upload_2017-8-14_11-34-29 Kaa Kwa Sababu Ya Upendo Sio Woga

Kwa nini kujaribu na kujaribu kwa bidii kukaa kwenye mahusiano  yasio na upendo na ambayo hayana Furaha, lakini  unakaa kwa woga.

Uchumba kwenye jamii siku hizi ni mgumu,  ni kama kutaka shamba la kumiliki mwenyewe. Mara mtu anapompata mtu wa kuwa naye anatamani  adumu naye. Hata kama kwa kurekebishana ndani kwa ndani. Hata kama hakuna furaha ndani ya mahusiano hayo. Lakini anakuwa anajipa matuamini kuwa yatakuwa mazuri.

Kusema kweli hakuna mtu anayependa masikitiko .lakini kwa nini  watu wanaamua kukaa katika mahusiano ambayo hawana furaha wala upendo?

Fikiria maisha kabla ya kuingia katika mahusiano hayo , ulikuwa na furaha, ulikuwa huru, ulikuwa na amani, ulifanya kitu ulichokitaka.

images-2-1 Kaa Kwa Sababu Ya Upendo Sio Woga

Halafu ukakutana na mtu na mkapendana , na hapo hapo mambo yakabadilika.

Mwanzo yalikuwa mazuri , na wakaanza kutengeneza box lao la kuweka dhamana yao au kifungo chao

Halafu mambo yakaanza kubadilika  kwa sababu ya  sababu tofauti tofauti. watu wanaweza kukutana na huzuni, masikitiko, maisha yasio na ukamilifu kwa sababu ya hilo box. hawawezi kutoka.

Wanaweza kuanza kusema wanaishi kwa sababu ya msingi. Huenda wana watoto, au wameshirikishana kumbukumbu nyingi, wamekuwa pamoja kwa miaka mingi na wamewekeza mambo mengi ndani ya box lao.Hawataki kupoteza chochote walichokitengeneza.

wanachokikosa-wanawake-1024x538 Kaa Kwa Sababu Ya Upendo Sio Woga

Wanaweza kuwa wanafikiri bado wanaweza kuyaweka sawa mahusiano yao. Wanatazama kila kitu ndani ya box na kuona kama kuna maendeleo  na kutaka kuweka vizuri mambo yao. wanaamini kwamba Upendo ni mgumu na inahitaji nguvu kuutunza.Au wanaweza kufikiri kuwa hawajajaribu kufix baadhi ya mambo.

Wanadamu wameumbwa na tabia. unapokuta kitu kizuri na kinakupa furaha  unakipigania, kwa wengi wetu tunakaa kwa urahisi. hio ni kushindwa kutekeleza. box liko salama na linajulikana.

Tatizo la Box

Tatizo la box  ni kwamba linafunga watu kutoka kuwa na ufahamu  wa  kilichotokea ndani na nje  ya mahusiano yao.

Ingawa sababu kubwa inakuwa ni watoto au mali  mliochuma pamoja,  Watu wanahitaji kujua kwa undani kabisa sababu ya kuwafanya watake kukaa katika mahusiano.

Kama watu watatumia nguvu nyingi kuwekeza kwenye box,  Vitu mlivyoshirikiana, watoto, mali, hisia na kumbukumbu na kushindwa kuachilia. hii kitu inaumiza; Ina maana kama mtu ametumia muda mwingi katika hili hawezi kushindwa  kuwekeza katika njia isio sahihi. wamejifungia hapo na kukubali maumivu na kupoteza muda mwingi bila ya furaha ya kweli.

Kama wanadamu tumeumbwa kukumbatia kisichojulikana . ni kawaida yetu kushangaa kitu kinapotokea ambacho hatukutarajia. lakini kila mtu ni vizuri kama hataongozwa na uchunguzi wake bali katika maamuzi ya kutaka kufahamu maisha ya kweli yenye furaha mbele yake . Na hayo atayaona tu pale atakapoamua  maamuzi magumu.

Maamuzi haya ni ya mtu binafsi sio ya kuongozwa na mwanadamu mwingine. Ni kuchagua . tumepewa Hiari. Uhuru wa kuchagua Kuteseka au kutafuta amani. Ukweli  mara zote ni uamuzi wa mwisho.

Sio kitu rahisi , hasa kama wewe ni mtu unayejali mtu mwingine.

Kama unataka Furaha ya kweli, Afya na ukamilifu  ni vizuri kuongea  yalio magumu, Kuchukua risks. Kukaa mahali ambapo unajiona kabisa unapotea, unaugua kila siku, huna amani, furaha kwako ni ndoto, woga umekujaa, unajilaumu, huna upendo wa kweli na unamuumiza mtu mwingine na inakudhuru wewe mwenyewe, mwenza wako na mahusiano. Uamuzi ni wa kwako. Hakuna atakayekuamulia.

Kama kweli unampenda mwenza wako, Uwe na Ujasiri wa Kukaa. Kama sio, Uwe na ujasiri wa Kusema ukweli na kuondoka.

Vinginevyo badilisha mtazamo wako, kufikiri kwako, kutenda kwako. shughulika na nafsi yako mpaka mambo yakae sawa. Lakini sio kujaribu kumbadilisha mtu mwingine. Wewe.

Subscribe kupata makala mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here