Jinsi Ya Kutafuta Mume ,Mke Kwa Njia Ya Mungu


14446003_1121900937902293_6861290636277518833_n Jinsi Ya Kutafuta Mume ,Mke Kwa Njia Ya Mungu

Unapataje mke au mume kwa njia ya Mungu.

Kila mtu kwa wakati maalumu anahitaji awe na mwenza sahihi  ambaye ameumbwa au kutengenezwa kwa ajili yake. jinsi gani basi unaweza kupata mwenza  katika Maisha yako.

Kupata mume au mke kwa njia ya Mungu , Unahitaji  Uelewa na Hekima. Swali ni kwamba. Mtu anatakiwa kutafuta mume au mke ? na Unatakiwa kufanyaje kwa njia ya Mungu?

Njia ya maneno ya kumtafuta mke au mume

Kwa sababu kila mtu anahitaji kupata mwenza wa maisha yake, Kipo kitu kibaya ambacho huwa kinaingilia utaratibu wa mtu  na ndio maana wengi huangukiwa  mahali ambapo sio sahihi.

Tuangalie Sifa za Mwenza Sahihi.

landscape-1445021142-internet-sex-addiction-1024x512 Jinsi Ya Kutafuta Mume ,Mke Kwa Njia Ya Mungu

Wanadamu wengi hawana uelewa na hawana hekima . Makanisa mengi yanafundisha watu jinsi ya kutafuta mwenza kwa maneno.  Na agenda ya shetani ni kukuondolea ukweli wa maneno ya Mungu ya kweli na wanakuwa hawaoni kabisa.

Turudi kwa Muumba mwenyewe. 

Mungu alimuumba Adamu na akampa kazi ya kutunza Bustani katika bustani ya Edeni.  Na Mungu akamuumba mwanadamu kwa udongo, na akampulizia pumzi ya uhai, na akawa  roho iliyo hai.  Mwanzo 2:7-8

Adamu alikuwa peke yake bustanini,  Na humo kulikuwepo wananyama  na mimea,  Lakini hakuhisi upweke.Lakini Mungu alijua upo wakati ambao atahisi upweke na atahitaji mwenza.

Mungu aliona hilo, si vema  Adamu kuwa peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Mungu alichukua hatua , hakwenda moja kwa moja kumpa Adamu msaidizi kwa sababu alikuwa yuko vizuri na aliyetosheka. Mungu akaanza kumtengenezea upweke, akampa kazi  ya kufanya. Akampa wanyama wote awataje majina. Naye Adamu alifanya kazi hio ya kutaja majina yao lakini hakuona mtu wa kumsaidia.

201410-tows-30-949x534 Jinsi Ya Kutafuta Mume ,Mke Kwa Njia Ya Mungu

Wanyama na ndege walikuwa wawili wawili.  Kila mnyama au ndege alikuwepo mke na mume. lakini Adamu hakuona wa kufanana naye.  Na kwa hali hio akajisikia mpweke na alihitaji mwenza.

Kumbuka hapo tayari ana kazi, ana wanyama, ndege, na wengine.

Lakini Mungu hakumpa nafasi ya kutafuta  kampani.

Ndipo alipompa usingizi mzito, akatoa ubavu wa Adamu na Kumtengeneza mwanamke, Na baada ya kumaliza alimleta kwa Adamu.

Ni mungu ndiye Aliyemuumba Adamu na alimtengeneza mwanamke, Sio  kwamba Adamu alimtafuta, Mungu alimleta, na wala hakumwambia kuwa akatafute mwenza.

Hapa tunaona kuwa kazi ya Adamu ndio ambayo ilisababisha kuletewa mwanamke. Kazi ndiyo inayochagua mwanamke wa kuoa sio  Akili ya mwanaume.

Ndio maana kwa mara ya kwanza tu Adamu alipomuona alitambua kuwa amepata mwenza sahihi wa kumsaidia katika kazi yake. Akampa jina kwa sababu alitoka katika yeye.

Somo Kuu Ambalo Tunajifunza Hapa Kutoka Kwa Mungu Kumtengenezea Adamu mwenza.

