JINSI YA KUONDOA SUMU YA WASIWASI NDANI YA MAISHA YAKO:


Paleo-PI-Blog-Photo-1024x769 JINSI YA KUONDOA SUMU YA WASIWASI NDANI YA MAISHA YAKO:

Wasiwasi, mashaka , hofu  limekuwa ni janga la  dunia.

Tuna wasiwasi ya kwamba watu wanatufikiriaje, kwa kila tunachofanya.

Tuna hofu ya kujishuku kuwa watu wanajisikiaje tukifanya hiki.

Tunaogopa maisha yanayokuja.

Tunaogopa hata maisha yaliopita tayari.

Tunaishi kwa kuhofia vitu vidogo vidogo na vitu vikubwa.na hivi vitu ni kawaida huwa vinatuathiri kimwili , kiakili na kihisia pia.

6a00d83451ece569e2014e8ae8de25970d-horz JINSI YA KUONDOA SUMU YA WASIWASI NDANI YA MAISHA YAKO:

Wasiwasi wetu umetufanye tuone kama ndio kusudi . ambao mfumo wake ni wa utawala wa yale yasiotawalika. tunafikiri woga wetu utaleta  nafuu na kutuondoa katika matatizo. lakini mara zote ni kunyume kabisa.

Unaogopa kuchelewa, na ukiona taa nyekundu tayari imewaka ndio kabisa ,kumbe kama ungetulia   mambo yangeenda kwa urahisi kabisa. lakini ndio wasiwasi wako umekuathiri.

Mawazo yetu yamekuwa na mazoea ,  tunapokuwa kwenye matatizo hatupati majibu kwa urahisi. zaidi sana tunaongeza stress inayotufanya tuone kuwa tayari tupo kwenye taa nyekundu, hapo ndio utaona  hofu ilivyo wazi kabisa.

FUNGULIA KESI HIO HOFU NA WASIWASI.

1.Pata Mpango Mahiri.

Huwezi kudhibiti kila kitu ulicho nacho, lakini unaweza tu kujiandaa  kwa kinachokuja , kama una wasiwasi na maisha yajayo, wewe yafungulie kesi mbaya. angalia wakati huu uliopo  je unaogopa ukweli? inawezekana labda unaogopa kidogo, lakini ukishajua ni hatua gani utachukua ,utaanza kuamini na utaamka ukiwa mshindi.

Jiambie kuwa huogopi  na huna wasiwasi na kitu hicho.

2.Punguza Kusoma Na Kuangalia Habari Mbaya.

1a11c-information-overload JINSI YA KUONDOA SUMU YA WASIWASI NDANI YA MAISHA YAKO:

Hakuna tatizo la  kusikiliza na kuangali yanayojiri, lakini endapo yanakuletea hali ya hofu na wasiwasi  inabidi uache. kwa sababu kuendelea kuangalia na kusoma utaiona dunia mbaya na watu wake wote ni wabaya. utaona dunia haina maana  kwako. ni dunia hatari, ni ya shetani tu.

Ukitaka kusoma au kusikiliza na kuangali habari , basi fuatilia zile habari za kukutia moyo, hapo utaona dunia ni nzuri na utaendelea kufikiria vitu vizuri , Anza kuchagua na kuruhusu vitu vizuri ndani ya akili yako.

3.Ongea Au Andika.

5StepsToChangeYourLifeAndMakeItStick-1024x574 JINSI YA KUONDOA SUMU YA WASIWASI NDANI YA MAISHA YAKO:

Hofu inatokana na mitazamo,kama utaelewa ni kitu gani kinakuletea hofu, fikiria ndani ya akili yako zaidi na zaidi utaona utatoka. kuandika au kuongea  inasaidia endapo utapata mtu unaemwamini. kwa sababu atakusaidia kujua na kupata mitazamo mipya na kupata majibu mazuri.

4.Uwe Makini Na Unachokidhibiti.

Hata kama una wasiwasi na  kitu unachokisema  ya kuwa ni  nini mtu anachofikiria kuhusu wewe, au ni nini kitatokea katika maisha yako yajayo, utakuwa unajisumbua sana  kwenye hivyo vitu. kwa sababu hutaweza kuvidhibiti, badala yake utaweka kisicho na muhimu na kitakuletea stress.

Unaweza kuviacha vikaendelea kwenye mzunguko wake, wakati huo wewe unajitahidi kuangalia kile unachoweza kukidhibiti.

2047844c-a85a-4c4f-ba1e-10dcbdb1820d-600_q60 JINSI YA KUONDOA SUMU YA WASIWASI NDANI YA MAISHA YAKO:

Unataka kuomba msamaha?.

Fanya unachoweza, na wasiwasi wako utaondoka kama kawaida.

HIVI NI KWA NINI MUNGU?

shirikisha familia na marafiki makala hii nzuri na utoe mawazo yako.

 

Previous VITU 7 AMBAVYO VITAKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO
Next MAPENZI YENYE MVUTO WA KWELI.

3 Comments

 1. Avatar
  Fares Masanya
  April 22, 2016
  Reply

  Nimeipenda sana makala hii. Inafundisha na inaelimisha pia.

  • Avatar
   April 28, 2016
   Reply

   Asante Fares Masanya , endelea kufuatilia mafunzo mengine mengi utafaidika nayo .

 2. […] -jinsi ya kuondoa sumu ya  wasiwasi ndani ya maisha yako. […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.