EmL0cnp-1024x683 Kiasi Gani Cha Sukari Kinafaa Kula Kila Siku?

Najua sukari ina utata, Kuna maswali mengi kuhusu vitu vitamu. Hapa kuna baadhi ya maswali  ambayo yanakuumiza kichwa .

Sukari ya kwenye matunda ni sawa? Nimesikia sehemu kuwa  ni nzuri, lakini nikasikia sehemu nyingine tena kuwa nikae mbali nayo , Nimepatwa na utata mkubwa. Na sasa sitaki kula ndizi.

Kuna  Baadhi ya matunda yenye sukari  kwenye mlo wa afya, lakini sukari ya matunda bado ni sukari. Sukari ikizidi huhifadhiwa kama mafuta. Nashauri kama una uzito mkubwa  tumia matunda ambayo hayana sukari nyingi  tena tumia kidogo.

Matunda ambayo hayana sukari nyingi ni kama Strawbberrie, raspberries, na blackberries , pears na apples.

Ndizi ni tundfa lenye kiasi cha juu cha sukari lakini lina  kiasi kikubwa cha fibers. kwa hio usijisikie vibaya kutumia mara moja moja.

Kula Kipande cha chocolate  kwa siku inaharibu afya yangu?  Nimekuwa nikiepuka sukari lakini  nakula kipande cha chocolate kila siku. Ni kweli ni mbaya ?

4332aec5ada4f28b8fec1fabb7ffac7e Kiasi Gani Cha Sukari Kinafaa Kula Kila Siku?

Chocolate , hasa ile yenye rangi nyeusi  ina lishe nzuri.  Chocolate ni chanzo kizuri cha madini  ya magnesium na chuma. Chocolate inapunguza  hatari  ya magonjwa  ya moyo, kupunguza stress, na kukuweka katika hali nzuri.

Lakini unaweza kujaribu kutotumia kila siku,  Anza kupita siku bila ya matunda au chocolate au kitu chochote kitamu , Halafu sikiliza mwili wako  unajisikiaje. Huenda sio lazima kutumia kila siku.

Sukari ipi ni bora kutumia ambayo ni ya Natural?

Hapa Kuna baadhi ya aina  bora.

Coconut Sugar.  Sukari ya nazi ina madini ya antioxidants ambayo huwezi kuyapata kwenye sukari nyeupe.

Coconut-sugar-The-latest-sugar-alternative_strict_xxl Kiasi Gani Cha Sukari Kinafaa Kula Kila Siku?

Raw honey. Asali ghafi, ni asali ambayo haijachanganywa na vitu vingine. pata kutoka shamba moja kwa moja. Asali za kawaida. Lakini asali hii hairuhusiwi kutumia  watoto wadogo, wanawake wenye mimba au wale vegans.

5_Health_Benefits_of_Raw_Honey_Featured_Pic-1024x576 Kiasi Gani Cha Sukari Kinafaa Kula Kila Siku?
Bee products, wax, honeycombs, pollen

Lakini pia sio lazima kutumia kila siku. Ingawa  sukari ya nazi  ina fructose ya kiasi cha chini , asali ina asilimia 4o . Sukari ya mezani ina asilimia 50 ya fructose. Kwa hio kuwa makini katika kila matumizi ya sukari.

Nimepata Utata kuhusu Yogurt. Wengine wanasema  ni nzuri , lakini wengine wanasema sio nzuri. Lakini zote zinaonekana kuwa na sukari ya juu. Watu wanasema tule yogurt kwa sababu ina afya.  Nikienda kunua vitu natumia muda mwingi kusoma  lables, mara nyingi natoka bila ya  kununua chochote.

greek-yogurt-fatty-foods-make-you-skinny Kiasi Gani Cha Sukari Kinafaa Kula Kila Siku?

Ni vizuri kuchukua muda wa kusoma lables.  napendekeza  kutumia low-or full-fat yogurt kwa sababu hazina sukari nyingi. Yogurt ni chanzo kizuri cha protein ingawa hatuhitaji  protein nyingi kupitia hizi yogurt. Hakikisha yogurt hio inatokana na   ng’ombe wa kienyeji  sio wengine, au inayotokana na matunda yasio na sukari nyingi.

Nitajuaje kuwa Aina hii ya sukari ni nzuri kwangu? Kwa sababu tunasikia sana kuhusu kutumia matunda mengi ni vibaya– Tunatakiwa kutumia hadi kiasi gani ?

Tunaweza kuwa na ufahamu  na hata kula vyakula vizuri , Lakini kama tunasikia ndani yetu wasiwasi, kujilaumu, au  kutumia muda mwingi kuhangaikia lishe nzuri katika vyakula vyetu, Hapo kuna umuhimu wa kufanyia kazi . Chakula cha shida bado ni shida,  na sio nzuri kwa ajili ya afya yako au uzito wako.

Tutazame ulaji wetu kwa ujumla ukoje.  tutazame nafsi zetu ,wasiwasi wetu , kujilaumu kwetu. Tunajisikiaje tunapokula. Kama moyo wako unasita kula kitu fulani usile. Na kama una uwezo  jaribu kusikiliza mwili wako unahitaji nini.

Ni ushari wangu kama utaamua mara moja kwa wiki kutumia kitu kitamu , kuliko kutotumia kabisa . lakini tumia kiasi. na iwe ni utaratibu wako.  Halafu rudi kwenye utaratibu wa tabia yako ya kutotumia vitamu.

Unaweza ukaona kama haiwezekani, lakini tunza list ya ushindi wako. Kila siku. Chagua kilicho bora.

Share kwa wingi.

Subscribe kupata makala mpya.

Kisha toa maoni yako kusaidia wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here