MAAMUZI YAPI YATAKUFANYA UBADILISHE MAISHA:


images-10 MAAMUZI YAPI YATAKUFANYA UBADILISHE MAISHA:

Kila siku umekuwa na mawazo ya kubadili maisha yako na kuna mambo ambayo unatamani kufanya ili ubadilishe maisha.Ni jinsi gani basi utaweza kubadili maisha yako?,kuna vitu vya muhimu vya kufanya ili uweze kubadilisha maisha yako. ili ufanikiwe  itakubidi ujifunze kusikiliza sauti ndogo sana  ilioko ndani yako.

Sauti hio huja kwa upole kiasi kwanza unaweza usijue kama ndio ili sauti unayotakiwa kuifuata na kuiamini. na hio ndiyo inayokuambia  kitu cha kufanya ili kubadili mfumo wa maisha yako. hapa naangalia zaidi katika mahusiano .

Kuna kitu nilijifunza  muda kidogo wakati napita katika mapito fulani katika maisha,  ya kwamba  wewe ndio kila kitu katika maamuzi, yaani wewe ndio Hakimu, wewe ndio Wakili wa maisha yako. Majibu yako ndani mwako una nguvu zote za maamuzi unayohitaji ya mabadiliko, shida ipo pale unajiamini vipi, kiwango chako cha kujiamini kipo vipi, ili kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Inabidi kujifunza zaidi bila ya kufuata ushauri wa watu wengine, ndio sikatai kuna ushauri mzuri kutoka kwa washauri mbalimbali, lakini maamuzi yako ya ndani ndio ya kufuata.

Maisha yako yatabadili maamuzi ya mahusiano yako.

Watu wengi wapo kwenye shida ya  mahusiano , na wamekuwa wakitafuta ni wapi pa kupata ushauri mzuri ili kudumisha mahusiano yao, kumbuka huwezi kushauriwa bila ya kutoa historia yako kwanza, na huyo mtu ambae atakupa ushauri hakufamu vizuri kama unavyojifahamu wewe binafsi.

Natoa ushauri wa mahusiano lakini ukweli ni kwamba sitaweza kukupa  maamuzi yeyote  kuhusu na maisha yako ya mapenzi, hio ni kweli. badala  ya kumwambia mtu afanyaje namtia moyo kusikiliza sauti iliyo ndani mwake, je utafanyaje?

SIKILIZA.

Mimi napenda kufanya mazoezi kila siku , napia napenda sana kumsikiliza Joyce Meyers, pia husikiliza  mafunzo ya  ya ujasiriamali , biashara na uongozi.lakini kila nikimaliza kusikiliza bado kuna sauti ile ndogo huja  na kuniambia nitafanyaje maamuzi yangu,pamoja na kuwa naandika haya , natamani zaidi kuwasaidia  wanawake wasikilize sauti ya ndani  katika maisha yao , kuwasaidia marafiki , na wengine wote kwa ujumla wake.

Sijasikia ni nini hasa nakijua ,NI nini Mungu ananiambia, vinginevyo nitoe yaliyoziba masikio yangu.

Je wewe unataka kufanya maamuzi gani? yanahusu nini, yawezekana uko ndani ya mawazo mengi ambayo unaona huwezi tena , mahusiano yako yako katika hatihati ya kuvunjika na wewe bado unayapenda,

CHUKUA MUDA  WA KUSIKILIZA SAUTI ILE YA NDANI

Kama kweli unahitaji kubadilika inabidi ujifunze kusikiliza sauti ya ndani  ile ndogo sana, sauti ya Mungu , itakuambia ni kitu gani cha kufanya

kaa na maamuzi yako.

niliokaa na kufikiria ni nini cha kufanya , nilipata mambo mengi , linakuja hili na hili , lakini moja tu ndio ambalo niliona lina nguvu, nilifikiri kuandika kuhusu wanawake na  hisia zao , na maisha yao,  nikafikiri kuandika kuhusu ni namna gani ya kufanikiwa katika biashara , lakini sauti bado ilikuwa  ikisema ndani yangu kuwa niandike kuhusu na  kuishi maisha Bora  katika kila nyaja ili kuweka usawa  (balanced life)

Hii inahusiana na  furaha, huzuni , ndoa , familia . mapenzi , kazi,mahusiano, maendeleo , yaani yote yanayohusiana na maisha ya mwanadamu. je wewe unafanya maamuzi yanayohusiana na nini?

Vuta pumzi kwa muda kidogo, halafu achia, sikiliza sauti ile ya ndani  sauti ya utulivu inayokuambia badilisha maisha yako, kaa na hayo maamuzi.

VITENDO.

Fanyia kazi maamuzi yako na kubaki nayo, hivi ndivyo unavyotakiwa  kuamua kubadili maisha yako, fanya kwa vitendo ingawa utakuwa kama hujiamini amini hivi, huna uhakika.

Uaweza kuanza kujaribu kuishi katika ndoa yenye upendo na amani hata kama hio ndoa ilikuwa katika hatari ya kuvunjika.na wakati huo huo ukiwa na muda wa kusikiliza sauti ile ya utulivu inayokuambia  usimwache mumeo , mkeo. na utakaa na maamuzi hayo ya kutengeneza ndoa iliyo nzuri zaidi.

Namna  gani utafanya ; utaendelea kujishauri wewe mwenyewe na engine utaenda kwa washauri wa ndoa, lakini jifunze  kubadili maisha yako ndani ya ndoa nzuri bila ya kukimbia , unaweza pia kuwa unasoma vitabu  vya namna ya kutunza ndoa na kuponya ndoa, mategemeo yako yatabadilika.

Ukitaka badili mawazo yako;

hujachelewa bado kuwa kama ulivyotaka  maisha yako yawe , bidii yako ya mabadiliko ndio majibu yako.

MASWALI KWAKO;

1.Kuna faida gani ya kutafuta ushauri wakati unapofanya maamuzi ambayo yatabadilisha maisha yako?

2.Umewahi kuambiwa kuwa kufanya maamuzi kunabadilisha maisha yako?

3.Utaenda kwa nani unapotaka kufanya maamuzi makubwa  ya mahusiano  na mapenzi?

Kama utafanya maamuzi yanayohusu mahusiano inabidi kujiuliza kwanza , naweza kuacha? inasaidia nini,

Siwezi kukupa ushauri wa jinsi ya  kufanya maamuzi ambayo yatabadili maisha yako, lakini nakukaribisha  utoe maoni na mawazo yako  .

how-to-make-a-decision-that-will-change-your-life MAAMUZI YAPI YATAKUFANYA UBADILISHE MAISHA:

 

 

 

 

Previous NGUZO 6 ZA KUJITENGENEZEA HESHIMA.
Next KWA NINI WANAUME WANAKUWA WASALITI KWENYE NDOA?.

2 Comments

  1. […] -maamuzi yapi yatakufanya ubadilishe maisha yako. […]

  2. […] -maamuzi yapi yatakufanya ubadilishe maisha . […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.