1493235317_love1 Kitu Gani Kinatesa Watu Wengi Leo?

Umezaliwa ukiwa fresh ndani ya ubongo wako, kila kitu unahitaji kuingiziwa na watu waliokuzunguka. Mazingira uliopo. Kila hatua unayopitia  inahitaji kupata mafunzo.

Lakini Ujinga umefunika nafsi kubwa ya mtu, hata asijue  nini cha kufanya , matokeo yake anateseka. Kutafuta Pesa kunatesa watu wengi kwa sababu wanatafuta Pesa bila ya kumjua Mungu. Bila ya kupata maarifa kwanza.

Tuangalie Uwiano ulipo kati ya Namba na Maneno.

0= Upendo. Ukikosekana upendo ndani ya mtu, hataweza kufanikiwa katika kumpenda mwingine. hataweza kumpenda Mungu . Hata kama atafanya mambo makubwa kiasi gani , hatadumu na hayo mambo.Atateseka kila siku. upendo unabeba  kila kitu.

Ujapokuwa na mali nyingi  kiasi gani , Ukiwa na imani kubwa ya kuhamisha milima, ukawa ni mtu wa kuongea lugha  zote za wanadamu, kama huna Upendo ni kazi bure.

1=Muda . Hiki kitu , Muda ni kila kitu katika maisha yako. ukikosa upendo kama unao muda utatafuta upendo. lakini ukipoteza muda wako  hutaweza kuutafuta bali utakuwa umekufa. Muda ni kitu pekee ambacho mwanadamu amepewa na Mungu.

2=Taarifa. Ukitumia muda wako vizuri utatafuta taarifa mbalimbali, utafikiria, utatafuta wazo la kukutoa mahali ulipo.

3=Uelewa. Utakuwezesha kuishi vizuri na mke wako, mume wako, familia yako, wafanya kazi wenzako, na wengine. ujali nafsi yako, utawajali majirani, na kumcha Mungu.

4=Ufahamu.  moyo wako unahitaji kupata ufahamu, unatakiwa kutafuta  ufahamu kama hazina, kama  unavyotafuta pesa, ili ufahamu kumcha bwana.

5=Imani. Bila imani huwezi kufanikiwa, huwezi kumpendeza Mungu. Imani ni jicho la Mungu. Fanya kila kitu kwa imani, kwa sababu hakuna kitu Mungu alikifanya bila Imani.

6=Hekima.  Unapewa na Mungu. ukiwa na hekima utafahamu kusema asante.Utatoa maarifa kinywani mwako. Utakuwa mkamilifu. utafahamu haki na hukumu.

7=Watu. Ukiweza mambo yote kuanzia 0-6. Utakutana na watu. Hapa ndipo penye mafanikio yako, hapa ndipo pa kuanza kutokeza mwanga wako. Hapa ndio penye mavuno .Huwezi kufanikiwa kama huna Upendo, hutumii muda vizuri, Hutafuti taarifa, huelewi mahusiano yako,kazi yako. Huna ufahamu  na huna Hekima.

8=Pesa. Ukisha kutana na watu tayari una pesa. biashara ni watu, shughuli ni watu, kazi ni watu. Watu watakuletea pesa.

9=Vitu. Ukipata  pesa utanunua vitu unavyovitaka.

Kitu gani kinakutesa wewe? Huna Upendo. Ni ujinga wa kuanza kutafuta Pesa kabla ya kutafuta upendo, Kutumia muda vizuri, kutafuta maarifa, hekima, Huna Imani na Mungu. Huipendi nafsi yako, humpendi jirani yako, Huna ushirika mzuri na Mungu. 

Angalia Pesa ipo namba ngapi hapo. Umeruka sehemu kubwa mno. Rudi kule juu , Acha kuteseka kutafuta pesa ili ununue vitu. maisha sio biashara yako. Ni biashara ya Mungu mwenyewe. Ukiipenda nafsi yako, utampenda jirani yako, utampenda Mungu. Ukimpenda jirani hutaweza kuzini naye, hutaweza kumuibia kitu. hutamuua. Badala yake utamsamehe, utamuombea. Atanunua kitu kwako, utanunua kitu kwake. Utampenda mke /mume wako. utawapenda watoto, utawapenda watu.

Mungu ataachilia kwako baraka. Utajiri unaodumu. Utajiri usio na majuto. Amani, Furaha  na raha itaachiliwa kwako.

Subscribe ili kupata makala mpya .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here