”Kama” Ni Neno Ambalo Limetumiwa Upande Wa Mwanadamu Sio Wa Mungu


SAM_6595-1024x815 ''Kama'' Ni Neno Ambalo Limetumiwa Upande Wa Mwanadamu Sio Wa Mungu

Neno hili kama Linavutia.Ni moja ya neno Lililoongelewa sana Kwenye Biblia moja kwa moja kwenye majukumu yetu na lina masharti.

Yesu alitumia neno hili mara nyingi kwenye Agano  Jipya kwenye vitabu vya injili. Mara nyingi alitumia neno kama kwa mwanadamu sio kwa Mungu.

Kama Na Sikia.

Ikiwa una ufahamu , sikia neno hili. Isikie sauti ya maneno yangu. Ayubu 34:16

Kwa maana ndiye Mungu wetu. Na sisi tu watu wa malisho yake, na kondoo za malisho yake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake.

Mtu akiwa na masikio ya kusikia na asikie.

Leo kama mtaisikia sauti yake, msiifanye migumu mioyo yenu.Kama wakati wa kukasirishwa  Waebrania 3:15

Kama Na Kusikiliza

Angalieni nawawekea mbele yenu Hivi leo , Baraka Na Laana. Baraka ni hapo mtakapoyasikiliza maagizo ya bwana, Mungu wenu, Niwaagizayo leo. Na Laani na hapo msiposikiliza  maagizo ya bwana Mungu wenu.Mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu msiyoijua.

Kama mkimcha Bwana na kumtumikia  na kuisikiliza sauti yake , msiiasi amri ya Bawana , Mkona wa bwana utakuwa juu yenu.

Kama ndugu yako akikukosea, Nenda ukamuonye, Wewe na yeye peke yenu. Akikusikia umempata nduguyo. La Kama hasikii, chukua pamoja nawe mtu mmoja au wawili ,  Ili kwa vinywa vya mashaidi hao  kila neno lithibitike. Na asipowasikia hao liambie kanisa,  Na asiposikiliza kanisa tena, na awe kwako kama  mtu wa mataifa na mtoza ushuru.

Kama Na Kutii

Sasa basi Ikiwa mtatii sauti yangu kweli kweli,na kulishika agano langu, Hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko mataifa yote, maana Dunia yote ni ya kwangu.  Kutoka 19:5

Kama mkikubali na Kutii mtakula mema ya nchi.

Kama mngekuwa na Imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia Mkuyu huu ng’oka ukapandwe baharini.Nao ungewatii. luka 17:6

Kama tu mtasikia sauti yake  na kutenda yale aliyowaagiza…

Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno la waraka huu , jihadharini na mtu huyo na wala msizungumze naye, ili apate kutahayari, lakini msimuhesabie kama adui, bali muonyeni kama ndugu.

Tazama nasimama mlangoni nabisha, mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye. Naye pamoja nami. Ufunuo wa Yoh. 3:20

Kama Na Moyo.

Lakini huko kama mkimtafuta bwana  Mungu wako utampata. Ukimtafuta kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.

Kama ningaliyawaza maovu moyoni mwangu, Mungu asingesikia. Zaburi 66:18

Ndivyo na baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi , msiposamehe  kwa mioyo yenu kila mtu na ndugu yake.

Tena tusichoke katika kutenda mema , maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

Mtu akidhani ya kuwa anayo dini , wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake,Dini yake mtu huyo haifai.

Dini iliyo safi isiyo na taka mbele za Mungu ni hii, kwenda kuwatazama Yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na Dunia pasipo na mawaa.

Wapenzi , Kama mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu.

Kama Na Imani.

Akawaambia, Ni kwa sababu ya upungufu wa Imani yenu. Amini nawaambia ,Kama mngekuwa na Imani kiasi cha punje ya haradali mngeuambia mlima huu ondoka hapa uende kule ungewatii, wala kusingekuwepo neno lisilowezekana  kwenu.

Tena nijapokuwa na unabii  na kujua siri zote na maarifa  yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, Kama sina upendo  si kitu mimi.

Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika Imani. Jithibitisheni wenyewe, au hamjijui wenyewe kwamba Yesu yupo ndani yenu?

Mwanangu kama ukiyakubali maneno yangu na kuyaweka akiba  maagizo yangu. Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukauelekeza moyo wako kupata upate ufahamu.Naamu ukiita busara  na kupaza sauti yako upate ufahamu, ukitafuta kama fedha., na kutafuta kama hazina iliyositirika. Ndipo utakapofahamu kumcha bwana. Mithali 2:1,2,3,4,5

Mara zote Kama ipo upande wa mwanadamu. na sio  upande wa Mungu. Kama mwanadamu atafanya, Mungu atafanya.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

 

Previous Nini Kusudi La Mungu Katika Ndoa Na Familia
Next Fundisha Akili Yako Maarifa Na Ukue Kwa Furaha

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.