Kabla Hujampata Mtu Wa Kudumu Kwenye Mahusiano ,Jitafute Kwanza Wewe. Ujitambue.


photo-1502767882403-636aee14f873 Kabla Hujampata Mtu Wa Kudumu Kwenye Mahusiano ,Jitafute Kwanza Wewe. Ujitambue.

Hutapenda kusikia hili, Lakini hujawepo hapa ili kumtafuta mtu, Ndioo. Unaweza ukawa umejidanganya mwenyewe kuwa utapata mtu wa kudumu maishani mwako ukasahau kuwa kuna kitu ambacho kitalazimisha huyo mtu asiwe  wa kudumu.

Wakati mwingine jaribu kutambua kuwa unahitaji kujitafuta wewe ili uishi maisha ya furaha na ya kudumu.  Lakini ukiwa na mawazo ya kupata mtu wa kudumu utajikuta unaondoka wewe kwa kufa au kwa talaka baada ya kuishi naye kwa muda wa miaka michache sana.

Utambuzi huu usikuchanganye.Ni lazima ukuinue .  ukupatie juhudi  ya  kutoka katika mazingira mabaya  ya kujiwekea kipaumbele cha peke yako, kwamba utapata mtu wa kudumu maishani mwako.

Bonheur-pourquoi-les-gens-heureux-sont-en-meilleure-sante Kabla Hujampata Mtu Wa Kudumu Kwenye Mahusiano ,Jitafute Kwanza Wewe. Ujitambue.

Unaweza usikubaliane na hili. Kwa sababu wazo la kupenda  ni tamu , Lakini kuna cha zaidi katika haya maisha kuliko kupata tu mtu wa kuwa pembeni yake. Marafiki watakuja na kuondoka ,  Mahusiano yanaweza kuanza na kufika mwisho.  Kitu pekee kitakachobaki ni wewe.

Huwezi kujivunja mwenyewe. Huwezi kukua mahali  tofauti na wewe. Huwezi kujiepuka mwenyewe.  Hata kama kuna tatizo gani lipo ndani yako.  Ni lazima ujifunze kujipenda, Kwa sababu hutaweza kujitupa popote.

Watu wanaokuzunguka hawawezi kuona wema wako  kama hawajakaa na wewe,  Lakini wewe utajua kitu gani ulichonacho. hutakiwi kujidharau, kulalamika, kujilaumu, usijione mzigo, kwamba umepoteza nafasi na uwezo ulionao.

Ni lazima ujifanyie wema ambao ungeweza kumfanyia mwingine. wapende watu lakini usiwaogope. usiwafanyie watu kitu ambacho wewe hutaki ufanyiwe.

Jikubali mwenyewe. Jisamehe mwenyewe.  Jitafute zaidi ili ujitambue.

Badala ya kwenda movies na marafiki, badala yake  fanya kitu kingine. kuwa huru  na ustawi peke yako. Jiburudishe bila kuwepo na mtu mwingine ambaye anaweza kukuibia  hewa yako.

o-HAPPY-WOMAN-facebook-1024x512 Kabla Hujampata Mtu Wa Kudumu Kwenye Mahusiano ,Jitafute Kwanza Wewe. Ujitambue.
anajifurahisha na kahawa.

Hutapata ukamilifu kama kila mara unasubiri  mtu fulani  akukamilishe. Unavyo vitu vya kutengeneza furaha yako. huna haja ya kutafuta, jikubali mwenyewe.

Hata kama unahitaji kuolewa au kuoa ni vizuri kama utajitafuta mwenyewe kwanza kabala ya kukutana na mtu mwingine kwenye mahusiano. Kwa sababu  mahusiano hayataweza kudumu kama hutaweza kujitambua  ndani yako. Wala usitake kutafuta kwa mtu.  Ni lazima uwe na mawazo yako mwenyewe, maamuzi yako,  Sababu yako ya kuishi.  Huwezi kutegemea mtu kwa sababu na wewe ni roho.

Bila shaka kupata mtu wa kudumu  isiwe ni lengo la mwisho.  Isiwe ndio kitu  cha kutaka kukifikia.  Lengo lako pekee liwe ni kuwa mtu mwenye furaha siku zote. Mtu asikuharibie furaha yako.  Watu wanaojiamini, wanaojikubali, wanaojipenda , ni watu wanaompenda Mungu. Haijalishi wako katika mahusiano au  La.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Kwa Nini Ni Ngumu Kupata Upendo Ndani Yako (kujipenda)
Next Ili Ufanikiwe Lazima Ushinde Vita Ya Ndani

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.