Kuelewa Hamu Ya Mwenza Wako Itakuongoza Kupata Sex Iliyo Bora


iStock_000023317931Small1 Kuelewa Hamu Ya Mwenza Wako Itakuongoza Kupata Sex Iliyo Bora

Mwanaume anataka sex muda wote. Mwanamke  yuko kwenye mood mbaya.Mwanaume anataka sex ili kujisikia kuwa karibu. Mwanamke anahitaji kupata hisia ya karibu kwanza kufikia hamu ya sex. Mwanaume anataka furaha ya mwili. Mwanamke anataka kujisikia kupendwa.

Kuna vitu vichache tu ambavyo vinatakiwa kuelezea jinsi gani mahusiano  yatafanikiwa.  Pamoja na kwamba statements hizo zitaonyesha ukweli kwa baadhi ya wanandoa, kila mtu anaweza kukubaliana na mimi kwamba ,  wanaume wanaweza kuchanganyikiwa endapo mwanamke atamkatalia kufanya naye sex.

Lakini je ni kweli tuko tofauti sana?

Huenda hatuko hivyo. Lakini wachunguzi wamegundua kuwa wanawake kwa wanaume  wana hamu  zinazolingana au kufanana kuliko wazo la kwanza nililoandika .Lakini tazama kwa undani zaidi  kama utaweza kuona jinsi gani kama utafamu hisia za mwenza wako  kwanza ili uweze kupata sex iliyo bora zaidi.

Ingawa inaonyesha kwamba hamu za wote zinalingana  zaidi kuliko utofauti uliopo , Zipo siri  ambazo zina athari mbaya kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi.

1.Wanaume Wanapenda Sex Zaidi Kuliko Wanawake

Ukiuliza watu wengi kwamba nani anapenda ngono zaidi kati ya mwanaume na mwanamke , atakujibu ni Mwanaume. Na hii imetokana na kujifunza kutokea tukiwa wadogo  na tumejifunza kutoka kwa walitutangulia kwamba wanaume wanapenda ngono kuliko wanawake.Tumejifunza kwamba wanaume ndio ambao wanatakiwa kuonyesha kuwa wana hamu na sio sisi wanawake.

Kusema kweli,Wengi wetu tunafikiri kwamba kama mwanamke ataonyesha hali ya kupenda ngono kuliko mwanaume hapo kutakuwa na tatizo. mwanamke huyo ataonekana malaya. Kumbe sio. Na hiki ndicho kinacholeta shida ndani ya mahusiano mengi.

Lakini kusema kweli , mwanamke anataka sex sawasawa kama mwanaume anavyokuwa anataka sex. vinginevyo kuwe na tatizo kwa mwanamke. Na kwa sababu ya kutumia madawa ya kuzuia mimba, naamini hili ni tatizo kubwa sana linalowafanya wanawake kupoteza hamu ya sex. Ukweli niujuao mimi , mwanamke anapenda sex kuliko mwanaume au wote tuko sawa, tunapenda.

2.Kujisikia Hamu Ni Kitu Muhimu Sana Kwa Mwanamke.

Hali ya kuhisi kwamba nahitajika, natakiwa ni kitu muhimu sana kwa mwanamke kupata hamu ya ngono, na hasa unaposikia neno hilo kutoka kwa mtu ambaye unampenda. Mwanaume anapochukua hatua ya kwanza kusema kitu kinachomfurahisha  mwanamke, hujisikia vema, hujiona kuwa na thamani ya kipekee kwa huyo mtu. lakini sio wanawake wote wanaofahamu  au kuona umuhimu huo  kwamba mwenza wa kiume anahitaji  kuonyesha kitu hicho muhimu kwake.

Ingawa katika uchunguzi wangu mwenyewe , kwa upande wa mwanaume nimeona kuwa wanafurahia pale wanapoona mwanamke ana hamu  ya kufanya sex . Lakini je vipi kuhusu wao , wanaume ,hamu yao inakuja kwa njia ipi hasa?  Wanaume wao hupatwa na hamu pale unapomsifia kwa kitu anachokifanya, mwonekano wake au tabia yake. hujisikia vizuri na hutamani kufanya sex na mwenza wake huyo. Hata nguvu yake inakuwa ni ya tofauti. kwa sababu anahisi kuwa amehitajika.

Wanaume pia wanapenda kuwa na hamu. Lakini wanawake wengi hawajui  jinsi gani mwanaume anapata hamu .Ni kitu muhimu  kabisa kwao.   Pongezi , shukurani.

3.Mwanamke kuguswa ni heshima, Mwanaume anataka sex.

Kitu cha tatu ni kikubwa, kuhusu jinsia . tofauti inakuja pale mwanaume anapotaka kuridhisha mwili wakati mwanamke anataka upendo na mapenzi. lakini  kitu cha kufahamu hapa ni kwamba kila mtu anahitaji urafiki wa kimapenzi ambao unaenda zaidi ya  sex.

Kitu cha muhimu na cha kwanza ni Mawasiliano. Kuwa na muda wa kutosha na mwenza wako. kutoka pamoja kutembea  mahali. Hii inaleta hamu kwa kila mmoja. ingawa kuna wanaume ambao hutaka sex kwanza ndio aweze kufanya mambo mengine. Lakini ni muhimu sana kuweka kipaumbele katika hamu ya kila mtu. Kuelewana.

Kwa nini Sasa hivi vitu  vinakuwa tofauti? Utafanyaje kuhusiana na hili? 

Ni kuondokana na dhana ya kuwa mwanaume ndiye wa kuanza kusema. Hasa naongelewa wale ambao wako kwenye mahusiano ya kweli. Mwanamke usiogope unapokuwa na hamu ya sex , mwambie mwenza wako atafurahi kusikia kuwa unamjali , atajisikia vizuri. Usiwe unawaza mabaya kuwa ukitangulia kumwambia utaonekana malaya au unapenda ngono, maadamu uko kwenye ndoa  usiwe na wazo hilo.  Unyesha hamu yako kwake.

Jitahidi kuonyesha ukweli wako, kuwa wewe, usiishi maisha yasio kuwa ya kwako kwa kuogopa  mafunzo yaliopitwa na wakati. Furahia  hali uliyonayo. uko sawa na wala usihofu kitu.  Mume wako anahitaji kukufahamu  ili aweze kushirikiana nawe vizuri katika maisha yenu ya sex.

Upande wa mwanaume kama wewe hamu yako ni ya chini kuliko mwanamke, kubali kwamba ni kawaida , ni hali tu ya kawaida , ni vizuri kupata ufahamu huu kwamba hata mwanamke anaweza kuwa na hamu kubwa ya sex kuliko wewe. Mwanamke nawe uelewe hilo , na wakati mwingine kujitahidi kuamshana kwa njia moja au nyingine ili kufurahia mahusiano.Mjitahidi kuelewana.

Subscribe Kupata makala mpya kila mara.

 

Previous Kwa Nini Ukiwa Kwenye Mahusiano Huna Uhakika Wa Kuwa Na Furaha
Next Date Na Mtu Ambaye Unamwamini Asilimia Mia

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.