Kuwafundisha watoto kuchangia vitu na watoto wengine inweza isiwe na faida kwao baadae.
Tunatakiwa kufanyaje badala yake?
Tokea mwanzo tumekuwa tukifundsha watoto kucheza na watoto wengine vizuri bila ugomvi na wajifunze kuchangia vitu vyao .haijalishi awe na michezo ya aina ngapi, kama mtoto mwingine atachukua vitu vyake ni sawa tu achukue.
Katika hili kila mara wazazi wamekuwa wakiwatia moyo watoto wao kushirikiana na wenzao kwa kila kitu, kuwa na mda wao wenyewe na kuacha watoto wengine kuchukua chochote wanachohitahi kwao, ingawa, kuna utaratibu wa mila zingine zinazofundisha kushirikiana, hata hivyo inaonekana kutofautiana dhana ya ufundishaji kwa watoto wetu kuwa wema na lakini kuwa na uwezo wa kuzingatia, hii pia inajenga uwezo wa akili yenye ukarimu na uelewa kulingana na rika lao.
Kwa nini kuwafundisha watoto kushirikiana inaweza isiwe na faida kwao.
Ushauri kwa wazazi.
Ni vitendo vya mwanzo inawezekana bila shaka niwe nawafundisha watoto kushirikiana na wenzao! ,hata hivyo watoto wanahitaji kujifunza kwamba hawawezi kufanya vitu peke yao na wanahitaji kufahamu kuwa kuna wengine wanahitaji kutumia hivyo walivyonavyo. Lakini kwa kufanya hivyo tunawafundisha watoto somo sahihi?
Pamoja na kwamba ni kitu kizuri kwa mtoto uliemfundisha hivyo kumpa kitu anachokipenda mwingie, huenda ni kwa kujitolea au kwa kutoa chozi- kuna upande mwingine wa hiki kitu- ambacho tunawafundisha watoto kwamba ni sawa kumpa mtu kitu anachohitaji kutoka kwako eti tu kwa sababu anakihitaji. Kwa mafunzo haya inaonekana kama ”wanadaiwa” , kwa njia nyingine ni kutaka tu wapewe kitu. Pamoja na kuwa atazoea hali hio , lakini unawafundusha kuwa kila wanachotaka watapata. Hata kama alikuwa hataki chochote lakini itakuwa ni nafasi yake kutumia kupata kama watoto wengine wanavyohitaji kitu kwake na kuwapa.
Malengo ya hapa ni kwamba, mtoto ajifunze, kuelewa na kukua katika wema na kuwa watu wakarimu wanaoweza kukubali mahitaji ya wengine na kuendeleza sifa hizi mwanzo kabisa katika ukuaji wao kwenye mazingira waliomo.
Kwa kuwalazimisha kushirikiana na wengine , tunawajenga katika mawazo yao.
-Mjengee kushinda hisia mbaya kwa watoto wenzake.
– msaidie mtoto kujua jinsi anavyolia ili kupata kitu, ndivyo atakavyoweza kupata anachohitaji. Hio ni hali ya bidii ya kupata kitu.
-Wajue muda maalum wa kucheza, sio kila wakati.
-Wafundishe kujitolea, na kuwa na bidii kwa wanachokitaka.
Nini Cha Kufanya
Cha kufanya ni kuruhusu watoto wao wenyewe wajidhibiti na kufikiria , kuwaelewa wazazi. Mara nyingi tunaamini kuwa tunawarekebsha , na kudhibiti tabia za watoto kwa sababu ya kuelewa mazingira zaidi na hali zao kuliko kuwaelewa watoto wenyewe.
Kwa maana nyingine ni kuwaacha watoto wafanye maamuzi wenyewe wakati mwingine.
Kwa kufanya hivi watoto watacheza kwa furaha kwa muda uliowapangia, bila shinikizo la kuogopa kuwa wazazi wanawadhibiti katika maamuzi yao ya kutoa au kutokutoa walivyonavyo kwa wengine kwa upendo bila ya kulazimishwa. Huu ndio uhuru unatakiwa kumpa mtoto, kuendeeza uelewa na kuwa na hisia za kweli.
Na sio hivyo tu , lakini pia mtoto atajifunza kuwa nikimpa mwenzangu sasa na kuna wakati na yeye atanipa cha kwake kwa sababu atakuwa ameelewa hisia za yule mwenzake.
-Mfundishe mtoto kusubiri , akifahamu kuwa nae atapata muda wa kuchezea kitu cha mwenzake.
– mfundishe kuwa na subira na kwamba ni nzuri.
-Mfundishe kuwa hatakiwi kulia na kupiga kelele anapohitaji kitu. Kila mtu hupata na atapata kwa wakati mzuri.
-Mfundishe kuwa na mawazo mazuri kwa watoto wenzake. Yaani asiwaze kuwa hatapewa labda kama mwenzake anachezea toy, aelewe kuwa nae atapewa achezee.
-Mfundishe ukarimu wakati anapokuwa nacho basi akumbuke kuna mwenzake anahitaji.
CONCLUSION.
Kwa ujumla kuleta mawazo haya yenye mitindo tofauti ya wazazi ni kuongeza uelewa wa akili kwa watoto wakati wanacheza. Michezo ya watoto ni mizuri na ni wakati wa kujifunza kuwasiliana vizuri na mbinu hizi zinasaidia kuendeleza akili zao za uelewa na akili za kuwa na subira, ambazo ni msaada mkubwa kwao kukabiliana na hali ya baadae wakikua.