KUNA UMRI SAHIHI WA KUBEBA MIMBA?


pregnant-teen-large_trans_NvBQzQNjv4BqpJliwavx4coWFCaEkEsb3kvxIt-lGGWCWqwLa_RXJU8 KUNA UMRI SAHIHI WA KUBEBA MIMBA?

Inapokuja wakati wa kupata watoto,  kuna vitu vingi vya kuangalia : Nina afya nzuri na nina uwezo wa kutunza mtoto? Nimepata mwenza sahihi ambae hataweza kuniachia mzigo wa matunzo? Niko tayari na ni muda sahihi?  Ni maswali yenye utaa kidogo yanaweza kukupa maumivu ya kichwa wakati mwingine.

Hakuna mashaka kabisa kwa mama mwenye umri wa kufaa na mwenye afya  kuwa na mtoto mwenye afya— kwa hio yote haya ni chini ya  msukumo wa muda , kukuongoza kwenye  miaka 30 ya  mwanamke  ya kuanza  kuwa na hofu.

Lakini umri kweli ni kigezo  cha muhimu  wakati unapohitaji kupata  mimba na mtoto mwenye afya? Kutokana na utafiti mpya , na hata mimi siamini hili.  Umri ukifika  miaka 35 unakuwa umepitwa na wakati wa kuzaa. Lakini nijuavyo mimi wanawake wenye umri mkubwa kama huu wa 35, 40 wanazaa watoto wenye afya nzuri  na kuwa na watoto wenye mafanikio makubwa.

Kuwa mama  mzima kiumri sio kama miaka 50 iliopita

Mtoto kuwaje ni kutokana na tabia za kiafya za wazazi  na mfumo wa maisha walionao, haijalishi  umri  mkubwa , lakini chini ya miaka 20 nayo kidogo  inanipa wasiwasi, sio kwa sababu hawezi kuzaa ila ni kutokana na akili ya mama ya kulea huyo mtoto. .

Utambuzi mzuri  wa mapema  katika maisha ni njia nzuri ya  kuweza  kuwa na mafanikio ya  na sifa nzuri  kwa ajili ya maisha ya baadae ya mtoto pamoja na  kufanikiwa katika Elimu, kazi na afya nzuri. Kwa hio ni muhimu kama mtoto ataweza kuzaliwa na mama mwenye umri wa miaka 25, 29, 35, 49. Lakini pia kuna changamoto katika umri huu wa miaka 35–49. Kulingana na wachunguzi wanasema kuwa ni muda mzuri wa mama kuanza kupumzika na kujenga afya yake  na kula matunda ya kazi zake alizokuwa anahangaikia miaka ile ya  kazi nyingi. 

Afya ya mtoto ni muhimu zaidi kuliko umri wa mama

Afya ya mama na sifa ya maisha yake ni muhimu zaidi kuliko umri wake,  miaka ya nyuma  wamama wakubwa  hawakuwa na pesa , lakini walikuwa na watoto wengi, na walikuwa na maisha ya chini . lakini siku za leo , wamama wenye umri mkubwa  ndio wenye kuwapeleka watoto wao shule nzuri,  wanajua kuwawekea watoto wao maisha mazuri , kazi nzuri na wakati wa ujauzito  huwa hawajishughulishi na  kazi nzito.kwa hio kama umri ni sababu,  sio sababu hio peke yake.

Kitu kimoja tu wanawake huwa hatukiwezi , muda  hausubiri.

Kando ya ushawishi  wa wanawake wengi,  mafunzo haya ni kuhusu kukua katika  kuonyesha mwili wako ukiwa na  afya unayoijali na kuchukua kipaumbele  cha mwili wako katika umuhimu wa afya  kulingana na umri wako. Na hio ni habari njema ,  kwa sababu hatuwezi kuzuia muda ,  lakini tunaweza kufanya mengi kuhusu sisi wenyewe ili tuwe na afya njema na  kuandaa maisha mazuri ya watoto wetu.

Umeipenda hii makala? unaweza kutoa maoni yako hapa

Previous KUTEKELEZA AZMA YA FURAHA NI CHANGAMOTO KUBWA MAISHANI
Next UTUNZE UBONGO UWE IMARA KIAKILI KWA AJILI YA MAISHA YA BAADAYE

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.