shutterstock Kama Unataka Kuona Upendo Wa Kweli

Anasema ,

”Nakupenda”

”Nakupenda zaidi” Unajibu.

Nakupenda zaidi ya zaidi. Anasisitiza.

Wewe ni mrembo. you are amazing. ni mtu sahihi kwa ajili yangu. ni ndoto yangu.  ni kitu ambacho kamwe hakijawahi kutokea maishani mwangu. Sitakuacha. Haijalishi kutatokea nini. Anasema hivyo…

Maneno mazuri kama hayo.

Yana ladha ya vanila.

Matamu kuliko asali.

Yanawaka kuliko mwanga wa jua.

Kitu gani kingeweza kuwa kizuri zaidi?

Maneno.

Maneno yote.

Anasema anakupenda.

Lakini hata hakuangalii machoni.

Kama anayvoangalia kitu kizuri kama nyota.

Anasema anakupenda.

Lakini Hakuambii alikuwa wapi  usiku.

Anasema anakupenda.

Lakini hawaambii hata marafiki zake kuhusu wewe.

Anasema anakupenda.

Lakini hata hakusaidii kufikia ndoto yako.

Anasema anakupenda .

Lakini hata hataki kusikiliza kitu chochote unachokisema hata kama ni cha ujinga.

Anasema anakupenda.

Lakini wakati mambo yakienda vibaya  hawezi kutafuta njia ya kutatua.

couple Kama Unataka Kuona Upendo Wa Kweli

Mpenzi, nisikilize  mimi.

Baadhi ya wanaume ni wazuri kwa maneno.

Baadhi ya wanaume ni wazuri tu kwa maneno.

Uwe mwerevu.

Unatakiwa kuwa na tahadhari.

Linda moyo wako.

Usimpe moyo wako mtu ambaye sio sahihi.

Unastahili kilicho bora.

 

Unastahili upendo ambao ni pure.

Upendo ambao ni wa upole.

Upendo ambao hauhesabu.

Upendo wa uhakika.

Upendo unaoweza kuhamisha milima.

Upendo unaoweza kukatiza katikati ya bahari.

 

Upendo ni uvumilivu.

upendo ni wema, sio wa Wivu.

Sio wa  kiburi.

Sio wa kujivuna.

Sio wa kudharau wengine.

Haujitafutii makubwa.

Hauna hasira.

Hauhesabu mabaya wala kutunza mabaya.

Haufurahii udhalimu.

Bali hufurahia pamoja na kweli.

Huvumilia yote.

Hutumaini yote.

Wakati wote hushinda.

(1 wakoritho 13:4-7)

 

Upendo haupimwi kwa maneno.

Bali kwa ukweli na matendo.

Kama anakupenda tu kwa ulimi,

Na kwa macho,

Sio kwa moyo,

Na Roho,

Huo sio upendo hata kidogo.

Upendo ni kitu unachokisikia ndani .

Ni kitu kinachozama  mahali fulani ndani.

Unaweka mizizi

Unaonekana kwenye tabasamu.

Na unaweza kuonekana ndani ya macho ya mtu.

Na unakamilishwa na matendo.

Unataka upendo wa kweli?

Fungua Biblia.

Upendo wa kweli ni ule Wa Mungu kumtoa mwanae wa pekee kutuokoa.

Upendo wa kweli ni jinsi Yesu alivyotoa maisha yake kwa ajili yako.

Upendo wa kweli ni wa Yesu kufa msalabani kwa ajili yako.

Upendo wa kweli ni jinsi Mungu anavyokubariki kila siku

Kuanzia wakati unapoamka asubuhi.

Mpaka wakati wa kwenda kulala tena usiku.

Upendo wa kweli ni jinsi anavyokusikiliza.

Haijalishi uko katika hali gani.

Upendo wa Kweli ni jinsi anavyokusamehe wewe.

Haijalishi umefanya dhambi gani.

Upendo wa kweli ni jinsi anavyokuzunguka na kukupa kampani unapokuwa mwenyewe.

Upendo wa kweli ni jinsi alivyokuvusha kutoka katika hali ngumu na kukufanya jasiri.

Upendo wa kweli ni jinsi anavyokufahamu.

Kila kitu ulicho nacho.

Jinsi mbingu ilivyo ya kupendeza.

Kukuona wewe ukiwa unatabasamu.

Kukupatia mvua.

Kukuondolea huzuni na upweke wako.

Upendo wa kweli ni pale unapomuita na kukuitikia.

Anakuwepo pamoja na wewe. yuko kwa ajili yako.

Kila sekunde, kila dakika, kila siku.

Upendo wa kweli ni jinsi alivyokuumba.

Uzuri wako.

Usahihi ulio nao.

Kutokana na mfano wake.

Upendo wa kweli ni Mungu.

Yeye asiependa hamjui Mungu.

Kwa maana Mungu ni pendo.

Na Pendo Ni Mungu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here