Screen-Shot-2016-03-01-at-7.16.17-PM Kama KWELI Unampenda, Utamuuliza Maswali Haya Kila Siku

Unauliza maswali haya?

Tunapotaka kuwa na mahusiano mazuri na mwenza tunayempenda, Wote huwa tunajaribu kuwasiliana vizuri . Tunafahamu kuwa Mawasiliano mazuri  ni muhimu katika kuleta furaha , ndoa yenye msimamo. Pia tunaelewa  kwamba tukiwa  watu positive  tunapunguza magomvi  ndani ya ndoa.

Lakini  katika kuwasiliana vizuri kuna njia mbili zinazofanya kazi .

Kwa hio  ni mara ngapi kwa kawaida  wanandoa wanaweza kutumia muda pamoja  kwa kuongea  mambo ya kawaida kila siku?  kwa inavyojulikana siku hizi ni ndoa chache sana zenye muda wa kuongea pamoja kwa muda wa kutosha kwa njia ya maana .

Na kipi kinachofanya mawasiliano yawe na maana ?  Ni  muungano  ulio imara wa wenza  wa muda mrefu  na wenye kiwango cha  juu katika upendo wao, sio watu wa kudanganyana.

Na hapa kuna maswali 10 ya nguvu  ya kumuuliza mwenza wako  ili kupata msaada wa ndani  utakaowawezesha kupendana.

1.U hali gani leo?/ morning beatiful/ handsome

Sio. Vipi wewe mzima…Lakini ukweli ni u hali gani leo?  Unapomuuliza swali hili mtazame mwenza wako machoni.  Kama unafikiria kuwa kuna kitu kinaendelea ambacho anataka kukiongelea, Mshike mikono yake au  mabegani unapouliza swali lako, au  mshike usoni mwake taratibu na  umwambie , Nataka kufahamu  unajisikiaje.

2.Kuna chochote naweza kufanya ili nikusaidie? 

Unaweza kuona mwenza wako alivyo bize, mwenye haraka, na  anaonekana  kama kuchanganyikiwa  kutaka kukamilisha  anachokifanya. Uliza swali hili na uwe tayari kuchukua hatua kwa chochote atakachokuomba kufanya.

Kama unaona anasitasita, mshike begani na mwambie nahitaji kukusaidia hiki. nifanyeje?

3.Kitu gani cha muhimu kwako?

images-8 Kama KWELI Unampenda, Utamuuliza Maswali Haya Kila Siku

(Kiss me and never, never, never let me go)

Unapoona mwenza wako anajaribu kufanya maamuzi ya muhimu , muulize swali hili.

Njia nyingine ya kumuuliza ni hii  Unataka nini hasa? Kuelewa mawazo ya mwenza wako na hitaji lake , ni muhimu kufahamu moyo wake  unahisi nini katika swali hilo. kumuuliza  inamleta ukaribu kuanza kuongea  kitu anachokithamini zaidi.

4.Ungependa kufanya kitu gani?

Swali hili unauliza wakati ambao mko huru, mnapojaribu kupango kutoka, kusafiri, au kuzungumzia malengo  na mwongozo katika maisha yenu.

Njia nyingine ya kuuliza haya , kama ungetaka kufanya kitu chochote unachokitaka ungefanya nini?  Unafahamu malengo na ndoto za mwenza wako, kwa hio fanya naye ili kuona  kitu anachokitaka, shauku,  na  hamu yake aliyonayo.

5.Nitawezaje kukushawishi?  ( kama unataka kusikia kwa nini nakupenda , naweza kuongea usiku wote)

86a19647aa7665dacff170f607b28046 Kama KWELI Unampenda, Utamuuliza Maswali Haya Kila Siku

 

Swali hili utauliza wakati unapoona mwenza wako anapitia wakati mgumu au kuchanganyikiwa.  Huwenda ni changamoto anayopitia mwenza wako,  au ni majaribu ya maisha  ambayo mnapitia pamoja.

Tafuta njia ya kutuliza   ili uweze kumsaidia  muda huo, Na fanya hivyo kwa kadri uwezavyo.

6.Malengo gani unataka kuyapanga kwa ajili yetu na kwa ajili yako?

Swali hili unaweza kuuliza kila baada ya muda fulani , sio kila siku.

Fikiria kuhusu  maeneo mengi mnapoongea kuhusu hili ikihusisha, kazi, familia, mali au umiliki, urafiki, ndoa yenu, maendeleo ya kipekee na Elimu. Na usisahau  kuongea kuhusu kukua kwa akili na kukua kiroho. Mwili unakua kawaida.

7.Unafurahia mahusiano yetu yanavyoendelea?

Swali hili nalo hutaweza kuuliza kila siku, Lakini ni swali muhimu sana ambalo kila wenza wanatakiwa kuliongelea kila mara.

Tazama mambo yanaendaje kati yenu  baada ya miezi kadhaa. Na mmeenda mafunzo gani muda huo kwa ajili ya kuboresha  afya ya mahusiano yenu na kukamilika kwenu.

8.Woga wako mkubwa ni upi?

Sio swali la mara kwa mara. Ila ni muhimu kufahamu jibu lake.

Ulimwengu tunaoishi umebadilika kupita kiasi , Kuna hatari kila mahali.  Huenda mwenza wako ataweza kupenda kuongelea kuhusu jambo fulani linalompa hofu. Ingawa hutaweza  kuona umuhimu wa kitu chenyewe.

Huenda ni kuhusu mradi wa kazini , mazungumzo ya wanafamilia,  au maisha ya ndani mwenu,  fahamu kinachomwogopesha mwenza wako ili umsadie aone urahisi aishi vizuri.

9.Kitu gani kinakufanya uwe mwenye furaha? 

healthy-relationship-1024x682 Kama KWELI Unampenda, Utamuuliza Maswali Haya Kila Siku

(Kwa sababu niko na wewe, kila kitu ninachokitaka ninacho)

Maisha hayawezi kuwa mazuri kila siku. ukweli. Tunatumia muda mwingi katika kazi, iwe kazini au nyumbani,  hakikisha kuwa mnapata siku ya mapumziko  pamoja.

Tazameni mambo ambayo yanawapa furaha. Kitu ambacho kitawabadilisha kulingana na hatua mliopo katika maisha yenu. kwa hio usishangae  wakati  kitu fulani kipya  kitajitokeza kati yenu.

10.Kitu gani unachokitaka nje ya maisha yetu ya pamoja?

Swali hili linahusu  muda mfupi na muda mrefu wa malengo,  shauku na vifaa.

Chukua muda wa kufahamu  ni watu gani wako karibu naye , na umpe  usikivu  anaostahili. Nguvu yako na wazo lako liwe la kumpa msukumo wa kukamilisha  malengo yake, shauku yake, katika vitu vyote.Onyesha kujali  na mfanye aweke kipaumbele  katika hayo malengo.

Kama umeipenda  makala hii. like , share, na kisha  Subscribe.

Toa comments zako hapa chini kusaidia wengine.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here