Mambo yote mapya tunayoyaingiza ndani kutokana na hali ya mitandao iliopo, tunatengeneza hali ya akili yenye hofu na kutuweka katika hali ya kujilinda.
Tunaishi katika kujihami kwamba huenda kuna kitu kibaya kinaweza kutokea. tumekuwa na hofu hii kwa sababu hatuaminiani kila mtu. tunaogopana sisi kwa sisi na kujiogopa wenyewe.
Hatukuzaliwa hivi. Sio kusudi letu tuliloijia katika Ulimwengu huu ili tuishi kwa kuogopana. Tumekuja Ulimwenguni tuishi kwa kupendana, kumpenda Mungu.
Ili tuwe kamili , lazima tuwe na akili ya wazi ya kujua sisi ni kina nani na kuelekeza nguvu hizo katika Upendo na sio hofu.
Inatokea Nini Tunapoonyesha Hofu Na Hasira?
Tunazo silaha zote tayari za kuonyesha Ulimwengu bila ya hofu. Tunao uwezo wa kujali, Kupenda, Kusaidia, Na kuwa na kila kitu.Tunafanya hivi vitu muda wote maishani mwetu. Bado hatutumii zawadi hizi kiroho tunapozihitaji. Tunakuwa na hofu kwa sababu tumesahau ukweli wa ndani kwamba ni sisi. Sio kusema wewe, Ambaye umeteseka,sio kusema wewe ambaye umepotea, na wala sio wewe ambaye umefanyiwa vibaya. Ni sisi ambao tumepotea, ni sisi ambao tumeteseka, ni sisi ambao tumefanyiwa vibaya.
Maisha mara zote ni kukutana na watu, na watu ndio watakaokufundisha jinsi gani utaweza kujishughulikia mwenyewe. Umeona mifano mizuri hapa?
Unapokuwa hujui jinsi ya kuipenda nafsi yako, utakuwa unajiona hauko salama, Na nguvu hii utaitumia kwa wengine unapokuwa unawazungumza nao.Tena nimewahi kuona watu wanaopenda kuwadhibiti wengine kwa sababu wanajiona hawako kamili, na hawawezi kujionyesha jinsi walivyo. huenda ni kwa sababu mitazamo yao ni tofauti au hawako tayari kuonyesha ukweli wao.
Kuna mahusiano mangapi ambayo yameharibika kwa ajili ya hili, kwa sababu tu ya mtu kutokumkubali mwingine jinsi alivyo? Ni mara ngapi tumejaribu kutaka kumbadilisha mtu kwa kutowakubali jinsi walivyo?
Badala ya kujitahidi kuwaelewa tabia zao, mila zao, tofauti zao, tunawahukumu, tunawalaumu. Hii yote ni kwa sababu ya kuwa na hofu badala ya kuimarisha upendo.
Jinsi Gani Utaonyesha Upendo Na Ukweli?

Maisha ya siku hizi, Utamaduni wa leo, Kuna mchanganyiko wa watu mbalimbali , backgrounds zao, mitazamo yao, Imani zao na waliokuja navyo. Tuna maamuzi ya kumpa mtu uhuru wa kuonyesha ukweli wake bila hofu, hukumu, au kulaumu. Na pia tunayo maamuzi ya kwetu wenyewe kuonyesha ukweli wetu, hatuhitaji kujidharau jinsi tulivyo. tusijiwekee mipaka ya kuonyesha upendo.
Kumbuka hata kama ukiwa na mtu ambaye umetoka naye kabila moja, kama hamtaonyesha ukweli ili kumfanya mwingine awe na furaha, mahusiano huwa sio mazuri. Tumekuwa tukikataa ukweli toka tukiwa wadogo, ukweli wa kujitambua sisi ni kina nani.
Wewe Ni Wa Kipekee jinsi ulivyo, na hata mwingine pia ni hivyo hivyo.
Nasema hili kutoka ndani ya moyo wangu: ACHA IWE HIVYO. Acha mtu awe jinsi alivyo. Uko hivyo ulivyo. Acha mwenza wako aonyeshe ukweli wake.Usijifiche jinsi ulivyo ili kumfanya mwingine apate furaha. Fahamu kuwa hutakiwi kuchagua Hofu kama ndio kitu cha kutofautisha.
Sisi inakuwa na nguvu, wakati wewe inapokuwa na hekima. Ni vizuri kudumisha upendo tulionao ndani yetu. Upendo tulioumbiwa wa kujipenda na kuwapenda wengine.Kama ukitaka kumbadilisha mtu utateseka. Na wakati mwingine ukitaka kujibadilisha wewe mwenyewe utateseka.
Hutaweza kuona simba atake kumbadilisha Tembo awe tofauti na alivyo. Anaheshimu mazingira hayo. Inafahamika kuwa tembo hawezi kuwa simba kama hatachagua kuwa tembo. Inaeleweka kuwa Sisi. inaeleweka ilivyo , acha iwe hivyo ilivyo. Kama muumbaji angetaka vitu vyote vifanane , Angefanya hivyo. Lakini alifanya hivyo kwa sababu kila kitu alikiona ni kizuri na cha kipekee.
Ulivyo umekamilika, na kila mtu ndivyo alivyo ni mkamilifu. Furahia maisha yako, mpende mwenza wako jinsi alivyo. wapende wengine jinsi walivyo.
Umependa makala hii? shirikisha wengi.
Subscribe kupata makala mpya.
Mungu Akubariki.