Kwa Nini Unadhifu Wa Mwanaume Humfanya Kuwa Mwenza Mzuri


ChrYcflUYAEGgcO Kwa Nini Unadhifu Wa Mwanaume Humfanya Kuwa Mwenza Mzuri

Unadhifu wa mwanaume ni ubora wa mahusiano yako.

Kuwa na mwanaume mwaminifu  unaweza kuwa na mahusiano ya kudumu. Inapokuja kuchagua mwanaume ni bora kujua  aliye smart kiakili.

Uwezo wa mwanaume smart ni katika kutengeneza uchumi ulio bora. ni yule ambaye ana maono  makubwa , maono ambayo hayana longo longo.  Nikiwa na maana kwamba ana kazi ambayo Mungu amempangia, Mwanaume Nadhifu  ni yule mwenye kumjua Mungu, Anayesoma  Neno la Mungu. Haijalishi . Uwezo alionao, lakini anasoma Neno la Mungu.  Hajilinganishi na mtu mwingine, Kimavazi, kiuchumi, Anajifahamu kuwa yeye ni Agizo la Mungu . Mtu anayeweza kumlinda mwanake. Mtu mwenye Akili kubwa, Mwenye afya nzuri, yupo  uweponi mwa Mungu.

Utawala wake ni dhahabu safi. Anawafanyiwa watu kitu ambacho yeye anataka kufanyiwa. ni mwenye huruma. mtu asiyelaumu,  mtu anayeachilia na  kuwapa watu vitu.

Ni agizo la Mungu.  ni  mtu mwenye kumpenda Mungu kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote na kwa akili zake zote. Anampenda jirani kama nafsi yake.

black_businessman Kwa Nini Unadhifu Wa Mwanaume Humfanya Kuwa Mwenza Mzuri

Ni amri ya kwanza pamoja na Ahadi.  kwa kuwa yeye ndiye aliyechaguliwa wa kwanza ili  awe mtakatifu na mkamilifu katika Upendo . mtu mwenye hekima. kwa kuwa hekima ni ulinzi na  ubora ni katika maarifa. mtu mwenye kuwekeza muda wake katika ulinzi wa Mungu.

Viko vitu ambavyo vinaharibu watu. Pombe , Sigara, Umalaya. Mpira, Tv. Smart phone. Vyote hivi vinachukua watu. Mtu ambaye anajiepusha na haya ni mzima.

Mtu mwenye mamlaka kubwa. Hakuna ufalme bila watu.  mwanaume mwenye kuwafundisha watu habari za uzima wao, habari za kufufua akili zao, kazi zao, ndoa zao, maisha yao , imani zao kwa Mungu.  kuaambia watu wasiwe na hofu,  wawe na amani .

Mtu anayemuweka Mungu mbele. haishi kwa woga, anaishi kwa upendo, mitazamo mizuri. ana ujasiri.  haishi kwa labda. kama ni No ni No. Kama Yes ni Yes.

black_man_praying Kwa Nini Unadhifu Wa Mwanaume Humfanya Kuwa Mwenza Mzuri

Wanawake huwataka wanaume smart kiakili, kiroho na kimwili.  Wale ambao wanajieleza wenyewe kitabia wanapokuwa wanataka mahusiano na ni wakomavu. Ndio wanaume ambao wanaweza kukaa katika mahusiano ya kudumu na wenza wazuri.

Kumbuka kuwa mwanaume hatakiwi kuoa kabla Mungu hajampangia kazi. Kazi ya kuajiriwa ni kibarua. Kazi hasa ya mwanaume ni ile ya kujiajiri mwenyewe, hio ndio kazi. Lakini kazi ya mwanaume mwingine hio ni kibarua. Kwa hio mwanamke olewa na mtu ambaye ana maono tayari.

Kazi ya mwanaume ndio ambayo inachagua mke. Mwanaume haombi Mungu ampe mwanamke , anamuomba Mungu ampe kazi kwanza. Mke mwema Mungu atampatia ambaye atasapoti maono yake.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

 

Previous Unawakumbuka Lakini Huwataki
Next Thaminisha Muda Wako Katika Mambo Ya Maana

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.