Kuwahi Au Kuchelewa Kuoa Na Kuolewa, Wapi Kuna Faida?


1-3-2 Kuwahi Au Kuchelewa Kuoa Na Kuolewa, Wapi Kuna Faida?

Hakuna Muda Mbaya wa kufanya mambo sahihi.

Kuna muda sahihi wa kuoa au kuanza mahusiano ya kudumu? swahi hili nimelipata kutoka kwa mteja wangu mmoja. 

Iwe  kuoa mapema au kuolewa , kwa muda sahihi, au kwa kuchelewa kulingana na umri wao.  Tofauti hizi zinaweza kuonekana kutokana na ustawi wenyewe.

Ingawa watafiti wamegundua kuwa watu walioko kwenye ndoa wanaridhika zaidi ya wale ambao ni single au wenye talaka, bado kuna utata kwa nini iko hivyo. Au ni kwa sababu watu ambao ni positive ndio wanakuwa na ustawi mzuri  katika  maisha ya ndoa au ndoa yenyewe ndio ina ustawi huo?

Reltionship-Kitchen-Duties-KOKOTV5 Kuwahi Au Kuchelewa Kuoa Na Kuolewa, Wapi Kuna Faida?

Lakini neno la Mungu linasema; vitu vyote ni halali , bali si vitu vyote  vifaavyo, si vyote vijengavyo. mtu asitafute faida yake mwenyewe.

Watu ambao wameachwa mara nyingi hupata   Huzuni na kuwa wenye stress nyingi. ndio maana inashauriwa kuwa ni bora kama ana nguvu aolewe au kuoa tene.

Lakini hata hivyo kuna vipengele vingine  ambavyo vina faida  ya ustawi katika ndoa , kwa kadri watu wanavyokua pamoja.  kunakuwepo na uzoefu  wa muhimu kwenye mabadiliko ya maisha  kama kutoka ujana kwenda hali ya utu uzima. wakati huo wanaweza kuanza kuchukua sheria mpya  na kujikuta wanashughulika zaidi na mambo ya  familia na ya kijamii.

56d50e_cf9a7b115096403dab86cbcde8013c12-mv2-1024x682 Kuwahi Au Kuchelewa Kuoa Na Kuolewa, Wapi Kuna Faida?

Lakini kama ukiwa katika umri wa kawaida , utakuwa na majukumu ya kutunza mahusiano ili yaweze kudumu ili kuepukana na aibu kwa mila zingine.  Na hii ni wale ambao wanaamini kile walichoambiwa kuwa ni aibu kuharibu mahusiano , ndoa yako. kwa hio inabidi kuvumilia yote ili kudumisha ndoa.

Umri wa miaka 19, 20, 22 na 25 ndio umri mdogo  ambao ni wa kuwahi kuoa na kuolewa. na umri kati ya 32 na 43, hawa ndio walichelewa kuoa na kuolewa. hii ndio tofauti iliopo.

Lakini pia hapa kumegawanyika katika makundi matatu tena, kwa wale waliowahi sana  ni wale walio chini ya miaka 23 kwa wanawake. On time ni miaka 23 na 27.  waliochelewa kawaida ni miaka 27 na 30 kwa wanawake.

Kwa Wanaume  waliowahi ni miaka chini ya 26,  on time ni miaka 27 na 30, na waliochelewa ni  baada ya miaka 30.

MATOKEO.

Wale ambao wanawahi kuolewa na kuoa wako kwenye hatari kubwa ya kuachana , lakini wale ambao wanaolewa na kuoa on time mara nyingi wanafikia umri wa kati bila matatizo  na watakuwa ni wenye heshima katika mahusiano yao , hawana shida ya kipato.  Na hata wale amabao wamechelewa kwa sababu nzuri , kama kutafuta shahada, kujiimarisha kiuchumi wataishi vizuri na kuwa na mahusiano mazuri.

Wale wanao oana mapema wanakutana na changamoto nyingi . hasa katika majukumu ya kuanzisha familia  na kuwa na familia kubwa ya ndugu wengine.  hawatakuwa na muda wa kusoma zaidi  na kufikia malengo yao  au katika kazi wazipendazo. Pia kuoa mapema unaweza kupata pressure kutokana na wanafamilia na kubeba mimba zisizotarajiwa, kitu ambacho kitakupa msongo mkubwa wa maisha.

Kwa sababu unakuwa bado hujakua kiakili binafsi ,hujakaa sawa kimwili, kiakili,na kiroho. itaonekana kuwa umechukua maamuzi magumu ambayo  huna ufahamu nayo. umeingia kwenye ndoa ukiwa giza.  huenda ilikuwa ni tamaa tu imekupeleka.  ulitawaliwa na mwili.

Sio watu wote ambao wanaoa mapema wanakutana na matatizo haya, lakini  asilimia kubwa ndio hivyo.  Napendekeza watu kuoa na kuolewa on time. Na wakati ambao umefahamu kusudi lako , wakati ambao umetambua kuwa sasa unaishi. wakati ambao una ufahamu wa kutosha.  Umeshajua kupigana na ujinga. Ili kupunguza hatari ya kukutana na magonjwa ,talaka na hata kuishi kwa taabu maisha yako yote.

Kaa chini sasa anza kuangalia maisha yako hapo ulipo ni kitu gani kimekukwamisha usiweze kusonga mbele.

Ukioa kwa wakati au kuchelewa na ukiwa tayari unaishi. utakuwa mtu mwenye afya, furaha, na utele .

Sababu Za Kawaida Kabisa Ambazo Zinaharibu Mahusiano

Mwanaume Anaposema Hataki Kuoa , Mwamini

 

Previous Usidate Naye Kwa Sababu Tu Ya Upweke Ulionao.
Next Aina Ya Upendo Unaohitaji Kusubiri Uje Kwako

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.