Ninachoka pale watu wanapokata tamaa bila ya kupeana muda wa kusameheana.
Kinachonichosha zaidi ni mtu kuamua kujinyonga kwa ajili ya kukataliwa. Nikiona hivyo naumia kwa sababu ya mtu ambaye amefungwa ufahamu wake . Akili yake imefungwa hawezi kufikiria tena, hawezi kuona picha nyingine mpya.
Akili yangu wakati mwingine inachoka ninapoona watu hawawezi kuwasiliana kama watu waliokomaa kiakili, kimawazo na kimatendo. Sipendi kuona mtu hawezi kukabili kitu ambacho amekifanya, badala yake ananyamazia na kujifanya hana habari nacho kumbe kinamuumiza.
Nachoka pale mtu ambapo hawi mkweli kutokana na hisia zake, kwa sababu ni bora kusema na kuonekana kituko kuliko kuficha hisia za kweli.
Inachosha zaidi unapoambiwa kuwa hukuonyesha kujali sana ili kuwa karibu au kuonyesha kitu kinachotakiwa kwa wakati huo. Nachoka kusikia watu ambao wanalinda mioyo yao kwa kuwasukumia wengine mbali ili wasiwe karibu yao.
Hali hii pia inanichosha , kuishi kwenye Dunia ambayo watu hawafix vitu kwa sababu ya kuogopa ukweli kwamba wamevunjika moyo. Upendo umejawa na mpasuko. Watu bado wanahitaji Uponyaji. unaweza kujiingiza tu kwa mtu unaempenda. utachanganyikiwa tu utakapokuta hakuna ukweli wala hisia ambazo ulizifikiria.
Utaenda kuogopa na kulemewa muda utakapofika wa kupata mtu ambaye anakupenda kweli. hutaweza kuwa mkamilifu katika hisia zako hata kama kutakuwa na pesa nyingi kiasi gani, haziwezi kujaza upendo unaohitaji. kumbuka kuwa upendo mzuri ni ule wa kujipenda mwenyewe. hapa hutaweza kuwa na kazi kubwa , utahitaji tu uvumilivu kidogo, utahitaji mtu wa kukaa naye. mtu ambaye atakuonea huruma unapochoka badala ya kukukatisha tamaa.
Kwa sababu ukweli wa mtu huonekana pale anapopenda. Hupona pale anapopata mtu wa kweli katika upendo, mtu ambaye atamkubali jinsi alivyo. hupata nguvu nyingi pale wanapotambua kuwa kuna mtu mahali anampenda na ameamua kukaa naye.
Lakini inapotokea kukatishana tamaa, huko ndiko kunakotokea wasiwasi, huzuni, kukosa usalama, kutojiamini na hujikuta hawezi kufungua moyo tena .Kuachana bila ya sababu nzuri, hicho kinawapa watu wengi maumivu makubwa ya moyo. Huwafanya watu washindwe kupenda tena. Hufanya watu waamue kuishi peke yako milele. Kukata tamaa ni mzizi wa ubaya wote. ndicho kinachoharibu uwezo mzuri alionao mtu.
Natamani kuishi wakati ambao kila mtu anapoona mtu amekwama mahali asaidiwe ili kuondokana na tatizo alilonalo. Lakini sasa inaonekana sisi wote tunaongezeana pressure kwa kila mtu.
Sasa wakati mwingine tunaitana ili kupotezeana muda, wakati mambo hayaenda vizuri. Tunaishi na kuwa na tumaini la kupata mtu sahihi, kwa sababu hatuna nguvu ya kufix au kumponya mtu mwingine. Hatutambui kwamba wakati mwingine hatuonyeshi sehemu ya uzuri wa mtu uliopo kabla ya kuelewa ni kina nani.
Wakati mwingine utakuta mtu anaelewa hisia za mtu, badala ya kujitahidi kukaa naye na kumwelewesha , anaamua kumuumiza kwa dharau . Tunaenda wapi, wewe unayefanya hivyo huoni kwamba unapanada mbegu mbaya?
Subscribe. Kupata makala mpya.