TNMCoupleSmileHappyTeethFeature-589x260 Kila Mahusiano Yaliofanikiwa Ni Kutokana Na Wawili Kuwa Na Lengo Moja

Mahusiano ni sawa na kioo ,Mpasuko mdogo unaweza kuvunja kioo chote. Inahitaji umakini wa hali ya kipekee. Mahusiano yalio sahihi  sio rahisi kudumu  katika mafanikio.

Utahitaji kujikita  na kujitolea kwa ajili ya hilo. Vitu vidogo ambavyo vinaleta kutokuelewana , ambavyo huwezi kushughulikia kwa urahisi  vinaweza kuharibu mahusiano yako. Lakini wakati wowote inawezekana kuponya mahusiano yako, hata kama yalikuwa yanaelekea kuvunjika kabisa. kama hufanyi kitu , hakuna muujiza wowote ambao utakutokea ili uwe na mahusiano mazuri.

Wengi wetu tunajitahidi kila siku, iwe nyumbani , kazini , au katika masaa ya kati ukiwa popote . Mahusiano ni kipengele ambacho cha muhimu  katika kila maisha ya mwanadamu. Jinsi gani utaweza kudumu katika mahusiano mazuri , ni katika majadiliano ya watu wawili.

Tabia Za watu Waliofanikiwa Katika  Mahusiano 

1.Wako pamoja kwa sababu sahihi

2.Wana matarajio ya kweli kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi

3.Kitu cha muhimu kwao sio mawasiliano bali ni Heshima kwa kila mmoja

4.Wako wazi, huongea kila kitu wazi , hasa yale mambo yanayowaumiza.

5.Mahusiano yenye afya yana husisha watu wawili wenye afya.

6.Hupeana nafasi

7.Wewe na mwenza wako mnakua  na kubadilika kwa njia zisizotarajiwa. kumbatia hilo

8.Mnapita katika mazuri na mapigano.

9.Mnapita katika mazuri na magumu lakini mnasameheana.

10.Vitu vidogo vinaongeza vitu vikubwa.

11. Sex matters…a lot.

12.Hutengeneza kanuni za kwao za mahusiano

13.Hujifunza kuyapiga mawimbi .

Safisha Au ondoa Maji Yaliomo.

Mahusiano yanakuwa na maji pale mtu mmoja anapokuwa hawezi kuelewa au kukataa  kukua, kutokana na kile walichojifunza,uzoefu au hisia zao. Mahusiano yalio na maji ni rahisi kuvunjika . Kunakuwa na uelewa mdogo, hakuna heshima, hawafurahii wenza wao, hata zile sifa za mwanzo zilizowafanya kuwa pamoja wanapoteza. Ukitazama kwa akili hawa watu  wamebadilisha chujio lao la akili. Wanachukulia tofauti mitazamo , tabia na hisia za wenza wao. wanawafikiria tofauti kwa kila kitu.

2-a-total-ban-on-mind-reading-1024x768 Kila Mahusiano Yaliofanikiwa Ni Kutokana Na Wawili Kuwa Na Lengo Moja

Ili kuondoa maji yalioingia ndani ya mahusiano ,Itabidi wote wakubali mabadiliko na kukua  kwa wenza wao, bila kujali mazingira.Kila mtu ajitahidi kwa upande wake.

Kumbuka kama mahusiano yako yameingia kwenye tatizo, haikutokea siku moja, unaweza kurekebisha, lakini itahitaji nguvu ya ziada, uvumilivu mkubwa na upendo wa kutosha ili kuponya mahusiano yako. Pamoja na kwamba , huenda kuna mmoja wenu amekata tamaa au hajakata tamaa, utahitaji ushauri wenye nguvu ili kurudi hali ya kawaida. Kwa sababu Upendo wa kweli unahitaji  kupiganiwa.

7152071 Kila Mahusiano Yaliofanikiwa Ni Kutokana Na Wawili Kuwa Na Lengo Moja

Fanyia kazi vitu ambavyo unaona vinakusaidia kukuza mahusiano yako. Hasa katika vipengele vya Kiakili, kiroho, kimwili, kiuchumi. hivi ni vitu vya kuongea na mwenza wako wazi wazi . Usiogope kumweleza mwenza wako kitu ambacho hakileti furaha .Weka kipaumbele kwa kila mmoja wenu. Heshima ni kitu cha kwanza. Mshikilie mahusiano kwa pamoja, sio kumwachia mtu mmoja. Kujijali na kumjali mwenza wako. Kuaminiaina.Kuwa wazi. Ondoa mashaka.Kubali tofauti zenu. Mpende mwenza wako jinsi alivyo.

Subscribe kupata makala mpya kila mara

2 COMMENTS

  1. I see you don’t monetize your page, don’t waste your traffic, you
    can earn extra bucks every month because you’ve got high quality content.
    If you want to know how to make extra bucks, search for:
    Boorfe’s tips best adsense alternative

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here