Tunapoongea kuhusu furaha, Tunafikiria kukaa na furaha kila wakati –kila siku. kila dakika bila ya mashaka. Tunajaribu kufikia hali hii ya Furaha kama ndio lengo letu. Na kuepuka kila kitu ambacho kingeweza kuondoa hio furaha.
Lakini kuna maana gani katika aina hii ya furaha? ni kama chakula chako kizuri ukipendacho. Kwa kadri unapokuwa nacho ndivyo unajisikia vizuri zaidi. kwa maana nyingine, wakati tu unapokuwa na nafasi ya kula , ndio wakati unapookoa kila kitu. kwa hio ni chakula tu ndio kinakupa furaha hio, au muda unaopata wa kutafuna chakula chako?
Tunatakiwa kukumbuka mara zote kwamba ni katika uzoefu wa masikitiko tu ndipo tunaelewa kwamba furaha ni muhimu kuwepo.
Kufikiria kuwa wengine kila wakati wana furaha ni kutokuelewa jinsi furaha ilivyo.
Watu wengi hufikiria kuwa wale wenye maisha mazuri ni watu wenye furaha kila mara. Tangu wakiwa wadogo, tunakimbiza kupata furaha baada ya kuona maisha ya wengine yalivyo, kwenye mitandao kila mtu hutaka kuonekana vizuri kuliko uhalisia wake, pamoja na sisi wenyewe. kwa hio ni rahisi kuwa kwenye mtego wa kukimbiza furaha ambayo tunataka iwepo kati yetu.
Katika Uhalisia,Kila mara kunakosekana kitu fulani,au kitu fulani hakipendizi.
Hakuna mwenye maisha sahihi. Hata wale ambao unaona wako juu kuliko wewe. Hata mabilionea, Kila mtu ana changamoto zake na matatizo yake .
Unapokuwa negative, Unalenga vitu vidogo ambavyo haviko kwenye mstari. Hata mimi nimekuwa nikishughulikia matatizo mengi , na hata mengine kuonekana kuwa ni magumu. Kwa wakati huo unaweza kuona kama kila kitu hakiwezekani. Lakini kumbuka kuwa kila kitu kitapita. inaweza kuchukua wiki, mwezi, na hata miaka ukawa bado upo kwenye ups and downs.
Unatakiwa kutazama mbele . kutazama nyuma sasa , mambo mengi hayo, makubwa sana, yatakuwa yamekupa uzoefu. ukianza kuyakumbuka wakati ambao tayari umepita , utajisikia kutabasamu.
Acha kujaribu kuwa na Furaha .Kuwa tu mwenye furaha.
Ni kawaida kutaka kuwa na furaha kwa kadri iwezekanavyo. Kwa hio tunafanyaje? Kwanza, Tupa mbali imani kwamba kuwa na maisha sahihi ni kuwa na furaha.
Binafsi , ningekuwa na matatizo kama kila kitu kingekuwa sahihi. Ni kutokana na uzoefu wa maumivu ya maisha na changamoto ya maisha inayotufanya tuwajali wengine wakati wanapitia uzoefu wa majaribu kama yetu.
Kama maisha yangekuwa sahihi, ungeweza kutambua .Kama maisha yangekuwa sahihi , usingeweza kukua.
Kuwa na furaha ya kweli, Acha kukimbiza furaha ya kudumu.
Inakuwa kama kitendawili. Ninachomaanisha hapa ni kwamba , Kubali unapokutana na ups and downs katika maisha yako. Kwa uangalifu elewa kwamba furaha ina matukio positive na negative.
Elewa umuhimu wa shukrani. Badala ya kukazana na nyakati mbaya kwa sasa, achana nazo, kumbuka wakati unapokuwa na kitu na wakati ambao huna kitu. Napenda kufikiria kuhusu kazi yangu kwa mfano. Nilipokuwa sina cha kufanya nilikuwa sielewi , na nilikuwa nafikiria kila mtu ana maisha mazuri isipokuwa mimi.
Lakini nilipokutana na kusudi la maisha yangu, nilifurahi sana, hata kabla sijatambua kama nimefanikisha. Kumbukumbu kama hizi zitakufanya uwe mwenye shukurani kila mara , hata kama unapita katika majaribu .
Furaha na huzuni ni kama ndugu, vipo pamoja.
Vinapokuja vyote hapa ni hivi: Maisha yako yatajazwa na uzuri, furaha na nyakati nzuri. machozi ya furaha, kupiga kelele na historia za kuchekesha.Lakini pia maisha yako yatajazwa na mvua na dhoruba ambazo unaweza kuona kama hazipiti wakati unapopambana nazo.
Lakini vyovyote vile, Fahamu kwamba yote hayo ni maisha. Uwe na furaha wakati wa furaha na inapokuja huzuni , huzunika pia. Usijaribu kuepuka. huzuni au negative experiences, na kuwa kipofu wa kukimbiza furaha.
Mwisho utakuja kufanikisha hatua ya kweli katika maisha . Yenye maana na mafanikio mazuri. kuwa tayari kutengeneza maana hio kamili katika kukua katika matukio yote positive na negative– huo ndio ukweli wa maana ya Furaha katika maisha.
Toa maoni yako kusaidia wengine. kisha like page yangu.