1.Ulipoumbwa na kuwekwa kwenye bustani yako ya Edeni , yaani Ulimwengu wako,Hukuhisi upweke wa kuhitaji mke au mume.

Unapokuwa mdogo huhitaji mwenza  na wala unakuwa hujui chochote kuhusu jinsia nyingine. Lakini Mungu anajua kuwa upo wakati utahitaji kuwa na mwenza. Lakini kabla ya hapo unaishi ukiwa vizuri na unakuwa na utoshelevu mkubwa, hakuna upweke.

2.Hata kabla ya kutengenezwa au kuumbwa, Mungu alijua kuwa si vema uwe peke yako na anakuwa amekuwekea wakati ambao utajihisi upweke.

Ndio . Mungu anajua. Ndio maana alimpa Adamu kazi kwanza, Hakumpa mke kwanza. Na hii sio kosa. Alifahamu kuwa , mwanaume kuwa mkamilifu ni lazima awe na kazi na atawale vitu kwanza , ndio ataweza kutambua upweke na kuhitaji msaidizi.

3.Kwa wakati Sahihi, Mungu aliweka ili Utambue kuwa U mpweke na unahitaji mwenza.

Mtu anapewa kazi kwanza, huyo ni mwanaume. Halafu  atazidiwa na kazi hizo na kuhitaji msaidizi.

4.Baada ya  kutambua kuwa Unahisi upweke  na unahitaji mwenza,Mungu anakutengenezea  kwa kukulaza usingizi .

Unapohisi upweke wa kuhitaji mume au mke , usiende kutafuta, badala yake lala usingizi. Watu wengi hawakubaliani na Neno la Mungu ndio maana wanajikuta kukosea katika maisha . Kwenda kutafuta kwa akili ya kibinadamu huwezi kupata mtu sahihi.

Unapohisi upweke na kwenda kulala ndio wakati ambao Mungu anakutengenezea Mwenza sahihi.  Kulala ina maana kwamba huendi kutafuta, Bali akili yako , roho yako na mwili wako vinakuwa katika utulivu. vinalala.

Kwa kufanya hivyo , Mungu atakuwezesha  kupata mwenza sahihi , kwa wakati sahihi na mahali sahihi.

5.Ni Mungu Ndiye Anayekuletea Mtu wa Kufanana  Nawe.Mtu aliyemuumba kwa ajili yako.

Tulia, jiweke fiti,  Lala bila wasiwasi, Mungu atakuletea Mume au mke  Kwa wakati sahihi na mahali sahihi.  Endelea na maisha yako, ona kuwa hakuna unachohitaji, kama vile hakuna unachohisi katika kuhitaji. Mtazame Mungu na atakuletea mtu sahihi. Na utakapomuona kwa mara ya kwanza , utasema kama Adamu. huyu ndiye mifupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu. ataitwa mwanamke kwa kuwa ametoka katika mwanamume.

Utasema huyu ndiye. 

Watu ambao wamefuata utaratibu wa Mungu wamekutana na wenza sahihi katika maisha yao. Jaribu kuuliza  na utagundua kuwa  mara ya kwanza walipokutana walitambuana. Na jibu lilikuwa Ndio.

Msubiri Mungu. Unaweza kusubiri.

Ukiruka maandiko ni lazima Utateseka. Ukiingia kwenye ndoa kwa akili zako, bila ya kupata kazi kwanza  ni lazima kuteseka kwa mwanaume. Mwanamke ukiingia mahali ambapo sio mahali pako utateseka.

Kama tayari umeingia kwa makosa , Tubu, Tubu Tubu.

Tubu Kwa Ajili ya Ufalme wa Mbinguni Uje Mkononi mwako.

Subscribe kupata makala mpya .

Previous Kufikiri Nje Ya Box Imepitwa Na Wakati. Badala Yake Fikiri Kwa Mapana Ya Hali Ya Juu
Next Huyu Ndiye Msichana Anayejifunza Kuipenda Nafsi Yake

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.