Kwa Nini Mungu Alimtengeneza Mwanamke Kutoka Katika Ubavu Wa Mwanaume


1 Kwa Nini Mungu Alimtengeneza Mwanamke Kutoka Katika Ubavu Wa Mwanaume

Inashangaza jinsi Mungu alivyomuumba Mwanaume, Na Inapendeza jinsi alivyomtengeneza mwanamke!

Kwa nini Mungu Alimtengeneza mwanamke kutoka katika ubavu wa mwanaume, Wakati huenda iliwezekana kabisa kumuumba kama alivyofanya kwa Adamu kutoka katika udongo?  hii ni sababu ambayo inagusa uzuri:

Alipoumba mbingu na Nchi alitamka neno. Wakati alipomuumba Adamu ,Alimuumba kutokana na mavumbi, akampulizia pumzi ya uhai kupitia matundu ya pua zake. Lakini mwanamke Akatengenezwa baada ya  mwanaume kupuliziwa pumzi  kwa sababu pua za mwanamke ni nyepesi zisingeweza  pumuzi hio kubwa ya Mungu. Ilibidi mwanaume alazwe usingizi mzito kwanza  ili kuwepo urahisi wa kuchukua pumzi ya mwanamke kwa utaratibu. Alichagua mfupa ambao utaweza  kumtengeneza mwanamke, ilikuwa ni mfupa mmoja tu. Akachagua ubavu ambao utaweza kuulinda  moyo na mbavu za mwanaume na kumsaidia , Kama ilivyotakiwa kuwa.

1-1 Kwa Nini Mungu Alimtengeneza Mwanamke Kutoka Katika Ubavu Wa Mwanaume

Kutokana na mfupa huo mwanamke akatengenezwa.akampendezesha. Akampa umbo zuri la kupendeza. Tabia za mke ni kama za mbavu, hazina nguvu ,ni za kulindwa. Ndio maana mwanamke anatakiwa kulindwa na mwanaume, kwa sababu ni kiungo cha mwanaume. ni moyo wake. moyo wake ndio ustawi. mbavu zake zimeshikilia  pumzi ya maisha. Kwa hio kama zikivunjika itasababisha madhara makubwa kwenye moyo. Msaidie mwanaume kama ilivyotakiwa kusaidiwa.

Haukuchukuliwa chini ya miguu yake ili uwe chini yake, Tena hukuchukuliwa kichwani ili uwe juu yake, Ulichukuliwa ubavuni. upande  wake, ili uwepo  upande wake kuziba hio sehemu ulikotokea. Mwanamke ni malaika mkamilifu, ni mrembo, umekuzwa katika uzuri, ubora wa ajabu. Macho ya mwanaume hujazwa wakati anapoona moyo wako ulio wazi kwake. Macho yako, Usibadilishe,lips zako usibadilishe, mikono yako ni laini usiwekee mambo mengine. Uso wako usibadilishe. moyo wako uko karibu na mumeo, kwa pumzi zote na maisha yote, mnafanana .

Mungu anasema, Adamu alitembea naye kila ifikapo jioni , na bado alikuwa hasikii upweke. Hakuweza kumuona Mungu wala kumshika. Alikuwa akimhisi tu Mungu. Kwa hio kila kitu ambacho alitaka Adamu ashirikiane naye  ni kumfahamu Mungu, Akaamua kumtengeneza mwanamke: Katika utakatifu, katika nguvu zake, katika usafi, katika Upendo, Kwa ulinzi wake na kwa msaada.Mwanamke ni mtu muhimu  kwa sababu yeye ni kama Extension ya Mungu.

Mwanaume anawakilisha Image ya Mungu , Mwanamke –pamoja na hisia zake, anawakilisha ukamilifu wa Mungu. Kwa hio mwanaume Mpende mwanamke, mfanyie vizuri.MUHESHIMU.Kwa kuwa yeye ni dhaifu kwako. Unapomuumiza yeye unamuumiza Mungu. Kila unachomfanyia , Unamfanyia Mungu. Unapomuumiza moyo wake, unaumiza moyo wako mwenyewe. Unaumiza moyo wa baba yako na moyo wa baba yake.

35919008-cute-young-black-couple-hugging-at-the-harbor-Stock-Photo-1024x682 Kwa Nini Mungu Alimtengeneza Mwanamke Kutoka Katika Ubavu Wa Mwanaume
ukamilifu

Mwanamke msaidie mwanaume. Katika Upendo.muonyeshe nguvu ya hisia uliyopewa na Mungu.Kwa upole na utulivu, onyesha nguvu zako.Katika Upendo, muonyeshe kuwa wewe ndio ubavu wake, ndio unayemlinda.

Mwisho kabisa , Nasema . Mwanaume jitambue ukuu ulionao, nguvu ulizopewa na Mungu, mamlaka uliyopewa na Mungu. Mwanamke jitambue jinsi ulivyo na nguvu kwa mwanaume. Mungu anakuambia kuwa wewe ni Extension yake, wewe ni ukamilisho wake. Tambua nguvu uliyonayo mwanamke.

Mungu awabariki kwa kulielewa somo.

Subscribe ili kupata makala mpya kila mara.

toa maoni yako kusaidia wengine.

 

Previous Huyu Ndiye Msichana Anayejifunza Kuipenda Nafsi Yake
Next Mapenzi Mazuri Ni Ya Wakati Uliopo

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.