Kitu Kimoja Ambacho Wanawake Huelewa Tofauti Kuhusu Wanaume


black-couple-50-percent-of-women-have-back-up-plan Kitu Kimoja Ambacho Wanawake Huelewa Tofauti Kuhusu Wanaume

Nataka nikushirikishe story moja  ambayo ni nzuri  na ina point kubwa.

Miaka mingi iliyopita nilikutana na kijana, nilifikiri kuwa ni sahihi kwangu, Japo nilimsikia kabla  hatujawa watu wenye akili ya kutosha, mara nikaona kuwa ni mwanaume maalum kwa ajili yangu.

Hatimaye tukawa marafiki wa karibu , na nilianza kufikiria picha kubwa ndani yangu kuwa atakuwa ni yeye. Niliona ni mtu sahihi kwa ajli yangu.

Sio hivyo tu , Hisia nazo zilinituma hivyo, maongezi yalikuwa mazuri,  Dalili za mwili, furaha ya nyuso zetu kila tunapokuwa pamoja zilishine. Mimi ni mshauri wa mambo ya mahusiano , ninapoongea kuhusu mwanaume najua  mwanaume anapopenda anaonekanaje, na hii ndio ilivyokuwa.

friends2504 Kitu Kimoja Ambacho Wanawake Huelewa Tofauti Kuhusu Wanaume

Baada ya hayo yote, hakuwahi kuuliza namba ya simu , wala kunigusa, lakini nilijua kuwa ananipenda. hicho kilinilewesha mimi.

Nilianza kufikiria , lakini sio kawaida, au kwa sababu sijaonyesha dalili yoyote ya  kumpenda, au  naogopa kukataliwa endapo nitaonyesha mazingira magumu niliyonayo kwake, au anasubiri anifahamu vizuri ili awe na uhakika na mimi, au ananipima kama nitakuwa mvumilivu. lakini nikaanza kuongea mwenyewe, nikikutana naye nitamuonyesha jinsi gani nampenda.

Baada ya miezi kama miwili, Nilimuona akiwa na wasichana wengine, lakini mimi nilijifahamu kuwa ni watofauti. Namaanisha.  Niko vizuri katika kusoma mazingira, hiki ndicho kinanisaidia katika maisha yangu, siwezi kukosea hapo.

Hatimaye alionyesha kitu cha tofauti mbele ya watu wote , kunikumbatia na kunishika mkono  , alionyesha tabasamu la tofauti  na macho ya tofauti kabisa na anavyofanya siku zote.  Kwa hio nikaanza kufikiria, hivi ndivyo anavyoonyesha kunipenda kuliko wengine?

Ndio. ilitokea hivyo, ilikuwa hivyo na nilijisikia hivyo lakini haikuwa hivyo.

Sasa nilichanganyikiwa. Sikuelewa kitu. Kwa nini asiwe na muda na mimi? Labda kwa sababu hataki mambo yajulikane haraka. lakini kwa nini?  Labda anataka kuwa na uhakika kabla hajafanya maamuzi ya kudumu. Au anaona kabisa kuwa mimi ndiye hasa ninayemtaka , hicho kitu kinamfanya awe na woga…Kwa hio anaendelea kutazama kitu gani kinaendelea.

Nilibaki kwa zaidi ya miezi kadhaa nikiwa nimechanganyikiwa , nitamwingiaje huyu mtu? Natafuta password lakini wapi. Nilijiuliza nitawezaje kuwa na mahusiano naye?  Yote hii ilikuwa ni kuchanganyikiwa.

Lakini kwa sababu ni mtu ambaye najua kujirudisha kwenye hali ya kawaida sikuweza kufikia pabaya. Niliweza  kutatua kila wazo ambalo lilikuja ndani yangu  hata wakati ambao nilijiona kama mjinga fulani hivi.

Nilijisikia tofauti.

Ok, ni story ndefu , kwa kifupi. Nilialika moja wa marafiki zangu k kwenye sherehe  na yeye pia alikuwepo. Alimtazama yule rafiki yangu na ndivyo ilivyokuwa. Alimuomba namba ya simu, wakaongea mengi, na haikupita muda akamuuomba wakatembee wote mahali. Nilijisikia vibaya kupita maelezo. Siku iliyofuata  sikuwa na nguvu hata kidogo, niliona giza.

Hii ndio hasa wanawake wengi  mara nyingi tunakosea kuhusu wanaume.

Tunafikiri kuwa wanachanganyikiwa. Tunafikiri kama haileti maana yoyote. Tunafikiri kuna mchezo wa kuchanganya ujumbe. Hatuelewi kwa nini?

Ukweli ni kwamba tuko hivyo. Tatizo liko hivi kwamba hatukubali ukweli .Hatutaki kufahamu kuwa hawezi kukupenda kama unavyofikiria wewe.Ingawa umempenda.

Kitu ambacho nataka ukifahamu ni kwamba , ukimpenda mwanaume, mpende na ujue kuwa unajifunza kupenda. Kama atakuja kwako itakuwa ni nafasi nzuri ya kuongeza upendo. Lakini kama hataweza kuja kwako Acha aende , Wewe utakuwa umejifunza kupenda.

Hata siku moja usiachie mawazo ya kumlazimisha mwanaume akupende, utateseka.  Penda nafsi yako kabla hujampenda mtu mwingine, utakuwa mwenye nguvu ndani ya moyo wako.

Hisia mara nyingi sio za kweli. Hapa kuna ukweli nakupa. Wanaume hawako complicated kama tunavyofikiria. Wanawake ndio tunawatatiza na ndio tunaleta ugumu.

Mimi siwalaumu wanawake , lakini  nasema kwamba huwa hatukubali  hisia za wanaume wanaposema na kuonyesha ukweli wao. Kumbuka kuwa wanaume ni viumbe  warahisi na wenye msimamo ulionyooka.

Wanaume hupenda kujionyesha jinsi walivyo, wanaweza wasije  kwa kusema maneno. Lakini mara zote unaweza kutambua kitu gani anahitaji kama uko makini. Kama akikuambia kuwa hataki kuingia kwenye mahusiano na wewe Amini.  Usianze kuleta mambo mengine  mwamini kabisa.

Jitahidi sana kusoma  mazingira kila mara unapokutana mna mwanaume ambaye unampenda, mwanaume sio mgumu , utamwelewa kwa urahisi.

Unaweza ukashangaa ninapokuambia kwamba , hakuweza kubaki na yule msichana kwa muda. Tulikuwa marafiki wa karibu na nilitambua kuwa tunaweza kuoana. Lakini ninavyokuambia alioa mtu mwingine na mimi niliolewa na mwingine na rafiki yangu pia aliolewa na mtu mwingine. Kwa hio kila kitu kilienda vizuri.

Subscribe. usisahau.

 

Previous Unahitaji Kitu Gani?
Next Siri Za Kudumisha Mahusiano Yako

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.