Kanuni Za Maombi Yanayojibiwa


does-god-answer-prayers-today Kanuni Za Maombi Yanayojibiwa

Watu wanafundishwa kusali. Ni kweli , ni kweli kabisa.

Zipo kanuni nyingi, kuna kanuni za kiaskari, Zipo kanuni za ufalme wa Mungu.

Maombi ni ushirika kati ya mwanadamu na Mungu.  Mungu amesema Niite nami nitakuitikia, Nitakuonyesha mambo makubwa , magumu usioyajua. Ni kuuliza na kujibiwa.Ni kueleza hitaji lako. Unataka nini? Kuwa wazi. Unashikilia kuwa umejibiwa. Kuona jibu katika Ulimwengu wa Roho kabla hujaona likiwa halisi mkononi.

Ikiwa bado hujajibiwa , jitathimini upya. Huenda huombi bali unalalamika. Mungu anapenda shukurani sio malalamiko. maombi sio njia ya kumsukuma Mungu  kufanya jambo unalolitaka wewe. Mungu ana utaratibu.

Mungu anatazama moyo wako, anatazama Imani yako kwake, Anatazama kujitolea kwako kutumika katika ufalme wake. Anatazama unatumiaje Muda aliokupa.

Kwa kuwa hatukupokea roho ya utumwa bali ya wana. fahamu kuwa Mungu anakujali, Anakupa usalama.Anakupenda. anakupa afya na tiba. anakupa amani , maisha.

Omba kwa imani bila ya kujali mazingira uliyonayo. Omba Toba unapokuwa unaona hauko vizuri kiroho. Chochote ambacho unakosa nacho amani mwambie Mungu. Ipo dhambi ya kutokusamehe, jitahidi usamehe na ujisamehe mwenyewe. dhambi ya kufanya masturbation. omba toba.

Tembea ndani ya tunda la roho. Upendo, Furaha, Amani, Uaminifu, Utu wema. Uvumilivu usio na mateso, Kiasi.

Maombi ambayo yatajibiwa haraka ni kufanya kazi ya Adamu, Na kazi ya Yesu. 

Kazi ya adamu ni kusafisha mazingira. Tafuta sehemu kila mara au kila siku safisha sehemu hio mpaka igeuke kazi yako.Ni ngumu kidogo kuelewa , lakini ukweli ndio huo. Umeumbwa kwa  udongo, wewe ni mfano wa Mungu. Kwa hio unaposafisha ardhi, unasafisha mwili wa Mungu.

Kazi ya Yesu ni kwenda kuwaona wafungwa, kwenda kwa Yatima na wajane, Kuwaona wazee wasiojiweza. Hata kama huna pesa. Muda wako unatosha  Kutumika katika nyumba ya Mungu. Dini ilio safi  isio na taka ni hii. Kazi ya Yesu ni kumfundisha mtu Upendo. Kuipenda nafsi yake, kumpenda jirani yake na Kumpenda Mungu. kuwapenda watu.

Majibu ya Haraka katika maombi yako ni kufanya kazi za aina hizo mbili  hapo juu. hizo ndio madhabahu safi na ni namba moja.

Ukiona huna kazi tambua kuwa huna nguvu, ukiona unaumwa, tambua kuwa nguvu ya Mungu haipo ndani yako. Ukiona mahusiano yako mabaya , tambua kuwa huna nguvu ya Mungu. Ukiona huna furaha, amani, utulivu, huna nguvu ya Mungu.

Kupata nguvu ya Mungu, toa muda wako , nenda kasaidie kufanya kazi katika nyumba za yatima, wajane na wazee wasiojiweza. Utarudisha nguvu zako. Nenda kamfundishe mtu habari ya Kumpenda Mungu. habari ya kuipenda nafsi yake . Habari ya Kristo.

Vitu Vitakavyokusaidia Kupata majibu kirahisi wakati ukiwa katika vitendo.

1.Uwe na ushirika mzuri na Mungu

2.Utulivu wa Roho yako

3.Enenda kwa Upendo

4.Uhuru wa roho.

5.Ujasiri na Mungu ya kwamba ni baba. ukimwomba mkate atakupa mkate na sio jiwe. samaki sio nyoka. Yai na wala sio nge.

6. Furaha ya moyo.

7.Utii.

8.moyo ulio wazi na umakini wa kiroho.

Vitu Ambavyo Vinazuia Maombi Yako …

Hofu,Mashaka, Dhambi, Kiburi, Wasiwasi, Mila na Tamaduni,Na Uvivu.

Anza leo kufanya mabadiliko ya maombi yako ya kulia na kulalamika, badala yake  nenda kafanye kazi ya Adamu na kazi ya Yesu. Ambatanisha na vitu ambavyo vitakusaidia kuwahi zaidi. Pia achana na mambo ambayo yanaleta vizuizi. Haraka utapata majibu yako.

Kila unapofanya kazi ya Adamu au ya Yesu, huko huko mwambie Mungu maombi yako. Ukirudi mwambie Mungu asante kwa majibu mazuri.

Mungu Akubariki, akupe nguvu, akuongeze Imani.

Subscribe kupata mafunzo mapya kila mara.

 

Previous Jaribu La Muda Kwa Mwanadamu
Next Kitu Gani Kinatesa Watu Wengi Leo?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.