hqdefault Kwa Yeyote Ambaye Anapata Taabu Kujikubali

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wameshikiliwa sana na mambo yaliopita, Ni ngumu kwako kujikubali. Mambo mengi ambayo sio hata ya muhimu . Maamuzi yako ya sasa, Mchakato wa mawazo yako, tabia, mahusiano na kutazama katika uzoefu uliopita.

Mara kwa mara unajikuta unarudia hali yako ya zamani. Kila wakati unasema natamani kama ningekuwa kama mwanzo.  Kama tu ungekuwa na moyo kama wa mtoto mdogo. kama tu usingejali, kama tu ungeweza kurudi hali yako ya zamani.

Kama upo Hivyo ACHA.

Unaweza kuwa unaogopa sasa hivi. Kukubali  mabadiliko yaliopo kwako, lakini kitu cha kutambua ni kwamba unakua.  Kukua kwako ni katika njia ya kutojikubali.  Yaliopita ni mahali pazuri pa kupatembelea, lakini  ni mahali pa hatari kubwa .

Jifunze kujipenda jinsi ulivyo sasa. Tazama mambo kwa jicho chanya. safari yako,  hatua unazochukua kufikia  mahali ulipo leo. Watu wengine wanaweza wasione hili, lakini kutazama  watu kwa ajili ya kutaka kutambua hili katika safari yako, utajirudisha nyuma. Hutapata maendeleo.

Ndio. Ni wakati mgumu kwako wa kukubali kukua kibinafsi, lakini  ni vizuri kuanza kufanya zoezi la kujipenda, kujijali na kujikubali mwenyewe . Jione wa thamani, jione kuwa wewe ni jasiri, una Amani, na una furaha. Una afya na wewe ni mtu wa matumaini.

single-black-woman-alone Kwa Yeyote Ambaye Anapata Taabu Kujikubali

Unalo kusudi. Unayo zawadi uliyopewa na Mungu, lakini bado hujaigundua kwa sababu ya kukosa uwezo wa kujitambua. Unaweza ukakutana na changamoto nyingi ,magumu, kupoteza , lakini kumbuka kuna kuamka tena, hutaweza kulala moja kwa moja. labda kama utakuwa umeondoka Duniani.

Kila mtu yupo tofauti, kuna mnene na kuna mwembamba, Kuna weupe na weusi. Ukiweza kutambua jinsi gani kila mtu ni wa tofauti  utaanza kujikubali.Kuna mtu ambaye ni mwepesi kujifunza jambo jipya, lakini kuna mtu mwingine mpaka asukumwe kujifunza kwa faida yake mwenyewe.

Hivi hujawahi kujiuliza kwa nini watu wengine wanafanya vizuri na wakati hawana Elimu. Lakini wengi wenye Elimu nzuri hawafanyi vizuri katika mambo mengi?  Hujawahi kujiuliza kwa nini unarudia jambo hilo hilo kila mara wakati halina faida kwako? mimi nimewahi kujiuliza  zaidi ya miaka 20.

Akili inatawala kila kitu. Ina nguvu katika kila kitu.  tabia na nafsi yako.  Hukutakiwa kuonekana kama unavyoonekana,   hukutakiwa kujifananisha na ndugu yako au mtu mwingine yeyote. hutakiwi kuwa mtu mkamilifu kama unavyofikiria wewe.  Kilichopo ni kujikubali jinsi ulivyo, ubora uko ndani yako.  Hivyo ndivyo unavyotakiwa kujiona. Lakini  usianze kusema vipi kama  ningekuwa hivi kwa muda wote?  vipi kama majani  yangekuwa mara zote yanaonekana ya kijani tu yasikauke? ni kwa sababu utakuwa umesahau kujimwagilia maji wewe mwenyewe.

Mtu mwenye kujitambua  wakati wote atakuwa kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji , anazaa matunda kwa majira yake , na majani yake hayakauki, na kila analolitenda  kwake ni positive tu.  Furaha , amani, Upendo umejaa kwake. anajipenda na kuwapenda wengine, anajikubali na kuwakubali wengine. anajiheshimu na kuwaheshimu wengine.

Kwa hio Fanya Hivyo Leo.

Usitazame yaliopita kwa sababu yaliopita yanakuletea Huzuni, Usitazame yajayo kwa sababu yajayo yatakuletea  Wasiwasi. Wewe Ishi wakati uliopo , sasa hivi.  Ukweli ni kwamba hakuna mtu anaweza kuwa wewe.  Na hio ndio nguvu iliopo kwako.

Upendo.

Subscribe kupata makala nzuri kila mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here