunje uaminifu.

108.Mimi naweza kukusamehe lakini sitakuwa mjinga wa kukuamini tena.

109.Kitu kinachoumiza zaidi ni pale unapokuwa na mazoea halafu mara mahusiano yanavunjika,halafu baadae unagundua kuwa ulikuwa unadanganywa na kuonewa na hata hukustahili kuujua ukweli.

110.Ukifanikiwa kumsaliti mtu,usifikiri ni mjinga, tambua kuwa mtu huyo anakuamini, kuliko hata unavyohitaji kuaminiwa na yeye.

111.Mtu anavunja uaminifu, usifikiri ni mjinga kuwaamini wao, hukufanya baya ila ni watu  ambao hawastahili kuaminiwa.

112. Unapoanza kushangaa ni vipi naweza kumwamini mtu, ni kwa sababu unajua huwezi kuamini.

HAKUNA UAMINIFU.

unnamed JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:

113.Tumekutana tumezoeana,tumependana, tumetoka pamoja, tumewekeana ahadi. umenisaliti, basi, tumefuta, muda wote huo tupo ilimradi tu pamoja. lakini sio sisi tu bali ni pamoja na wengine.nafikiri hakuna tena uaminifu.

114.Kama hakuna uaminifu hakuna kitu cha sisi.

115.mapenzi hayawezi kukaa bsehemu ambayo hakuna uaminifu.

116.Kama leo hakuna uaminifu hata kesho hakuna.

117.Hakuna uaminifu , hakuna mahusiano ni mradi watu wawili wanatumia muda wao pamoja.

118.Bila uaminifu hakuna uaminifu, na bila uaminifu hakuna urafiki.

119.Hakuna uaminifu ,hakuna imani, hakuna ukweli katika wanaume wote wanaoapa uongo na  wanaofanya hayo yote ni dhahili hakuna uaminifu.

120.Mahusiano bila uaminifu ni kama simu bila network  utakachofanya ni kucheza game.

121.mahusiano hukoma kwa sababu ya maneno,uongo, usaliti, social networks, kuwa feki, hakuna uaminifu kwa wengine kukosekana kwa ngono na kukosekana kwa mapenzi.

122.Mungu nifanye chombo chako cha amani palipo na chuki, palipo na kutofautiana, palipo na giza, mwanga na pale palipo na huzuni kuwe furaha.

123.Hakuna uaminifu,hakuna imani, hakuna ukweli kwa wanaume.

IMANI YAKO WEKA KWA MUNGU.

1907-1-1024x512 JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:

123.Mawazo yenye wasiwasi ni hasara kubwa, kwa sababu chochote au vyovyote alivyonavyo Mungu  kwako ni vyako. mwache Mungu aonekane.

124.Weka imani yako kwa mungu, na kwako mwenyewe.fuata moyo wako mara zote, uwe na tumaini linaloishi katka kila ufanyacho.

125Mungu atakuongoza njia pale pasipokuwa na njia.

126.Uwepo wa Mungu upo wakati wote  kuwajibu wenye mahitaji  na wenye imani kwake.

127.Mungu nifanye chombo chako cha amani palipo na chuki iwe tumaini, palipo na giza  kuwe mwanga, na pale palipo na huzuni pawe na furaha.

128.Mungu hukutana na mahitaji ya kila siku sio kila wiki au majira,  atakupa unachohitaji wakati kinapohitajika.

129.Kuweka imani kwa Mungu ni kujihakikishia  ujasiri kwake.

130.Mungu hajakuita ili akuache, amekuita ili akuongoze.

131.Usiogope kumwamini kwa ajili ya baadae isiyojulikana kwa mungu anayejulikana.

132.Maisha yakiwa magumu kumbuka Mungu yupo pamoja na wewe, na atafanya maisha kuwa rahisi.

134.Mungu kama ni mapenzi yako na yafanyike, lakini mungu kama sio mapenzi yako basi nionyeshe njia ya kupita ulioiandaa kwa ajili yangu.

135.Uwe na uhakika kuwa uko kwenye zamu yako leo, na mwache Mungu ashughulikie.

136.Ukiogopa ni dalili kuwa huo ni woga,  acha woga kwa sababu Mungu yupo anakulinda.

137.Ukiwa umechoka omba nguvu  kwa Mungu, wakati huwezi kuongea , ongea na Mungu, ukiwa mpweke , Mungu yupo nawe.

138.Maisha yana changamoto unapokuwa unafikiria sana, mwache Mungu aongoze hatua zako.

139.Vyovyote ulivyo ndani ya roho yako, kwamba unamjua Mungu,anayekuelekeza kufanya jambo, haijalishi kuna  mawzo ya aina gani yanayokukwamisha, songa mbele.

140. Najua Mungu anakuwazia mawazo mema na ana mpango mzuri na wewe katika maisha yako.

141.Kumwamini Mungu ni hekima kubwa, kumfahamu mungu ni amani , kumpenda Mungu ni ni nguvu ya tofauti, imani kwa Mungu ni ujasiri.

142.Ninapopita katka magumu huwa najikumbusha  kuwa Mungu yupo upande wangu.

143.Kufuli haliwezi kutengenezwa bila ufunguo, hivyo Mungu hawezi achia tatizo bila majibu. ni hitaji tu la kufungulia linalohitajika.

144.Taarifa mbaya ni maisha sio rahisi, taarifa nzuri ni  usitegemee akili zako mwenyewe , mtegemee Mungu.

145.Pamoja na kuzoea ugumu wa maisha fahamu kwamba Mungu anaweza kila kitu, mwamini yeye na uache mapenzi yake yatimie.

146.Usijidharau,kila kitu Mungu anaweza kukufanyia katika maisha yako.mwamini tu.

147.Mungu ana mpango na kila mtu pamoja na mimi, huwa sifahamu ni nini, lakini nina imani katika hukumu zake, mapenzi yake ni mapenzi yake, yeye hutawala sio mimi.

148.Kma hajakufanyia vizuri , utambue sio mume ambae Mungu amekupa, mwanaume ambaye amekuchezea jitie nguvu mwache aende, .

149.Maisha ni jinsi unavyoyaweka kwa hio endelea kuyapigania, na mara zote kumbuka kuwa Mungu yupo nawe haijalishi unapita vipi. usikate tamaa kwa imani ulionayo.

150.Endelea kuomba na kupigania, kwa msaada wa Mungu na nguvu yako ya ndani utapita tu. utashinda.

-Hivi ni kwa nini Mungu.

-kazi yangu ni kuwapenda watu sio kuwabadilisha.

shirikisha rafiki na familia  maneno haya mazuri , pia toa maoni yako upendavyo karibu sana.

 

 

 

 

 

 

 

 

Previous JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:
Next Mume Akataka Talaka, Kwa nini?, Kwa Sababu Eti Mke Hafanyi Kazi:

1 Comment

  1. Avatar
    February 23, 2019
    Reply

    kazi njema.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.