shutterstock_208386529 Kufahamu Au Kutokufahamu Makubaliano Katika Mahusiano

Mahusiano yanapoharibika.

Kila mahusiano yana mikono miwili. Mmoja uko juu mwingine chini. Mkono wa kwanza unafahamu makubaliano kati ya wawili, unasema  , ”Tutasaidiana’, Kujali mahitaji ya kila mtu,  kusikilizana na kubebeana mizigi kila inapohitajika”.

Haya ni makubaliano muhimu. Ingawa yana kikomo, kwa kadri siku zinavyokwenda.  Kawaida inakuwa ngumu  kutunza  makubaliano  kwa sababu ya vipengele vinavyojitokeza  ambavyo havikuwepo ndani ya makubaliano.

Mkono wa pili ni ule usioongea, wa kutofahamu makubaliano kati ya watu wawili inasema,  Tutaenda kuachana na vipengele vyote vya mahitaji yetu  ili yasiwe tishio kwetu tunapokuwa pamoja katika maisha yetu, kuepuka migororo, na kila mtu awe vizuri. Hapo ndio tutafikia maono yetu ya mahusiano.  hii ya pili ina maana ya ubiafsi wao, utamaduni wao, mahitaji yao,  shauku  ili kuweka boti lao imara. Hivi vipengele  vinabaki kuwa kimvuli cha mahusiano yao.

slide_269757_1881834_free-1024x683 Kufahamu Au Kutokufahamu Makubaliano Katika Mahusiano

Vipengele hivi vinasababisha kila mtu, awe anataka au hataki  kuwepo au kusikiliza kitu ambacho hukitaki kwa mwenza wako. kufuata mambo yako mwenyewe, kama kusafiri, kuzunguka na marafiki au familia . Kutazama  michezo unayoipenda… hata kama mwenza wako hana interest na hayo . mambo haya  yanakuwa kama ya upande mmoja  hutaweza kujisikia vizuri.

Kwa mfano mwenza mmoja anaweza akawa ni mtu mzuri katika kuwasiliana, ni mtu wa kujali ni mwepesi kwa kila kitu kuliko  mwingine. Na mwingine huyo anaweza akawa ni mtu wa taratibu, mwoga,  mkimya. Mwenza wa kwanza anaweza  kuwa na nguvu ya  kumkaribia kwa upole na kwa urahisi zaidi.  Wa pili  atakuwa anatumia nguvu nyingi ili kufikia  mwingine. Hali hii haitaweza kudumu kwa muda mrefu.

Kwa mtindo huo  kama mtakuwepo pamoja mtasababisha matatizo . kama vile hasira, ndoto mbaya, hali kuwa sio nzuri kila mara,  stress, woga na usumbufu mwingine Katika point hii  swali  linakuja: Nitashughulikiaje tatizo hili?  nitapataje hali nzuri?  naweza kuachana na makubaliano haya na kurudi katika makubaliano ya kwanza?  Ok nimepata njia ya kufanya ili niweze  kutulia katika mahusiano haya katika maisha yangu yaliobaki.  Ninayo shauku, utayari, na ujasiri  wa kupigania safari hii  pamoja na mwenza wagu?

Ni makubalino yapi unayoyafahamu na usioyafahamu unayafanya katika mahusiano yako?

Njia za kawaida ambazo wanandoa wengu huchukua

Katika kukabiliana na changamoto za kutofahamu mahitaji, shauku na  mengine yanayojitokeza safarini, Hapo ndipo utakuta mwenza anaamua kurudi katika mkono wa kwanza  na kuanza kushughulikia mbinu  zinazosumbua kwenye mahusiano. Njia hii inaweza kumuweka mtu kwenye maumivu makali.  Wakati mwingine utakuta mtu anaamua kuwa mlevi, kutumia madawa ya kulevya, kuwa na huzuni,  au kuanza kutafuta nyumba ndogo.

Au atasema nitaenda kuweka nguvu yangu yote kwenye malengo, muda katika kutengeneza pesa ili kuepuka kurudi nyumbani mapema  kuwa na mwenza wake. au wanaweza kusema kama wanandoa  kuwa tunaenda katika mapumziko zaidi ili tujifanye kama kila kitu kipo vizuri  lakini sio kweli. hapo ni kuepuka matatizo kadhaa kwenye familia . hasa panapokuwepo watoto mnawawekea mazingira magumu ya kutokuelewana kwenu.

Mwisho mtajikuta container lenu halina nguvu tena , linafikia mwisho kwa sababu hakuna anayeweza kushikilia  maumivu kama haya.

Njia nyingine ambayo wanandoa wanaweza kuchukua ni kuamua kuanza upya. kuamua kujifunza na kutaka kukua kiakili, wanarudi katika mkono wa kwanza  ili kurudisha mahusiano katika hali nzuri.  Ina maana kila mwenza hapa ametambua kwa  nia nzuri  kuwa ni lazima waweke kipaumbele katika kutokujua kwao , kama mawasiliano mazuri,  ukweli, uwazi kwa mwenza. hii sio kitu rahisi  na sio njia rahisi ya kupita inahitaji msaada wa kutoka nje, kama mshauri wa mambo ya ndoa. Ili kubadilisha mwelekeo wa mahusiano.

Hapa hakuna kulaumiana,  hakuna kuhukumiana. wote wanakuwa wazi kujifunza  na kukua. Na ni katika kufanya maamuzi ya kweli kila mmoja.

Wakati Ambao Mwenza amekua na mwingine bado

Katika mahusiano ya kudumu hasa ya ndoa, unaweza kukuta mwenza mmoja amekua  kwa sababu ya kupenda kujifunza  katika kukua  na kuhusu mabadiliko kila wakati, na mwingine hana muda huo. Mara nyingi katika mahusiano utakuta mwanamke ndiye amekua kuliko mwanaume.  Bila shaka unaweza kukuta mwanamke mara nyingi anahudhuria mafunzo sio mwanaume. Kutokana na hali hio mwanamke anajifunza mambo mapya mara kwa mara na kuwa mtu bora. Lakini mwanaume anasema hana muda. kwake mafunzo sio kitu, lakini kwa mke ni kitu kizuri katika maisha yake.

Kwa mtindo huo  ni ngumu kumbadilisha mtu. Kwa sababu  unaweza kubadilika wewe sio kumbadilisja mwingine.  Anaweza kupata njia nzuri ya maana  na kutaka kujitenga na mahusiano kwa kutumia akili bila  ya ugomvi ili kuepukana na  stress nyingi, huzuni, magonjwa ya moyo, kisukari. Anaweza akaanza kujitahidi kufanya kazi zake, bila ya kumjali mwenza wake, au kuamua kuondoka

Sio kila mahusiano yanaweza kufika mwisho mzuri, mahusiano ya aina nyingi yanadumu kwa maumivu mengi. ingwa kuna machungu kwa kila mtu, lakini wanaweza kushukuru kwa  kushirikiana pamoja kwa upendo  na amani katika kufahamu  na kuelewa maana ya kuwa wawili  ni katika kukubaliana mkono wa kwanza kwa kila mtu kufahamu shauku, kusaidiana, mahitaji  ya mwingine  na kubebeana mizigo.

Toa maoni yako hapa chini kusaidia wengine.

Kisha Subscribe  ni bure kabisa  ili kupata nakala mpya kila mara.

Mungu akubariki unapofanya hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here