KWA NJIA ZIPI NILIACHA KUJARIBU KUDHIBITI KILA KITU KATIKA MAISHA YANGU.


Woman_biking_hero KWA NJIA ZIPI NILIACHA KUJARIBU KUDHIBITI KILA KITU KATIKA MAISHA YANGU.

Nilipokuwa mdogo, niliona kituko fulani vitu vidogo kwenda vibaya. Sijui ni kwa nini  nilikuwa na mawazo haya., lakini nilikuwa na wasiwasi mkubwa mno muda wote .Nilipatwa na ugonjwa mbaya wa kukosa usingizi kila siku.

Nilikuwa na tatizo la kupata haja kubwa,  na nilikuwa naogopa kila kitu , kuwa kitakuaje sahihi., na nilijifungia mwenyewe kwenye tatizo hilo kubwa lisilowezekana wakati huo wa udogo wangu na kuendelea.  

Haikutokea kwa sababu ya uzoefu wowote wa maisha,  na  ukweli sikuwa naweza kuona kama kuna  tatizo zaidi , mpaka kipindi  nilipofikia umri wa teenager, ndipo nilipoanza kugundua  ukosefu wa kuwa na mahusiano mazuri na wengine.

Kuanzia hapo,  nilianza kuwa na mahusano  zaidi na watu mbalimbali ambao walikuwa wanawezekana  kulingana na umri wangu.Na nilianza kuelewa matatizo yaliyokuwa yakitokea kwenye matarajio ya watu wengi. Nikaanza kuwa mtulivu zaidi  na  kuona jinsi gani watu hawawezi kufikia matarajio yao walioyaweka,  ili watulie angalau kidogo.

Ugeni wangu wa kutoka tu chuoni , nilikutana na neno locus of control, neno hili lilibadilisha  kila kitu kwenye mitazamo yangu , kwa kupitia mazoezi,  utulivu kwa kupitia tafakari,  nilijifunza mbinu za  jinsi gani ya kutuliza akili yenye wasiwasi, na ilinisaidia kutuliza wasiwasi wangu.  Pia nilijifunza jinsi ya kusikiliza mwili wangu,  na kuwa makini kwenye mawazo yangu yaliokuwa yakinidhuru.

Ilikuwa ni bora zaidi kuliko  kutazama hisia zingine za kudhibiti. Nilianza kutafuta utulivu wa ndani. Nilianza kusikiliza   jinsi gani najisikia, na kujiunganisha na hisia zangu. Ilinisaidia kuelewa  kuwa nilikuwa ni fikra zangu ndizo zilizokuwa zinanifanya nifikirie kuwa  nimetengwa na kila mtu.

Nimekuwa nikifanya hivyo kwa kipindi sasa, na nimeona kuwa ni kitu kizuri cha kuondoa msongo na wasiwasi wowote , kitendo rahisi cha kutulia kimya na kusikiliza pumzi zangu kwa muda wa dakika 15 mpaka 20 kwa mara moja kwa siku kimeleta  hali ya utulivu , amani ndani yangu kitu ambacho sikuwa nakifahamu  hapo kabla.

Baada ya muda, nimejikuta  naona maisha ni rahisi , hata kama  vitu havikufanyika  kwa kiwango nilichotaka.Nimeanza kuwa na uelewa zaidi  kwa watu wengine  na kuwaelewa jinsi  wanavyohangaika kutafuta usahihi katika maisha yao .

Nilipokuwa mdogo, sikuwa nahisi kutawaliwa na chochote,  nilitamani kukua  ili niishi kwa uhuru wangu na sheria zangu, niwe na nyumba yangu mwenyewe, . Nilipokua na kuondoka nyumbani , nilianza kutafuta amani yangu ambayo sikuwaza kama nitaipata. Kupitia  mafunzo ya   tafakari , mazoezi na usikivu mzuri, nilianza kupata nyumba yangu niliyokuwa naota, nilijikuta nikiwa mtulivu, nilikuwa  nafuata  sheria za kazi, kumheshimu bosi wangu na kuwaheshimu marafiki, na nilipata mahusiano mazuri  kwa kila mtu kwa sababu ya  kitu hiki kipya nilichokipata. Kilichonipa uwezo wa  kutoruhusu makosa  au matatizo yaniponde ponde.

Imekuwa ni muda sasa toka nimeanza  kubadilisha mitazamo yangu ya maisha. Nimetoka mbali, Lakini bado kuna matatizo yanayojitokeza ya hapa na pale , lakini ni rahisi kuyaachia yaondoke.  Nina furaha ya kutosha  katika maisha yangu ya kila siku, na kwa sababu  ninaweza kuachana na vitu vidogo vidogo,  nina uwezo sasa wa kutazama mambo makubwa  ninayotaka  yatokee maishani mwangu.

Kama umependa makala hii . toa maoni yako . kisha washirikishe wengine facebook.

Previous KWA NINI NI VIGUMU KUACHA KULA VITU VIDOGO VIDOGO USIKU
Next NJIA 10 ZINAZOFANYA NDOA YAKO KUWA NGUMU KULIKO INAVYOTAKIWA.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.