To Do List 2018. Gods 24hrs Economy


Notes
journal-therapy-man-writing1 To Do List 2018. Gods 24hrs Economy
list

Uchumi wako una masaa mangapi?  Wewe ni mtu unayeandika kitu unapofundishwa? unasoma vitabu ? Unafikiri kwa muda gani? Unatafuta taarifa za kutosha? Unatafuta wazo ndani yako? 

Kitu gani unaweza kuonyesha ambacho tayari umekifanya kipindi chote cha maisha yako mpaka hapo ulipo sasa hivi?  Mungu huwa hampi mtu yeyote ambaye ni mjinga miujiza mikubwa zaidi ya uponyaji mdogo.

Muda ukitumika vibaya lazima utakuwa mtu wa madeni mengi, utakopa sana. Anza sasa kujiuliza tangu mwaka ulipoanza ni kitu gani umekifanya cha Mungu.

black-woman-writing-pf To Do List 2018. Gods 24hrs Economy

Uchumi wa Mungu ni masaa 24. Huenda kuna mtu amebeba majibu ya maisha yako, anza kuuliza maswali. Kama ukichezea muda wako ni ngumu sana kufanikiwa.

Kazi ya Muda.

1.Kufikiri. jiulize umewahi kupata nafasi ya kukaa mahali na kufikiri  kwa dakika kadhaa? kama hujawahi wewe hujaanza kuishi bado.

2.Wazo. Mawazo yako unayopata , unayaandika au kuchora mahali ili Mungu aone nia yako akusaidie kuvuka mahali ulipo?

3.Kutafuta Taarifa sahihi.  Unatafuta semina mbalimbali ili kujifunza, unasoma vitabu gani ambavyo vinaweza kukupatia  ufahamu wa kutosha,  Unasisikiliza kitu gani ili ujifunze , unatazama nini, kitu gani unakipenda na nini hukipendi.

Unataka kuwa na kampuni kubwa anza kutengeneza maneno kwanza. hakuna kitu kinachotokea kabla ya Neno. Simu inatengenezwa kwa kutumia kitabu chake.  Mungu aliumba Ulimwengu kwa neno. Gari inatengenezwa kwa kuanza na maneno ya kwenye karatasi kwanza. Mwanadamu ni kitabu chake cha imani.

Kama muda wako umejaa masaa 24, tazama huo muda unaufanyia nini?  Muda una nguvu, Heshimu muda. Mtu anayeheshimu muda huheshimika, huonekana kuwa ni wa thamani . Ukitumia muda vizuri utakubalika na Mungu pamoja na wanadamu.

Unachotakiwa kufanya leo ni kuandaa list yako ya 2018. Nimetamani nikusaidie kitu gani cha kuanza kwanza.

Kabla hujaandika mambo yako yote, Anza kuandika mambo ya Mungu. Andika vitu ambavyo utamfanyia Mungu , Kazi ya Mungu mwaka 2018. Ukimaliza hayo, Anza kuorodhesha ya kwako.

Put God First. 

1.

2.

3.

4.

5.

…………

Andika ya kwako.

1.

2.

3.

4.

5.

………

Unaweza kuandika list ndefu sana ya kukutosha wewe.  Nakutia moyo fanya hivyo  utaona mambo mapya yakitokea katika maisha yako.

Mungu Akubariki.

Subscribe kupata makala mpya

 

Previous Tofauti Kati Ya Uongozi Wa Kiungu Na Mwanadamu
Next Mapenzi Yenye Ushindi

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.