Kufikiri Nje Ya Box Imepitwa Na Wakati. Badala Yake Fikiri Kwa Mapana Ya Hali Ya Juu


slide_3 Kufikiri Nje Ya Box Imepitwa Na Wakati. Badala Yake Fikiri Kwa Mapana Ya Hali Ya Juu

Wakati wowote ninaposikia  mtu anasema fikiria nje ya box”, huwa nashangaa kwa nini  kuna box  kwanza. Binafsi, huwa sifikirii ndani ya  box. Sifikirii nje ya box. Hata sijui  box liko wapi.

Tunajifungia wenyewe kwenye box. Tunapofanya hivi, tunashindwa kuona tatizo liliko nje ya box. Kama umejifungia mwenyewe ndani ya box, kwa urahisi tu ondoka ndani ya box. Kwa upande wangu mimi viko vitu ambavyo vinanisaidia  kuondoa box.

Mbinu hizi zinaweza kukubadilisha unavyowaza , lakini pia zitakuwesha kupangilia mtazamo wako  kwa ajili ya mabadiliko na kutatua matatizo. mbinu hizi zitakufanya ufikiri nje ya box wakati mwingine.

Kufikiri Kuponya Sio Kutibu tatizo

Kutumia Akili Ya Mbinguni sio akili ya Dunia

Kuponya Akili  sio kutibu akili.

Ukiona unateseka ndani ya box ulilojifungia mwenyewe, jua kwamba umeruka maandiko, Umesahau , au hujafundishwa kitu.

Inawezekana kabisa kuwa umetumia akili ya kidunia  sio akili ya mbinguni. Na kila wakati unatibu akili yako badala ya kuiponya akili.

Kama umemwacha Mungu , umejifungia  mwenyewe ndani ya box. Kwa sababu unatafuta pesa kwa ajili ya kutibu umaskini. Unatafuta pesa kwa ajili ya Kutoka ndani ya box, hutaweza kutoka ndani ya box kama utabaki na akili hio hio ambayo ilikuingiza ndani ya hilo box. Ni lazima utumie akili nyingine ili uweze kutatua tatizo.

Ukianza kumtafuta Mungu utaanza kuponya Umaskini, utatoka nje ya box na kuliona tatizo lako, vinginevyo  hutaweza kutoka hapo kama utazidi kutumia akili  iliyokufanya ujifungie kwenye box.

Umaskini ni ugonjwa  kama magonjwa mengine. huenda umejifungia kwenye umasikini , huna tofauti na mtu mwenye sukari, ukimwi, saratani, ukoma, kipofu au kiziwi.

Huenda wazazi wako waliruka maandiko ndio maana unateseka.  Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Wazazi kama walikataa maarifa Mungu aliwakataa kuwa makuhani  wake. Na Kwa kuwa waliisahau sheria ya bwana ndio maana na wewe umesahauliwa. umejifungia mwenyewe ndani ya box.

Sasa basi ukiwa humo ndani ya box , jitahidi ugeuke uione njia ya kutoka, anza kufikiri kwa kutumia akili ya Mungu. Anza kutumia muda wako wa masaa 24 vizuri. Mungu ndiye ataweza kubadilisha maisha yako , hasa kwa nyakati hizi, huna ujanja mwingine  .Ukiweza kuponya akili yako utatumia muda wako vizuri, utajua namna ya kununua muda na kuuza muda.

Kazi Ya Muda.

Ni Kufikiri

Kutafuta Wazo

Kutafuta taarifa sahihi.

Kazi ya Pesa ni kuokoa muda.

Ukitumia muda wako vibaya utapoteza. Ukipoteza muda na wewe unapotea.

Ukiwa na muda msafi utakuwa na akili nzuri. Lakini ukiwa na muda mchafu utakuwa na Akili chafu. Okoa muda , changanya Elimu yako na Imani.

Mbinu hizi ni nzuri lakini zinahitaji zoezi la kila siku ili upate uwezo wa kuondoa uchafu ndani ya akili yako iliyokuweka ndani ya box na kushindwa kuona tatizo lililoko nje ya box. Acha kupoteza muda kwa kusubiri mtu aje akutoe humo , Tumia nguvu zako , akili ya Mungu, itakutoa hapo.

Mara utakapogundua thamani yako, utaweza kuongeza thamani ya kazi yako. utatumia ujuzi wako . Natumaini mbinu hizi zitakuwezesha kuanza kuona tatizo  , utatoka ndani ya box ambalo ulijifungia mwenyewe na kujiingizia matatizo.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Vita Ya Ndani Isikufanye Ujisikie Mpweke Kupitiliza
Next Jinsi Ya Kutafuta Mume ,Mke Kwa Njia Ya Mungu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.