Wakati mwingine kwenye maisha tunajikuta tumefika mwisho. Hatuwezi kusogea. hujui ni wapi pa kuelekea. Haijalishi upo stage gani kwenye maisha yako, kama hufurahii ulichonacho, au huna uhakika katika kuendelea nacho, unahitaji utathimini upya.
Ulipokuwa shule ulikuwa umechagua masomo ya kukuwezesha kupata kazi ya kukupeleka miaka 50 mbele katika maisha yako. Ni maisha ya mashaka, utajuaje kama yatakupelekea furaha maisha yako yote, Hasa ikiwa ndio kwanza ulikuwa na miaka 17, 18.
Huwezi kujua ni kitu gani kitaweza kukupatia furaha hata sasa hivi.
Huwezi kujua mambo yote ya baadae. maisha yamejaa mambo mengi yanayokuja na kuondoka. Lakini kama tutafanya kazi ambazo tunazipenda, itaturahisishia kufurahia maisha kila siku.
Jaribu kuwa vizuri sehemu ambayo sio nzuri.
Mara nyingi maisha huwa yanachanganya, wakati mwingine tunakosa pesa. hatuwezi hata kununua kitu ambacho tunakitaka. Kama una kitu unataka kifanikiwe utahitaji uweze kuishi katika hali ambayo sio nzuri ili ufanikishe.
Maisha ni uhakika. Endelea.
Mambo hutokea. Nilifikiri nimefanikiwa, nilipokuwa na kazi nzuri, nyumba nzuri. Lakini siku moja ikatokea moto, vitu vyote viliungua. Na wakati huo nimejikuta nina miaka 40, halafu nilijikuta ni mjamzito, nilichanganyikiwa. lakini niliamua kuhama mji. Nilichukua yanayowezekana tu kichwani mwangu. Kila kitu kibaya kinachotokea hufungua mlango wa kitu kizuri.
Hii ni kweli , kwa sababu huwezi kurudi nyuma, bali ni kuanzia hapo ulipo. Kama hutafanya maamuzi yako sasa hivi hapo ulipo, hutakuwa na kitu cha kuonyesha. Lakini utabaki kupost facebook, na kukaa kwenye TV shows. Kama kweli unahitaji kufanikiwa ndoto yako. Na kuwa mtu maarufu kama wengine wenye majina, Anza hatua ndogo. Jitoe kwenye mitandao na uanze kujifanyia kazi wewe, Anza kufanya kazi kwa bidii sasa. Hutaweza kwenda popote kwa kufikiria bila ya vitendo.
Jiulize Maswali.
Pata muda kwa ajili yako. Jiulize maswali Makubwa na madogo…Jitathimini kama unampenda Mungu, Jifunze kuhusu wewe. Meditate.Andika vitu ambavyo unataka kuvifanya. Usifikirie pesa. bali kitu cha kwanza kabisa cha kufikiria ni MUDA.
Muombe Mungu akupe Imani. Tuliza akili yako na uone kabisa kazi unazotaka kuzifanya.
Jitolee Kwa Mtu .
Kama kuna kazi unayoipenda, jitolee kufanya bure.Kwa sababu mahali hapo utaanza kupata uzoefu. Ndoto yako haitaweza kutimia kama hutaweza kwenda kufanya kazi ya aibu kwanza. Kazi ya kuchafua mikono yako. Unaweza usielewe, lakini ndio kazi zinazofungua milango mikubwa.
Fungua Mlango.
Nafasi huenda inabisha hodi lakini kama hutafungua mlango, utawezaje kuifurahia hio kazi? Chukua nafsi kabla ya kuanza kupata malipo. wakati mwingine inaweza kuwa sio wakati sahihi. Lakini haina shida. wewe fungua mlango wa nafasi yako kwa kutumia mlango wa mtu mwingine ulio wazi tayari.
Kitu cha muhimu cha kufanya unapokuwa unajijenga katika maisha yako ni kwamba hakuna kitendo pasipokuwa na kitendo katikati yake. Ni lazima kufanya maamuzi na kuanza kujaribu vitu. Hata kama hupendi kufanya kitu hicho, lakini mwisho wa siku, hutajilaumu kwa sababu ya kujaribu na kushindwa. Lakini utakuja kujilaumu kwa kutojaribu kabisa.
Funika hio laptop yako , Nenda ukapate maisha yako.
Subscribe kupata makala mpya.